Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Mungu si athumani, naomba Mungu siku moja litokeo nyumbani kwake, alafu aje achukue wiki nzima yupo kimya, alafu akizungumza azungumzee maneno kama haya aliyoyasema!

NINA HASIRA ACHA NIISHIE HAPA

Duh..hivi mnajua hizi partisan politics Tanzania zimeshatuondolea roho ya upendo kabisa? Kila nikifikiria watu (CCM) walivyokuwa wanawakebehi supporters wa upinzani....inakuwa ngumu kuamini kwamba CCM haijali wapiga kura wake.....

Wacha tuisome number!
 
Miaka mitano tutaona Kama decade kwa mipasho utafikiri mswahili dah aseee.
hali hiyo kazaliwa chato huko angebahatika kuzaliwa pwani huyu jamaa angekua mkaali zaidi ya mzee yusuf wa jahazi....
 
Kauli ya mkulu inapokuwa janga kuliko janga lenyewe(tetemeko) la ardhi.......tumepatikana bongo land
 
Rais wa ajabu sana huyu!Watu kama hawa walio poteza hadi ndugu zao wanahitaji faraja toka kwa Head of State sio kuwasimanga! huyu
1474188071615.jpg
1474188078636.jpg
 
Usishangae Twaweza kufanyia research kauli hii ya mkuu wa kaya na majibu yakaonesha watanzania wamekubaliana nayo kwa 96%.
 
Kuna wakati rais.anakosea sana.kuna matukio ambayo unapaswa kuangalia unasema nini.asiwe kama Donald trump
 
Kwanza, kukosekana kwa rais na watoa huduma wa kwanza (first responders) tokea awali si jambo linaloeleweka kwa serikali makini. Pili, rais anaibuka baada ya wiki nzima "kupokea taarifa" ya maafa na misaada kama vile mgeni hakuwepo nchini! Halafu, kauli za kwanza anazotoa ni kuwapasha "wabaya" wake kwa kumtangulia "kuuza sura" kwenye maafa!

Hajui kwamba umma wake wa kwanza ni waathirika wa tetemeko waliofiwa, kubomokewa makazi na kuharibikiwa mali zao. Hawa wanahitaji neno la faraja. Wala hawahitaji kudanganywa kuhusu uwezo wa serikali. Si wajinga kiasi cha kuamini tetemeko limeletwa na CCM/serikali. Wamezoea kujitegemea. Wala hawapendi maisha ya dhiki kiasi cha kubweteka pale wanapoweza. Wanahitaji ujumbe wa faraja na sahihi kuhusu msaada wa dharura serikali itakaowafikishia, basi!

Hiyo mipasho ya kisiasa kwa washindani wake si kipaumbele wakati huu. There is nothing presidential in the behavior and "speak" of the honorable gentleman.
 
kuna wakati najiuliza HV huyu ni rais.au mjumbe wa nyumba kumi
 
HAYA ALIJIFICHA ZAMBIA HAKWENDA BUKOBA HAKWENDA KWENYE HARAMBEE HAKUINGIA NIKAJUA ANAPAKA LIPSTICK MDOMO ASISEME OVYO KUMBE AMEPAKA LIPSTICK YA MAPARACHICHI
Magu yupo poa..ukweli ndio huwa hatupendi tumekalia kona kona tuuu...
 
Kwanza, kukosekana kwa rais na watoa huduma wa kwanza (first responders) tokea awali si jambo linaloeleweka kwa serikali makini. Pili, rais anaibuka baada ya wiki nzima "kupokea taarifa" ya maafa na misaada kama vile mgeni hakuwepo nchini! Halafu, kauli za kwanza anazotoa ni kuwapasha "wabaya" wake kwa kumtangulia "kuuza sura" kwenye maafa!

Hajui kwamba umma wake wa kwanza ni waathirika wa tetemeko waliofiwa, kubomokewa makazi na kuharibikiwa mali zao. Hawa wanahitaji neno la faraja. Wala hawahitaji kudanganywa kuhusu uwezo wa serikali. Si wajinga kiasi cha kuamini tetemeko limeletwa na CCM/serikali. Wamezoea kujitegemea. Wala hawapendi maisha ya dhiki kiasi cha kubweteka pale wanapoweza. Wanahitaji ujumbe wa faraja na sahihi kuhusu msaada wa dharura serikali itakaowafikishia, basi!

Hiyo mipasho ya kisiasa kwa washindani wake si kipaumbele wakati huu. There is nothing presidential in the behavior and "speak" of the honorable gentleman.
amenisikitisha mhandika hotuba wake anatakiwa kuacha kazi au kufukuzwa
 
Aliyemwachia kijiti alituingiza chama sana... Jamaa yetu haamini hata pesa za misaada sio za serikali ni misaada tu ya watu mioyoni mwao... Sio pesa za kununulia ndege chakavu ukatangazwa mpya... Sasa mikwala ya nini kwa wahanga... Ajui wanaishi vipi.. Wala hajaenda...inasikitisha sana... Tulisema aliyetangulia alicheka hadi msibani sasa huyu Wa sasa anawakaripia wafiwa na wahanga ni Kali ya mwaka
 
kuna mziki ulipigwa na black eyed pies, unaitwa where is the love, ukiusikiliza huo mziki utajua watawala wanavyoharibu na kuchafua amani ya nchi
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Kama kuna mtu Mbeya aliamini serikali ndio imeleta tukio la Kupatwa kwa jua mbeya basi sitashangaa kama wakiamini na serikali ndio imeleta tetemeko
 
mh; Rais watafanyaje kazi ikiwa mali zao zimeteketezwa na tetemeko. serikali haijaleta tetemeko lkn inakitengo cha majanga,na hili ni janga mh. wanahitaji faraja zaid,kuliko maneno makavukavu. thats is too cold of u mh.
 
Back
Top Bottom