Rais Magufuli tuachie zawadi ya Halmashauri zetu kujiendesha

Rais Magufuli tuachie zawadi ya Halmashauri zetu kujiendesha

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Wewe ni msimamizi mzuri na ukiamua kitu kinafanyika mifano ipo hai kama Makao makuu yetu kuhamia Dodoma wengine hawakuamini na walifikiri ni usanii lakini sasa hivi Mji wetu Mkuu Kikatiba kabisa ni Dodoma.

Hivyo basi binafsi naamini kama Halmashauri zetu nchi nzima zikiweza kutumia sehemu ya mapato inazokusanya kwa maendeleo ya hizo Halmashauri tutafika mbali sana

Najua unaogopa wizi wa hizo fedha lakini kama ukiamua kutumia nguvu yako ya Kikatiba kama Rais wa Nchi nina uhakika hawataweza kuiba hizo fedha, tafadhali tuachie hii zawadi au niseme urithi kama ukifanikiwa hapo yaani kuacha Halmashauri zinazowajibika hakika utakuwa mkombozi wa hii nchi.
 
Acha Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Afanye Kazi
 
😁😁😁,yaani yeye ndiye alikwapua vyanzo vya mapato vya halmashauri na kupeleka TRA ili makusanyo yaonekane yamepanda,halafu baadaye hizo hela anazirudisha tena kwenye halmashauri😁😁!Unatoa hela mfuko wa kulia na kuweka wa kushoto!

Alitengeneza tatizo sasa mnamuomba alitatue!
 
Mkuu, wewe ni mtumishi wa halmashauri nini? Naona mirija ilikatwa.

Hint: Pima effectiveness ya utendaji wa halmashauri: kabla vs baada, ya serikali kuu kuchukua usimamizi. Utapata jibu.
 
Kwenye uchaguzi huu tumeona wizi wa kura wa kimachomacho, sasa kumsifia mtu huku yeye mwenyewe ndio anaratibu wizi, ni kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Hakuna sehemu watu walikuwa wezi kama halmashauri

Wewe maisha yameanza kuwa magumu kwako

Ahaaa Mwana ccm tulia

Unataka kuanza kupiga deal
 
Kiongozi,

Umeandika kana kwamba zimezuiliwa kutumia fedha? au hazitumii fedha kitu ambacho hakipo.

Miradi ya vyumba vya madarasa, maabara, vyoo, nyumba za walimu, mabweni, mabwalo, zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya, majengo ya ofisi za halmashauri, masoko na stendi yote haya yanatumia hela
 
Ila kama unamaanisha pesa za bure bure (kupitia miposho) nasema hapana (BIG NO)
 
Hakuna sehemu watu walikuwa wezi kama halmashauri

Wewe maisha yameanza kuwa magumu kwako

Ahaaa Mwana ccm tulia

Unataka kuanza kupiga deal
Yaani mkuu hizi halmashauri zilikuwa zimegeuka janga kwenye nchi hii, malalamiko bungeni yalikuwa mengi! semina, vikao vya posho, ziara na mambo chungu nzima ya kijinga kijinga tu, huduma ktk halmashauri hizo hafifu, Na sio siri kwa sasa wanalia njaa kweli kweli.
 
Wajinga nyie kipindi wabunge waupinzani wanakataa na kusema haya wewe na mapopoma wenzako hamkuwa mnaporomosha matusi?? Kisu kimekata upande wako?? Et akuachie zawadi?? Nchi au hizo halmashauri n Mali ya Magufuli??
 
Back
Top Bottom