Nyie Wasukuma akina Masanja mna wakati mgumu sana wa kumtetea mwenzenu, kila siku anakuja na jipya! Kazi yenu itakuwa ni kutetea kila uharo kuwa unanukia vizur
kikwete alihudhuria misiba mpaka wakawa wanamsema humu ni rais wa misiba,tena kuna mmoja alisema hayo mambo ya kuhudhuria misiba ni mambo ya waswahili teh teh teh,
jk ana hekima
Mimi mijadala inayomuhusu nimeamua kuufyata maana naamini kuna watu wakubwa tu hawasikilizi, itakuwa maneno ya huku Jf!? Nasubiria tu nione msema kweli pekee ambaye ni muda nione atakuja na jibu ganiNdio baadhi yetu tulikuwa tunasema kukaa kwake kimya ilikuwa ni heri. Akifungua kinywa tu, basi kuna watu ikiwa ni pamoja na wahanga wa janga hili watakwazika. Kazi ya serikali ni nini? Kwa nini basi serikali inakusanya kodi? Ndio, watu wachangie na waliishaanza kuchangia lakini ilikuwa ni WAJIBU wa anayekusanya kodi kuwa wa kwanza ama kutangulia kutoa huduma ya kwanza na kutoa uelekeo wa kitaifa katika kipindi cha masaa 24. Itamchukua muda mtukufu kujua majukumu ya serikali.
Tufanye nyumba haiwezekani, mahema ya kuwastil kwa muda nayo!? Chakula je!? Kuhakikisha hawapatwi na magonjwa ya mlipuko je!? Mtu kafiwa, kabomokewa na nyumba, kapoteza vitu kwa asilimia kubwa, watoto, wazee, wajawazito wanalala nje kwa wiki nzima sasa halafu Baba Mkubwa atakuja na kauli "tetemeko halijaletwa na serikali wala ccm, hivyo wafanye kazi kwa bidii"Tatizo waswahili tumezoea ahadi hewa za wanasiasa. Ndo maana tunadanganywa kila siku na tunakubali. Magufuli kaamua kuwa mkweli of what is on his mind. Go figure.
Hivi kweli kwa akili yako tukufu...serikali inaweza kuwajengea nyumba wahanga wote wa hili tetemeko? Get real bro!
Kuna Kipindi nilisema kuwa huu msemo wa HAPA KAZI TU kuna siku utakuwa kinyaa, naona yametimia haiwezekani mtu kupoteza ndugu na hana pa kulala unamwambia akafanye kazi
Magufuli is very RIGHT. Maisha yanaendelea. Tusitegemee serikali kutumia rasilimali zake kuwajengea nyumba wahanga. In fact to me, Magufuli angetumia hiyo hela ya michango kukarabati mashule, hospitali na barabara zilizo athirika. Na ndo inapashwa kuwa hivo.
Hili janga ni funzo kwetu sote. Jamani katieni bima nyumba zenu na other valuable properties (by the way bima ya nyumba iko chini mno). Tatizo waswahili kila kitu tunakifanyia mzaha tukitumia visingizio lukuki. Lakini kwa mwenye akili dunia ya leo huwezi kujenga nyumba yako kwa hizi hela za kuokoteleza...ukashindwa kuikatia bima.
Najua wengi tutapiga kelele tukisingizia umasikini (this is a popular excuse so far in our country).......lakini ukweli unabaki. Dunia ya leo...haina msaada tena! Ni jukumu lako kufanya uwezalo kujikinga na haya majanga yasiyotabilika (umeme, mafuriko, tetemeko nk). Ndo maana utakuta wazungu hata akizeeka hawi mzigo kwa ndugu au serikali. Au hata akifa...ana bima yake ya kumhifadhi kwenye nyumba yake ya milele. They always work hard and save for the rainy day!
Leo hii baadhi ya waTanzania wenzetu walioko mambelezz (au hata hapa nyumbani) wanatangulia mbele ya haki...tunaanza kupitisha bakuli! (kusafirisha mwili). This is bad and we should correct this culture. Kateni bima za maisha kwa uhai wenu, nyumba zenu na mali nyinginezo. Tuache hii tabia ya kuishi kwa kutaka kuonewa huruma na binadamu wenzetu. Undugu au urafiki haina maana kwamba tuwe mizigo kwa wenzetu.
Maisha yako. Jukumu lako.
Masanja
Miaka mitano tutaona Kama decade kwa mipasho utafikiri mswahili dah aseee.
Kufanya kazi siku hizi imekuwa fasheni.ni kazi gani ambazo wana kagera walikuwa hawazifanyi mnataka wazifanye ? Kauli zenye ukakasi namna hii kwa watu waliopata majanga hazivumiliki hata kidogo.watu wale wanahitaji kauli za faraja hakuna anayependa kulala nje wakati ana uwezo wa kuezeka kwa nyasi banda lake akajihifadhi na familia yake kwani hizo nyumba zilizopata madhara hapo mwanzo serikali ndiyo iliwajengea hao watu. Wana kagera na watanzania kwa ujumla tuna jambo la kujifunza hapa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Uyo mhaya bwana ila kakulia usukumani na wahaya ndio wananyodo sio wasukuma
Ila ni maneno yenye ukweli mtupu...Maneno ya kifedhuli sana
Kwa maneno haya kwa waliopatwa na zahma hii ni sawa na ikitokea tukivamiwa na kupigwa mabomu aje kiongozi atuambie wananchi mtajiju kwani serikali na chama hakihusiki..hii sio sawa.Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.
Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.
Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.
Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.
Hivi wewe aliyekwambia anataka kujengewa nyumba ni nani? Tangu nchi hii iumbwe ni serikali ipi iliwahi kuwajengea wananchi nyumba waliopatwa na majanga kama haya? Watu wanacho complain ni kauli zisizo na faraja zilizotolewa na mkuu wa nchi.hata kama wakiamuwa wasitoe chochote huwezi kuwambia wananchi msitegemee serikali fanyeni kazi kana kwamba wao hawafanyagi kazi au wamekaa tu kusubiri serikali. Haina shida ndugu zao wapo na watakaoguswa watawasaidia nakuwafariji. Sikutegemea kama rais angeweza kuongea kauli zile achilia mbali kwenda kuwatembelea wahanga wa tetemeko. Wana kagera hawana hiyana wataendelea kumuombea huku wakitambuwa sura siyo roho.Tatizo waswahili tumezoea ahadi hewa za wanasiasa. Ndo maana tunadanganywa kila siku na tunakubali. Magufuli kaamua kuwa mkweli of what is on his mind. Go figure.
Hivi kweli kwa akili yako tukufu...serikali inaweza kuwajengea nyumba wahanga wote wa hili tetemeko? Get real bro!