Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Uchaguzi utafanyika, wapo wanaofikiri kwamba tutaahirisha. Nani anataka kukaa kwenye maofisi haya muda wote huo?

Tume huru ndiyo habari ya mjini ....ikifuatiwa na corona!!

Tume huru kwanza !!
 
Kwaiyo hadi majukumu na maamuzi yako ya ngazi familia unataka maelekezo ya rais?

Basi subiri uteelekezwa cowards
Majukumu gani hayo ya ngazi ya familia? Mbona mnakuwa wajinga hivi? Nchi walizoamua kuwa hata mikutano ya ibada isifanyike wameingilia majukumu ya familia? tetea hoja kwa hoja na si vioja! Sema bado hatujawa na threat kiasi cha kuzuia hata mikusanyiko ya ibada, sio kuleta ujuaji mwingi.
 
Wakuongoze hadi ngazi ya familia mkuu?
Hili no janga la afya la kimataifa.

Si habari ya familia tu.

Halijawahi kutokea kwa takriban miaka 100 iliyopita.

Ndiyo maana viongozi Uingereza, Italy, South Africa baadhi ya states/ regions za China, Marekani na nchi nyingi zilizoendelea waliweka/ wameweka muongozo watu wasitoke majumbani bila sababu maalum.

Viongozi mpaka Saudi Arabia huko kwao Mtume wameweka muongozo watu wasiende Misikitini.

Viongozi Vatican huko wameweka muingozo watu wasiende makanisani.

Unaelewa hayo? Unasoma habari za dunia?

Au unaleta ushabiki wa kijinga tu?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
"Na uchaguzi tutafanya, wapo wanaofikiri kwamba tutaahirisha, nani anataka kukaa kwenye maofisi haya muda wote huo,"
Tumekuelewa mzee hiyo ofisi ni ngumu usichukue fomu tena.. Ila kingine tupatie tume huru ya uchaguzi ili wananchi wafanye maamuzi wenyewe
 
huyu jamaa japo nilimpa kura 2015...but now naomba isarel mtoa roho afanye yake
No wengi tunamwombea awe hai ili akamilishe miradi aloianzisha, hata kama hataimalizia by 2025 angalau iwe katika hatua za kukamilika morning ili atakayeingia baada yake awe na ari ya kuimalizia
 
kigogo alianza kulizungumzia hili jambo kule twitter wiki moja kabla ya hii kauli ya jiwe.
alisema jamaa kwa kutumia power aliyonayo, amepanga kuhairisha uchaguzi mkuu kwa kigezo cha corona.

alichofanya kigogo ni preempt tactics baada ya kuusoma udhaifu wa jiwe maana huwa hapendi raia tujuwe mapema mipango yake ovu ya baadae. sishangai leo katoa kauli ya kukanusha.

hii ni sawa na story za wawindaji wawapo poroni. wanakwambia mnyama chui anapotaka kukudhuru huwa anajificha kwenye kichaka usiomuone ili akufanyie shambulizi la ghafla.

kitendo cha kumuona tu kinamuondelea confidence na kumfanya awe na aibu. mwisho anaghairi na kuondoka zake.
 
Kiranga,
Kwaiyo kama Saudi Arabia wasema na hapa Tanzania waseme kwa vile Saudi Arabia wamesema?

Halafu nachokushangaa umetaja USA, ITALY then umesema nchi ZILIZOENDELEA, kwaiyo tuseme kama zilivyosema nchi ZILIZOENDELEA? Ushasema nchi zilizoendelea eti unafananisha na sisi nchi za mtaji wa masikini ni nguvu zako mwenyewe au unaowataka tuwafuate USA au ITALY ambani wanaweza wasi IMPORT bidhaa yoyote kutoka nje hadi hilo JANGA liishe.

Halafu ukisema ushabiki una maanisha ushabiki wa aina gani?

Ama kweli huu ugonjwa umekuja kwenye nchi kila mtu ni mtaalamu.

Kumbuka kila nchi au serikali yoyote ina style ya ku handle matatizo yake na ninavyowajua WATANZANIA hamna jema ata serikali ingesema hilo unalolitaka kufanyika ungekuja na blah blah tena.Na upuuzi kuhisi ushauri wako ni wa maana kuliko wa wengine.
 
misasa, Nimeonesha kwamba, hili si jambo la familia, ni jambo linaloeleweka kimataifa na nchi nyingi zinafanya hivyo.

Umeelewa hilo kwanza?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Nimeonesha kwamba, hili si jambo la familia, ni jambo linaloeleweka kimataifa na nchi nyingi zinafanya hivyo.

Umeelewa hilo kwanza?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Nimeelewa ndio maana tusilaumu na tuamini serikali maana inachukua maamuzi hatua kwa hatua.

Kwa nchi masikini kama yetu tukifanya maamuzi ya kukurupuka uchumi unaweza kudorora kisa mataifa makubwa ki uchumi yamefanya tutaumbuka uko mbele ya safari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…