Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Hiyo kauli ya Magufuli ni jaribio la hatari la kuikwepesha serikali yake na jukumu lake la msingi na ni kinyume kabisa na matakwa ya katiba. Kwa mujibu wa katiba ya JMT sehemu ya kwanza, jukumu la msingi la serikali ni ustawi wa wananchi. Katika mazingira ambayo wananchi hawana angalau moja kati ya mahitaji yao ya msingi kutokana na janga la asili, uhalali wa serikali uko wapi kama haitatoa msaada wa haraka?
 
Uko sahihi kabisa. Huu si wakati wa mkuu wa kaya kunyoosha mdomo.
Kwanza kabisa wanaKagera ni wachapakazi, wala si watu wa kubweteka (achilia mbali kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ya mkuu wa kaya). Mkuu wa kaya analijua hilo, analijua sana.
- Huu ulikuwa ni mkoa uliokuwa umejaliwa neema ya maliasili na pia malijamii lakini Muumba mwenyewe ndiye anajua kwa nini ameusukumia majanga, janga juu ya janga. Mkuu wa kaya analijua hili.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa mzalishaji mkuu wa zao la kahawa tokea kilimo cha biashara kilipoletwa na wakoloni. Hadi leo hii kuna kiwanda cha kusindika kahawa lakini zao la kahawa soko lake la dunia limedorora.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa na chama kikubwa cha ushirika - BCU - kilichosimamia uzalishaji, ununuzi, na uuzaji wa zao la kahawa. Kabla ya Mwalimu JKN kufuta vyama vya ushirika vilivyokuwa vimefanikiwa sana, BCU iliweza kufadhili watoto wa wakulima kwenda kusoma shule za private za Uganda na Kenya na hata masomo ya utaalamu ughaibuni.
- Mkoa wa Kagera ulikuwa, na bado, unazalisha zao la chai japo kwa kiwango kidogo. Hadi leo hii kuna shamba kubwa la chai na kiwanda cha kusindika chai pale Maruku.
- Mkoa wa Kagera umekuwa mzalishaji mkuu wa zao la miwa na hivyo kuwepo kiwanda cha sukari cha Kagera. Majeshi ya Idd Amin yalikibomoa lakini kiliweza kujengwa upya na kimeendelea kuzalisha.
Hii mifano michache ya ukulima wa mazao ya biashara (kahawa, chai, na sukari) ni ushahidi wa kutosha kuwa wana wa Kagera hawabweteki, hawajawahi kubweteka. mkuu wa kaya analijua, tena sana.

Mkuu wa kaya anajua vizuri sana kuwa mkoa wa Kagera umekumbwa na mfululizo wa majanga (ya asili na ya kijamii) pengine kuliko sehemu nyingine yo yote ya Tanzania na matokeo yake umeporomoka kutoka mikoa iliyokuwa na ukwasi na kujiunga na mikoa fukara:

1. Itikadi ya ujamaa iliua BCU - chombo kilichokuwa kikisimamia kwa ufanisi uzalishaji na uuzaji wa kahawa.
2. Kana kwamba hiyo haitoshi, soko la kahawa duniani nalo likadorora - uzalishaji wa kahawa ukafifia.
3. Vita ya Kagera ya 1978. Vidonda vyake vipo hadi leo
4. UKIMWI - miaka ya mwanzoni mwa 80 Kagera ilikuwa lango kuu ulipoingilia UKIMWI. Vidonda vyake bado vipo hadi leo.
5. Ajali ya MV Bukoba.
6. Ugonjwa wa Mnyauko umeteketeza migomba yote- zao kuu la chakula na rubisi - lililowezesha watu kujikimu na wakati huo huo kudumisha utambulisho wa utamaduni wao. Zamani hizo ilikuwa ni aibu kwa Mhaya kujulikana amekula ugali. Lakini myauko ulipopiga hodi, wamekubali hali halisi na leo hii ni walimaji wakubwa wa mahindi na ugali umegeuka kuwa chakula kikuu.

Majanga ni mapenzi ya Mungu. Mkuu wa Kaya anajua wanaKagera hawawezi kubweteka wala kubweteshwa na misaada hewa ya serikali ijapokuwa wanayo haki ya kikatiba kupewa huduma za dharura na serikali yao kwa sababu wanalipa kodi. Mkuu wa Kaya ameshauriwa vibaya, au kama amejishauri basi inabidi ajitafakari na ikibidi atafute fursa nyingine atumie lugha ya kuwafariji wahanga.
asante sana kaka kwa kuweka mambo sawa;
 
Rais kaongea ukweli, mkiongea suala la kutokwenda kwakweli rais km rais hayuko sawa, tulitakiwa kumuona akiwa kule, ni faraja tosha tu, lakini kwa speech sijaona ubaya

Unachokisema sio kweli ndugu yangu " Kidabibiago" hayo maneno haambiwi mtu anayekuomba msaada. Waombaji hawa, hawakujitakia, hawa ni wafa maji. Wanaomba wasaidiwe, hayo tunayasema kwenye kongamano la wanataaluma au la wasomi. Rais hakuwa anajadili mada, alikuwa anajadili tukio la kusikitisha, tukio lililopoteza maisha ya watu 17, lililowaacha watu zaidi ya 100 wakiwa majeruhi na wengine wapo hospitalini hadi sasa. Alikuwa anawambia yatima waliopoteza wazazi wao, alikuwa anawambia wajane na wagane waliofiwa na wapendwa wao, alikuwa anawambia wazazi waliopotelwa na watoto wao.
Hakika kauli hii haikuwa sahihi ukiongezea hata hili la kutofika kule.
 
Maana ake msisubiri serikali iwajengee nyumba ndo mana kasema tetemek halijaletwa na serikali, ni ajali km ajali ngingine tu, leo hii nyumba za sehem fulan ziungue pia mtataka serikal iwajengee? Kashasema atasaidia paliposhindikana, mnataka aseme nini?

Tusisubiri serikali itujengee nyumba kwa sababu serikali haijaleta tetemeko. Okay. Tunapodai serikali itujengee hospitali, serikali ndio imeleta magonjwa? Ni serikali gani duniani inasaidia pale tu ambapo ni wao serikali ndio wamesababisha matatizo?

Ndio maneno yenyewe ya ngebe hayo kutoka kwa Rais! Nani kailaumu C.C.M. kwamba imeleta tetemeko? Rais una inject siasa kwenye janga la Taifa, Rais is excessively and dangerously politicized.

Serikali imesema itasaidia patakaposhindikana. How? Umejuaje nani kashindwa? Ni wapi serikali imetangaza mchakato wa ku assess wapi panaposhindikana?

First of all, raia wote ni sawa ki haki mbele ya serikali, hakuna anae deserve kujengewa mwingine aachwe, wote tunalipa kodi! If anything masikini wasio kwenye ajira rasmi ndio hawalipi kodi! Kwa nini wajengewe wengine tujijengee?

Tujijengee, tusisubiri serikali, lakini misaada ya vifaa vya ujenzi inakuja. Inakuja kupewa nani ?????

Ikulu nzima na ofisi ya Waziri Mkuu zina mawaziri na wakurugenzi kibao mnakaa chini mnaandika ma speech yamepinda hayana mantiki namna hii, haya make sense mbele ya umma, these people are incredible light weights and tyrannical hawa Majaliwa na Magufuli ndio maana wanaandikiwa vitu ovyo ovyo vile wanavyotaka kuvisikia.

Magufuli anaposema watu waambiwe ukweli aende mwenyewe basi akawaambie wahanga wa tetemeko maneno ya ngebe namna hiyo.
 
Namnukuu ;"
Tetemeko halikuletwa na Serikali"

Kwa hiyo wajibu wa serikali ni nini?atuambie ni kukusanya michango basi, hizi sio kauli za kuwapa faraja wahanga wa tetemeko.
 
Tusisubiri serikali itujengee nyumba kwa sababu serikali haijaleta tetemeko. Okay. Tunapodai serikali itujengee hospitali, serikali ndio imeleta magonjwa? Ni serikali gani duniani inasaidia pale tu ambapo ni wao serikali ndio wamesababisha matatizo?

Ndio maneno yenyewe ya ngebe hayo kutoka kwa Rais! Nani kailaumu C.C.M. kwamba imeleta tetemeko? Rais una inject siasa kwenye janga la Taifa, Rais is excessively and dangerously politicized.

Serikali imesema itasaidia patakaposhindikana. How? Umejuaje nani kashindwa? Ni wapi serikali imetangaza mchakato wa ku assess wapi panaposhindikana?

First of all, raia wote ni sawa ki haki mbele ya serikali, hakuna anae deserve kujengewa mwingine aachwe, wote tunalipa kodi! If anything masikini wasio kwenye ajira rasmi ndio hawalipi kodi! Kwa nini wajengewe wengine tujijengee?

Tujijengee, tusisubiri serikali, lakini misaada ya vifaa vya ujenzi inakuja. Inakuja kupewa nani ?????

Ikulu nzima na ofisi ya Waziri Mkuu zina mawaziri na wakurugenzi kibao mnakaa chini mnaandika ma speech yamepinda hayana mantiki namna hii, haya make sense mbele ya umma, these people are incredible light weights and tyrannical hawa Majaliwa na Magufuli ndio maana wanaandikiwa vitu ovyo ovyo vile wanavyotaka kuvisikia.

Magufuli anaposema watu waambiwe ukweli aende mwenyewe basi akawaambie wahanga wa tetemeko maneno ya ngebe namna hiyo.
Mkuu maelezo yako yamenyooka sana, hoja nyingine ni kuwa aliomba japo robo ya roho ya JK na SHEIN kwa nyakati tofauti je yeye ana roho ya aina gani??siku zote mwanaume unavyoonekana ukiwa na wenzio maneno na matendo yako vina akisi mbali sana toka ngazi ya familia.Pata picha hapo mambo mengine ni magumu hata kuyaelezea.
 
Kama tungekuwa na umoja kila mfanyakazi angechangia tshs 15,000 mwezi huu, mkulima tshs 3000 na m/biashara tshs 115000. Hapa tungepata fedha zaidi ya 100 billion ambazo zinatosha kurudisha hali ya maeneo yaliyoathiriwa na majanga.
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Waswahili wanaita kusimbulia !nitakusaidia lakini utanikoma hiyo ngebe nitayofungia msaada mpaka utatamani kuukataa msaada!
 
tatizo kubwa la magufuli hua njano anaita njano,, kama kuna nyekundu hawezi kukwambia kuna kitu kinafanana na jezi ya nyumbani ya simba, atakwambia kuna nyekundu kifupi hana tabia ya kutoa matumaini hewa
 
...sasa naamini hata hizo zinaweza zisiwafikie walengwa...naona wanajenga precedent ya kuepa kupeleka pesa za wahanga....wazee wa kupindisha priority...hukawii kukuta pesa inapelekwa Dodoma...kusaidia kuhamia....lol
we amini tuu kwani who cares?
 
kama sikosei kuna mtu mmoja alimshukuru Rais kwa kutuletea kupatwa kwa jua, je?ilikanushwa?
 
Kama tungekuwa na umoja kila mfanyakazi angechangia tshs 15,000 mwezi huu, mkulima tshs 3000 na m/biashara tshs 115000. Hapa tungepata fedha zaidi ya 100 billion ambazo zinatosha kurudisha hali ya maeneo yaliyoathiriwa na majanga.

Mfuko wa TAIFA wa maafa hauna senti yaani uhuru Na Museveni wanarespond haraka kuliko serikali.
Unaahirisha ziara alafu unajifungia Ikulu wiki nzima ......sibora angeenda Zambia akamuombe waachee kupitisha copper Durban Wakati Tazara iPo..
Rais akienda mahala Ni Tofauti Na Waziri Mkuu Au Makamu ...rais Ni rais na marais wanaongea Na marais mambo ya kuongea Na mtu ambaye Hana uamuzi wa mwisho hawapendi
 
Kuwaambia wahanga wa tetemeko wafanye kazi na wasisubirie serikali hali ya kuwa wanatazama kwenye TV mapesa yao yanavyokusanywa ni kuwakosea kwa namna moja ama nyingine ,Ingawa kauli ilitawaliwa na upole ila naona kuna tatizo hapo huenda pesa hizi za wahanga hawa ZIKAELEKEZWA KATIKA JAMBO LINGINE hasa ukizingatia kauli kuwa tetemeko halikuletwa na serikali.
Inashangaza kuona mkuu huyu wa kaya anaonesha dhairi kuwa amegeuza tetemeko la Ardhi kagera kuwa source of Income katika taifa letu.
Sisi kma watanzania tunapaswa kujiuliza yale mapato yanayovuka malengo huwa yanakwenda wapi?
Iko wapi bajeti ya maafa na majanga kwa ujumla wake ili iweze kutumika katika wakati huu muafaka?
Kwanini serikali imeweza kutenga bajeti yake ya kuhamia dodoma kwa kipindi kifupi mno hali ya kuwa bajeti ya kuelekea huko haikuwepo wala kujadiliwa bungeni ?
Yapo mambo yanahitaji mwitikio wa haraka mno mfano hili la tetemeko kagera lakini serikali imetupa jukumu hilo kwa asasi za kiraia na mashirika mbalimbali ya kimataifa,hili swala halikuhitaji kujipanga zaidi ya siku tatu kwa wahanga hao.
Angalia misaada iliyotoka kwa watu wa sekta binafsi na wafanya biashara mbalimbali,hili linatosha kuonesha swala hilo halikuhitaji kujipanga kama serikali ya mkuu wa kaya inavyodai kutaka kufanya hivyo,sasa wafanyabiashara na asasi za kiraia zilizochangia zinajiuliza kama walichangia mbona watu wanasema misaada yetu haikuwafikia? Ndio maana leo ITV habari mbili za tetemeko kagera zinaonesha wanyonge wakilalamika kutofikiwa na misaada hiyo.
Tanzania sio nchi tajiri ni nchi masikini inayotaka kujikwamua.
Tanzania nchi yangu nitaipenda na kuitahamini kwa moyo wangu wote.
Magufuli rais wangu nitakusifia itakapobidi kwa furaha na shangwe.
hivi nyie wengine hizi bange hua mnavutia wapi?? we umefika kagera ujue watu wameanza kusaidiwa ama laa? wewe binafsi umewasaidia nini wabukoba?
 
Hahaha!huko ndo alikopiga pushup kwenye kampen,mkacheka,mkashangaa na wengine kukata mauno.Sasa zamu yenu
 
Habarini Wadau,

Hili nina ushahidi nalo, wengi wao nimegundua wana roho mbaya kwakweli na nina mifano mingi tu.

Yaani hao huwa wanaona kama watu wengine wasio walokole ni waovu tu. Niliwahi kushauriwa kuwa ni bora umuoe msichana aliyecharuka na kupitia starehe zote za dunia akatulia kuliko anayejiita mlokole namimi sasa naamini ule ushauri ni mzuri.

Naamini wapo wanawake wacha Mungu Kweli ila wapo neutral kama hawa waroman catholic na Walutheri na huwa hawajikuuti sana na kujiona watakatifu kama walokole.

Mabinti wa kilokole mbona mpo hivyo? Au ni stresses za makanisani kwenu?
Sio wanawake wote pande mbili... Nimeishi nao nawafahamu nadhani vichwa vyao vina mapungufu wana matatizo ya kisaikolojia poleni sana najua hapa
 
Back
Top Bottom