Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais yupo sahihi kabisa, hakuna haja ya unafiki. Wananchi waanze ujenzi wa nyumba zao sio kusubiri Serikali. Serikali na wahisani watasaidia si kwa asilimia 100 kiasi cha kuwafanya wabweteke kusubiri serikali.
Nani kabweteka anaisubiri serikali huku analala nje? Mnashangaza sana
 
Ndugu zangu wana bukoba poleni sana nimekaa nikafikiria nikatoka nje nikavaa viatu vyenu nimeona mko katika wakati mgumu sana najua mnachohitaji sasa ni faraja tu muwe Na amani katika mioyo yenu mpate nguvu za kuanza upya Na siyo matamko yeyote yasiyo Na faraja Machungu ya kupoteza wapendwa wenu Na kupoteza baadhi ya viungo Na Mali zenu ni makubwa sana Mungu awape uvumilivu Na roho za kusamehe kila baya litakalosemwa kwenu au maneno yanayowakera ili faraja na amani vitamalaki katika mioyo yenu ameni
 
Body language haiendani na yanayotoka mdomoni. Kama unazo japo akili kidogo tafakari,, angalia pia set nzima ya hayo makabidhiano. Angalia body language za wahusika wote.inahitaji akili kidogo kuelewa
 
Mwogope Mungu ndugu yangu....waliofikwa hawakupenda ndugu yangu.
Sasa kiongozi ulitaka Mh aongea vitu ambavyo hakiwezekani ili mkalili badae mje mnanga tatizo sisi watz tumezoea porojo ukweli hatutaki

Ebu nenda Kahama ulizia wale wahanga wa Ile mvua mwaka Jana waliambiwa maneno matamu ila je wamepata si bora mtu uambiwe ukweli ili ujiongeze tu

Mdogo mdogo tutazoea tu
 
Mimi naungana na mheshimiwa raisi , sababu unakuta mtu nyumba yake imeanguka ukuta upande mmoja tu lakini anadai hana chakula, maji, nguo, vitanda nk.Anataka asaidiwe na serikali vyote hivyo wakati migomba na maharage shambani haijaathirika.Nshomile ni wa hatari, wameona hii ni fulsa waitumie kukwamua mambo yaliyokuwa yameshindikana.
 
Katika kitabu cha mwanafalsafa Jean- Jacques Rousseau (1712-1778) aliandika namnukuu;

"..just as herdsman is superior in nature to his herd,so chiefs who are the herdsman of men,are superior in nature to their people,therefore Kings are gods or that men are brutes,he believes that men are naturally not equal,but that some are born for slavery and ohers for dominion"

Ikiwa Kweli Mungu wangemwamini ndani ya chama chao,wasingeishi kwa falsafa hii ambayo nikwa kila mwanaccm anapoona wenzake wanamatatizo anawatupia kila kauli anayoiona inawafaa maskini!!

Vitabu vya dini vinasema "..mtawatambua kwa matunda yao,je?, watu huchuma Zabibu katika miiba,au tini katika mibaruti?, vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mema,na mti mwovu huzaa matunda mabaya...hakuna mtumwa wala mtwana...( mathayo 7:16-18)

Ccm nakundi lao,inajiona imechaguliwa" the chosen one" ndio maana kila ajaye huja kama kondoo ila apatapo hugeuka na kuwa King John brother the song of Eleanor( 1189-1199)
Tusikubali
 

Dunia nzima majanga yapo kila siku, na mengine makubwa sana kuliko hili la Bukoba. Hata hapa kwetu yameshapita majanga makubwa pengine kuliko hili na kupoteza maisha ya watu wengi sana. Lakini mbona kauli za kukasirishana na kikatili kama hizi hatujawahi kuzisikia kote huko? Msipende kutetea kila kitu kama ile wanaokosoa ni maadui wa nchi hii, ni kukubali kuwa ulimi uliteleza au kashauriwa vibaya kutoa kauli hiyo
 
Kunufaika kwa Mwanasiasa yeyote nipale tu,Serikali iliyokabidhiwa dhamana ( mkataba wa o na serikali unaposhindwa kutekelezwa) kwa nini mpinzani asikumalize?
 
Nadhani wanachohitaji watu wa Kagera wakati huu ni misaada ya dharura. Nyumba ulijenga kwa miaka mitano leo unaanza upya sio kitu cha siku moja kwa uchumi wa Mtanzania, msaada wa hali na mali ni muhimu.
,
 
Bweteka sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…