Magufuli is very RIGHT. Maisha yanaendelea. Tusitegemee serikali kutumia rasilimali zake kuwajengea nyumba wahanga. In fact to me, Magufuli angetumia hiyo hela ya michango kukarabati mashule, hospitali na barabara zilizo athirika. Na ndo inapashwa kuwa hivo.
Hili janga ni funzo kwetu sote. Jamani katieni bima nyumba zenu na other valuable properties (by the way bima ya nyumba iko chini mno). Tatizo waswahili kila kitu tunakifanyia mzaha tukitumia visingizio lukuki. Lakini kwa mwenye akili dunia ya leo huwezi kujenga nyumba yako kwa hizi hela za kuokoteleza...ukashindwa kuikatia bima.
Najua wengi tutapiga kelele tukisingizia umasikini (this is a popular excuse so far in our country).......lakini ukweli unabaki. Dunia ya leo...haina msaada tena! Ni jukumu lako kufanya uwezalo kujikinga na haya majanga yasiyotabilika (umeme, mafuriko, tetemeko nk). Ndo maana utakuta wazungu hata akizeeka hawi mzigo kwa ndugu au serikali. Au hata akifa...ana bima yake ya kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele. They always work hard and save for the rainy day!
Leo hii baadhi ya waTanzania wenzetu walioko mambelezz (au hata hapa nyumbani) wanatangulia mbele ya haki...tunaanza kupitisha bakuli! (kusafirisha mwili). This is bad and we should correct this culture. Kateni bima za maisha kwa uhai wenu, nyumba zenu na mali nyinginezo. Tuache hii tabia ya kuishi kwa kutaka kuonewa huruma na binadamu wenzetu. Undugu au urafiki haina maana kwamba tuwe mizigo kwa wenzetu.
Maisha yako. Jukumu lako.
Masanja