Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Najuta kuchanga hela nukidhani zinaenda moja kwa moja kwa wananchi, kumbe zimejumuishwa kwenye mapato ya serikali!
 
Rais amesema ukweli. Kagera ina watu wengi sana na ina wasomi wa kutosha. Ukitathmini kwa undani unaweza ukawatenga waathirika katika makundi yafuatayo:

1) Kundi la Familia ya Watu Maskini kabisa, kama wazee wanaoishi peke yao au na watoto wadogo baada ya wazazi wao kuwaterekeza au kutangulia mbele ya haki, Hawa hawana mahala pa kupata msaada wowote
2) Kundi la Familia ya Watu wasio na kipato cha kila siku, Maisha yao wanayaendesha kwa kazi za mikono, hivyo nguvu ya kufanya kazi wanayo.
3) Kundi la Familia ya Watu wenye kipato cha kati. Wanafanya kazi na kupata mshahara kila mwezi
4) Kundi la Familia zinazojiweza. Zina watoto wasomi na wanauwezo wa kusaidia kujenga makazi mapya hata bila msaada wa serikali.

Kwa kuzingatia mahitaji, Kundi la kwanza linahitaji msaasa zaidi wa kujengewa nyumba. Kundi hili bila serikali kulisaidia itakuwa haijatenda haki.

Kundi la pili, nalo linahitaji msaada lakini si kujengewa nyumba. Kundi hili wasaidiwe vifaa vya ujenzi ili waweze kurekebisha nyumba zao kwa nguvu zao wenyewe.

Kundi la tatu, linaweza kusaidia kwa kiwngo tu kama fidia. Wote wanaweza wakapewa pesa kiasi fulani ili kuwasaidia kurekebisha nyumba zao.

Kundi la nne, halihitaji msaada wowote. Wanafamilia wanao uwezo wa kujenga au kurekebisha nyumba iliyoharibika.

Hivyo serikali inabidi itulie na ifanye tathmini ya kutosha ili kutambua familia zilizoathirika na kuzitenga katika makundi wakati wa kutoa msaada. Ikikosea ikakurupuka tu na kuanza kugawa misaada kiholela, kitakachotokea ni malalamiko mengi na wananchi kuichukia serikali yao.
Acha umburura na ushabiki usio na logic nakuombea haya majanga yangekukuta wewe ndio ulete hizo porojo.
 
Wewe Mama Kwani Barua Yako Imeandikwaje,
Inahusu Nini Kumbe Mapenzi. Kumbe Na Mimi Nimo
😀😁😂😄😄😃😃
 
Back
Top Bottom