Uchaguzi 2020 Rais Magufuli "theoretically" ameutangazia Ulimwengu kuwa tutakuwa na chaguzi zilzo huru, lakini "practically" hatutakuwa na uchaguzi ulio huru!

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli "theoretically" ameutangazia Ulimwengu kuwa tutakuwa na chaguzi zilzo huru, lakini "practically" hatutakuwa na uchaguzi ulio huru!

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tumeisikiliza hotuba ambayo Rais Magufuli ameitoa ya kulivunja Bunge letu na kuwaaga rasmi wabunge wanaporejea kwenye majimbo yao kwenda gombea tena, kwa nia ya kurejea tena kwenye Bunge lijalo

Rais Magufuli ametoa uhakikisho kwa Ulimwengu kuwa tutakuwa na uchaguzi ulio huru na haki.

Hata hivyo kuna tofauti kubwa ya kuutangazia Ulimwengu kuwa tutakuwa na uchaguzi mkuu utakaokuwa wa ihuru na haki na kutekeleza kwa vitendo kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki.

Mazingira ya uchaguzi wetu bado hayatoi matumaini kuwa tutakuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki.

Zipo sababu za kusema kuwa kwa mazingira tuliyonayo, hatutakuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki.

Sababu zangu ni kama hizi zifiatazo:
1. Kilio cha muda mrefu cha vyama vya upinzani vya uundwaji wa Tume huru ya uchaguzi, inaelekea watawala wetu wameendelea kuziba masikio yao kwa pamba.

Hivi inawezekanaje tuwe na uchaguzi huru na wa haki, wakati mgombea mmojawapo wa Urais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, akiwa ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na wajumbe wake?

2. Zimelazimishwa kuwekwa kanuni na Tume ya uchaguzi ya Taifa, ambazo zina lengo la kuufanya uchaguzi mkuu usiwe huru na haki

Hivi unawezaje kuwa na chaguzi huru na haki, wakati wasimamizi wa uchaguzi hawatalazimika kuwapa mawakala wa vyama nakala za matokeo?

Kama huo siyo mkakati wa CCM kufanya wizi wa kura, tunaweza kuita hiyo mbinu ya kutotoa nakala ya matokeo kuwa ina nia gani haswa?

3. Hivi Rais kupiga mkwara kuwa hataruhusu matusi kwenye uchaguzi mkuu ujao ina maana gani?

Hivi ni nani atakayeona kuwa lugha hii iliyotolewa kwenye majukwaa ya kisiasa ni matusi au laa?

Je ni Polisi wetu ndiyo watakaoamua kuwa lugha iliyotumiwa kwenye majukwa ya kisiasa ni matusi?

Ninavyojua mimi kwenye siasa za ushindani, ni kushindana kwa hoja kwenye majukwa ya kisiasa na wala hatushindani ubabe!

Chama kimoja kinapotaka kujibu upotoshaji unaofanywa na chama kingine, ni kwa kutumia majukwaa hayo hayo ya kisiasa kujibu hoja hizo na wala siyo kulitumia Jeshi la Polisi kuwanyamazisha na kutumia ubabe kwa kuwaweka ndani viongozi wa vyama vya upinzani, kwa madai kuwa wametumia lugha ya matusi!

Niseme wazi kuwa Rais wetu Magufuli ameshindwa kukabiliana na siasa za ushindani na badala yake yeye amekuwa mtu wa kutumia vitisho kwa kuvitumia vyombo "vyake" vyote vya dola kwa kukandamiza vyama vya upinzani

Kama kweli Rais wetu ana nia ya dhati ya kuufanya uchaguzi ujao kuwa huru na haki, ni kwanini anaziba pamba masikioni, kutotaka kusikia maoni ya vyama vya upinzani, ya kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi, ambayo ni maoni yenye maslahi mapana kwa Taifa letu na yenye kuleta mustakabali mwema kwa Taifa letu?
 
Nafasi ya kuitengua katiba ilikuwa awamu ya nne huko!.. mjeba wa sasa hataki michosho subirini mwengine baada yake labda atatengua!.
Magu kwasasa vipaumbele vyake ni ujenzi wa nchi huko kwenye makapi ya kidemokrasia subirini nabii wenu!!.

Hata hivyo swala la matusi si stahiki na wala si utamaduni wetu!
Maoni yangu ni kuwa still wengi wanamatumaini na mzee baba! Hivyo upinzani mjipange vya kutosha hata hivyo mtu hauwezi kuwa perfect for 100%
 
Ni nani wa ku-judge kuwa hili ni tusi na hili si tusi?

Kama jukumu hilo wataachiwa Jeshi letu la Polisi, basi tutegemee magereza kujazwa viongozi wa vyama vya upinzani!
 
Hebu tujaribu ku-imagine kwa mfano mpambano wa mpira wa miguu wa watani wa jadi wa Yanga na Simba, itokee timu mojawapo ndiyo iteue Refaree na washika vibendera wote wawili, hivi unategemea kweli timu ambayo haikupewa fursa ya kuteua hao waamuzi, inaweza kweli kupeleka timu uwanjani na kushindana?
 
Kwa tume hii hata angesema hayo yesu mwenyewe original hakuna chochote kingefanyika.Jana yeye anawapangia washindani wake nini cha kufanya kwenye kampeni wakati naye Ni mgombea pia. Itapatikana haki hapo?
 
Uchaguzi huru unanisaidia nini mimi mwananchi wa kawaida? Uchaguzi huru ndo unaingiza watu kama Waitara bungeni. Uchaguzi huru ndo unaingiza watu kama kibajaji bungeni.

Uchaguzi huru ni uchafuzi huru. Ndo maana JPM aliamua kuteua wabunge wake na kuwapa uwaziri. Kwa sababu wale waliochaguliwa kupitia uchaguzi huru hawana msaada.
 
Hebu tujaribu ku-imagine kwa mfano mpambano wa mpira wa miguu wa watani wa jadi wa Yanga na Simba, itokee timu mojawapo ndiyo iteue Refaree na washika vibendera wote wawili, hivi unategemea kweli timu ambayo haikupewa fursa ya kuteua hao waamuzi, inaweza kweli kupeleka timu uwanjani na kushindana?

Mwenyekiti wa NEC anateuliwa na rais aliyekuwepo madarakani... Hapa Ni rahisi kumteua mtu anayemtaka ( wa CCM) ili alinde masilahi ya CCM.

Wasimamizi wa uchaguzi (wilaya) wanateuliwa na rais na rais huyohuyo ndio anagombea urais... hizi Ni chenga za macho uwanjani....

Hakuna Uhuru wa maandamano ya amani, hakuna Uhuru wa mikutano kwa wapinzani, hakuna Uhuru wa vyombo vya habari...

Na bado watu wanatekwa, wanapotea, wanapigwa risasi na wengine kununuliwa ili wahame chama na kuingia kingine...

Na bado bunge, mahakama na vyombo vya Dola vinatumikishwa na chama...

Uwanja wa siasa haupo sawa...
 
Kwa tume hii hats angesema hayo yesu mwenyewe original hakuna chochote kingefanyika.Jana yeye anawapangia washindani wake nini cha kufanya kwenye kampeni wakati naye Ni mgombea pia. Itapatikana haki hapo?

Ni nani wa ku-judge kuwa hili ni tusi na hili si tusi?

Kama jukumu hilo wataachiwa Jeshi letu la Polisi, basi tutegemee magereza kujazwa viongozi wa vyama vya upinzani!

Uchaguzi huru unanisaidia nini mimi mwananchi wa kawaida? Uchaguzi huru ndo unaingiza watu kama Waitara bungeni. Uchaguzi huru ndo unaingiza watu kama kibajaji bungeni. Uchaguzi huru ni uchafuzi huru. Ndo maana JPM aliamua kuteua wabunge wake na kuwapa uwaziri. Kwa sababu wale waliochaguliwa kupitia uchaguzi huru hawana msaada.

Cha msingi Ni kukataa uchaguzi ujao mahakamani... hata Kama sio huu wa 2020.
Ilikufanya marekebisho ya mapungufu Kama nilivyoandika hapo post namba 7...
 
Mystery, hatuhitaji mjadala na Rais Magufuli. For all five yrs kuna uverwhelming evidence kuwa hakutenda haki, hapakuwa na uhuru wa habari, hapakuwa na uchaguzi wowote ulofanyika ukawa huru na haki, hapakuwa na mahakama, hapakuwa na bunge etc, etc. Linalohitaji ni nini kifanyike kurudisha "angalau" (nasema angalau maana nako kwa JK kulikuwa na mapungufu LKN hapakuwa na UDIKITEITA) tulipokuwa kabla ya yeye kuingia madarakani! NINI KIFANYIKE? Mimi sina jibu!
 
Zuio mahakamani ndio suluhisho... Tukisubiri uchaguzi wa maigizo ndio tumeshakubari matokeo.... Maana matokeo ya uchaguzi kwa rais hayana rufaa Wala kudai haki mahakamani.
 
Cha msingi Ni kuweka zuio mahakamani kuzuia uchaguzi wa urais... na kuweka serikali ya mseto kwa muda.

Huku marekebisho yakifanyika kwa Kasi na kwa usawa bila maslahi yoyote.

Baada ya hapo ufanyike uchaguzi wa wabunge alafu baadae ufanyike uchaguzi wa rais.
Huu ni uamuzi mzuri lakini waimba mapambio ya kumsifu yesu mpya wataupinga.

Uchaguzi wa wabunge pia, mambo yakiwa yale ya kwenye primaries tunapotezeana muda tu.
 
Kwa tume hii hats angesema hayo yesu mwenyewe original hakuna chochote kingefanyika.Jana yeye anawapangia washindani wake nini cha kufanya kwenye kampeni wakati naye Ni mgombea pia. Itapatikana haki hapo?
LIMBOMAMBOMA
Yaani ni ajabu na kweli!
 
Nafasi ya kuitengua katiba ilikuwa awamu ya nne huko!.. mjeba wa sasa hataki michosho subirini mwengine baada yake labda atatengua!.
Magu kwasasa vipaumbele vyake ni ujenzi wa nchi huko kwenye makapi ya kidemokrasia subirini nabii wenu!!.

Hata hivyo swala la matusi si stahiki na wala si utamaduni wetu!
Maoni yangu ni kuwa still wengi wanamatumaini na mzee baba! Hivyo upinzani mjipange vya kutosha hata hivyo mtu hauwezi kuwa perfect for 100%
Vipaumbele vya kujenga nchi vimeshindwa kuinasua nchi kutoka kwenye listi ya LDC (Least Developed Countries).

Hatudanganyiki na propaganda, kadanganye mambumbu wenzako.
 
Uchaguzi huru unanisaidia nini mimi mwananchi wa kawaida? Uchaguzi huru ndo unaingiza watu kama Waitara bungeni. Uchaguzi huru ndo unaingiza watu kama kibajaji bungeni. Uchaguzi huru ni uchafuzi huru. Ndo maana JPM aliamua kuteua wabunge wake na kuwapa uwaziri. Kwa sababu wale waliochaguliwa kupitia uchaguzi huru hawana msaada.
Na hao aliowateua akawatumbua vile vile, Tz hakuna cha profesa wala mkulima wa kijijini Ilalila, wote sawa tu.
 
Mimi nadhani inafaa tufike mahala tuachane na huku kulialia na kulalamika kwingi tunakokufanya, huku tukijua hatuna njia za kukubadilisha 'at least' kwa namna ilivyo sasa.

Miaka yote tunaongelea 'tume huru' pembeni, lakini kiuhalisia hakuna aliyefanya juhudi ya kuliweka hili mbele, sio vyama vya upinzani, wala asasi nyinginezo ili ifahamike kwamba bila tume huru hakuna uchaguzi kufanyika.

Tumeacha kuliweka mbele hili, hadi sasa, tukijua uchaguzi unafanyika kwenye mazingira tunayoyapigia kelele pembeni tu, na wala hatufanyi bidii kuwaelimisha wananchi juu yake.

Hapa tulipofikia, tumekubali kuingia kwenye uchaguzi bila ya masharti yoyote, kwa hiyo kwa maoni yangu, badala ya kuendelea na kulalamika na kulialia kusikokuwa na tija, ni wakati wa kushughulikia njia tunazoweza kuzifanya ili mazingira haya yasiyokuwa rafiki, tujaribu kupunguza madhara yake.

Maana yangu ni kwamba, ni bora sasa hivi kuweka juhudi za kujua,kung'amua njia zitakazotumika kuhujumu uchaguzi usiwe huru.
Tuwe tayari kutoa ushahidi usiopingika, ulio wazi kuonyesha hujuma hizo na kuziweka wazi dunia nzima ijue.

Huku kulia lia na ushahidi huna, na hata kama unao ni wa mashaka hakuleti maana yoyote.

Hilo ni moja.

La pili ni hili: Kama Magufuli ataruhusu kuwepo uchaguzi utakaoonekana kuwa na aina hata ndogo ya uhuru na haki, na wananchi wakamchagua na CCM yake, atastahiri pongezi kubwa sana, kwa sababu ni vigumu sana kuamini kwamba katika mazingira hayo bado waTanzania wakapiga kura kumpa yeye na chama chake pawe na sababu ya kulalamika tena. Atastahiri pongezi nyingi, na mimi pamoja na kura yangu kutompa, nitampongeza sana.

Maana ya pekee ya tukio hili itakuwa wazi kwamba wapinzani hawakufanya kazi waliyotakiwa kuifanya tangu miaka mitano iliyopita.

Katika hali ya namna hiyo, kwa nini umlaumu Magufuli, ambaye hakuficha lolote kuhusu utawala wake ulivyo.

Mara nyingi tunawalaumu waTanzania kuwa ni wajinga, lakini sisi tunaojitambua kuwa wajanja tunashindwa kuwaondolea ujinga huo wananci wenzetu, na kubaki tunawalaumu wao, badala ya sisi kujilaumu kwa uzembe wetu wenyewe.

Pakiwepo na mazingira wakati wa uchaguzi, hata kidogo yanayofanana fanana na yale ya 2015, na Magufuli akashinda, tena pengine kwa asili mia kubwa zaidi ya aliyopata wakati ule,...Nitampongeza sana.

Hadi hii leo, Lowassa anasema aliibiwa kura, lakini ushahidi upo wapi?
Na kama wakati huo ilishindikana kupata huo ushahidi, kwa nini miaka mitano baadae, bado pasiwepo njia ya kupata ushahidi wa tume huru kuvuruga uchaguzi.
Udhaifu wetu ndio faida ya CCM, kwa hiyo tuachane na kulialia kila mara bila kutafuta njia za kukomesha hayo yanayotuliza kila mara..
 
Kalamu1
Wewe unasema watanzania tunalialia, basi pendekeza wewe nini kifanyike, ili pasiwepo uchaguzi wa maigizo?
 
Hivi lugha za matusi kweli bado mnazitetea? Waliotumia sana lugha hizo awamu hii ni Halima mdee, yule mbunge wa Arusha mjini, na Lissu - hawa wa mwanzo walipopelekwa shule (lockup), walipotoka huko lugha yao ikawa ya staha inayo takiwa na watanzania. Lakini yule kichwa maji Lissu na yaliyompata hajajua ni lugha ipi ya kutumia. Nafikiri Lissu akishinda urais ataambiwa ni lugha ipi atumie.
 
Back
Top Bottom