Rais Magufuli ulimtumbua upesi aliyechana Quran, mbona unachelewa Kumtumbua Jerry Muro aliyewadharau Waislamu?

Rais Magufuli ulimtumbua upesi aliyechana Quran, mbona unachelewa Kumtumbua Jerry Muro aliyewadharau Waislamu?

Rais Dkt. Magufuli ulimtumbua upesi yule Mtumishi wa Halmashauri ya Kilosa Ndugu Daniel Maleki ambaye alikuwa ni Afisa Kitengo cha Biashara kwa Kosa la Kuchana Kitabu Kitakatifu cha Quran kinachotumiwa na Waislamu, ila tunashangaa ni kwanini hadi hivi sasa hujamtumbua Mkuu wa Wilaya Jerry Muro kwa Kosa la Kuwadhihaki Walimu wa Madrassa kupitia Msemaji wa Simba SC Haji Manara.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Kauli ya DC Jerry Muro ya Kumdhihaki Msemaji wa Simba SC Haji Sunday Manara kupitia Kituo cha Redio cha Wasafi FM na Mtandao wa WhatsApp wa Klabu ya Yanga kuwa Elimu aliyonayo Haji Manara ni ya Kufundisha tu Watoto Madrassa Kimantiki (Logically) haina tofauti na Kuwatukana Waislamu hasa ukizingatia kuwa hata hao Walimu wa hizo Madrassa wanatumia hicho hicho Kitabu Tukufu cha Quran.

Na najua Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli una mambo mengi ya kikazi (Kiutendaji) hivyo unaweza mambo mengine ukawa hujaambiwa na Mimi Mpiga Kura wako Mzukulu nakuambia muda kuwa tayari Msemaji wa Simba SC Haji Manara nae ameamua kwenda mbele ambapo sasa anaenda Kumshtakia DC wako Jerry Muro kwa Waislamu na kama haitoshi tayari kuna Waislamu kadhaa nao wameshaibuka (hasa Walimu wa Madrassa) wanajipanga ili waone Hatua Kali za Kumchukulia DC wako huyu Mpuuzi Jerry Muro kwani wanasema kuwa Dhihaka aliyotoa DC Jerry Muro hakumlenga tu Haji Manara bali amewalenga pia na Waislamu wote nchini.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Waislamu hawa (amba huwa hawana Masihara ukiyagusa Maslahi yao ya Kiimani) wameenda mbele zaidi na Kuhoji ya kwamba kama ni mambo ya Kimchezo ya Utani wa Jadi wa Simba na Yanga kulikuwa na haja gani kwa DC Jerry Muro kuingizia Masuala ya Kiimani (Dini) hadi Kuwadhihaki Walimu wa Madrassa kupitia Msemaji wa Simba SC Haji Manara ambaye anajulikana kuwa ni Mwalimu mzuri mno wa Madrassa?

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Mtumishi wako huyu DC Jerry Muro hakuanza leo Kumdhihaki Msemaji wa Simba SC Haji Manara na kuna Kipindi huko nyuma aliwahi Kumdhihaki hadi kupitia Ulemavu wake wa Ngozi (Ualbino) kwa Kumuita Dili na hakuchukuliwa hatua ila nina Ushahidi wa Watanzania kama Wawili hivi ambao walikamatwa kwa Kosa la Kuwaita Dili hawa Walemavu wa Ngozi (Maalbino)

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli wapiga Kura wako tunajiuliza Maswali hivi ni kwanini kila ambapo DC wako huyu Jerry Muro akiwa anazungumzia masuala ya Mpira hasa ya Utani huu wa Jadi wa Simba na Yanga akianza Kumtaja Msemaji wa Simba SC Haji Manara ni lazima tu atatoka kwenye lengo na ataanza Kuzungumzia Maisha yake binafsi, kumtukana, kumdharau na kumdhalilisha? Hivi na siku Msemaji wa Simba SC Haji Manara nae akisema afyatuke (afunguke) kwa mambo binafsi ya DC wako Jerry Muro (ambayo mengine ni mabaya kabisa na yanatia Aibu) patakalika Mheshimiwa? au DC wako Jerry Muro anadhani Yeye ni Msafi hivyo, Muadilifu, Malaika na hana Mauzauza yake tena ambayo yanazidi hata anayomdhihaki nayo Msemaji wa Simba SC Haji Manara?

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kama ulimtumbua Mchana Quran Ndugu Daniel Maleki basi nakuomba pia usijiulize katika kumtumbua Mtukana Walimu wa Madrassa Ndugu Jerry Muro kwani wote (Wawili hawa) ni Watumishi wako katika hii Serikali yako ya awamu ya Tano ambayo tunaamini kuwa inatenda Haki (japo najua haki ya kweli huwa ipo Mbinguni tu Kwake Mwenyezi Mungu) Baba Muumba.

Na nasikitika na hata Kushangaa kuona Mamlaka zako husika TCRA imenyamaza juu ya DC wako huyu ( Jerry Muro ) Kumdhihaki Muislamu na Msemaji wa Simba SC Haji Manara kupitia Kituo cha Redio cha Wasafi FM na pia kwa Jeshi lako la Polisi hasa la Mkoa wa Dar es Salaam kukaa kimya badala ya Kumkamata DC Jerry Muro kwani Kauli yake hiyo inaweza Kuhatarisha Amani na kukatokea Mzozo wa Kiimani nchini unaowahusu Wakristo (akina Jerry Muro) na Waislamu (akina Haji Manara)

Nakuamini Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli na najua hili hutoliacha lipite hivi hivi. Uwe na Kwaresma njema Mheshimiwa.
Wapi alipo kashifu Waislamu/Uislamu?

Kwa nini unapenda kuishi kwenye Dunia ya kutafuta lawama zisizo kuwepo? Kila siku kutafuta mchawi asiyekuwepo?
Uchawi huo unao mwenyewe katika fikra zako.

Huyo Haji kila siku anakashfu watu. Yeye ana haki hiyo? Watu wamwona kama mlemavu na kumwacha kama alivyo.
 
mimi ni muislamu lakini nasema jerry muro yuko sahihi, manara ana kashfa sana kwa yanga tumemchoka, kuambiwa akafundishe madrasa sio kosa, hakuna mahali ametukanwa
 
Kwani muumin wa kiislam kuambiwa akafundishe madarasa ni kosa??,

Inategemea anaambiwa katika tone gani Mdau. Ukirejea Tone ya DC Jerry Muro juu ya Msemaji wa Simba SC Haji Manara ilikuwa ni ya Kidhihaka na Dharau nyingi. Habari nilizozipata kutoka kwa baadhi ya Waislamu wanajiandaa Kumshtakia DC Jerry Muro kwa Mamlaka husika na kama asipochukuliwa Hatua haraka basi Wao Waislamu kama Waislamu watamshtakia Mwenyezi Mungu kupitia ile Dua yao moja Hatari sana ambayo wakiombea Ufe unakufa Kweli au wakiomba uwe Shoga unakuwa kweli au wakiomba uwe Mwendawazimu basi hapo hapo inakuwa hivyo. Nikiwa kama Mkristo nawaomba Waislamu Tanzania nzima wasilinyamazie hili la DC Jerry Muro na wamuadabishe upesi mno.
 
Wapi alipo kashifu Waislamu/Uislamu?

Kwa nini unapenda kuishi kwenye Dunia ya kutafuta lawama zisizo kuwepo? Kila siku kutafuta mchawi asiyekuwepo?
Uchawi huo unao mwenyewe katika fikra zako.

Huyo Haji kila siku anakashfu watu. Yeye ana haki hiyo? Watu wamwona kama mlemavu na kumwacha kama alivyo.

Wakristo tumezidi sana Kuwadhalilisha na Kuwadharau Waislamu na Mimi kama Mkristo ninayejitambua najitoa muhanga Kuwatetea. Na Wakristo wenzangu mkizidi Kunipinga katika hili au msipokubaliana nami basi na Mimi muda wowote kuanzia sasa nitaukana ( nitaachana ) na huu Ukristo wangu wa Ulutheri ( Lutheran ) Kidhehebu na kuhamia rasmi kwa Waungwana na Watu wema na wavumilivu Waislamu.
 
Inategemea anaambiwa katika tone gani Mdau. Ukirejea Tone ya DC Jerry Muro juu ya Msemaji wa Simba SC Haji Manara ilikuwa ni ya Kidhihaka na Dharau nyingi. Habari nilizozipata kutoka kwa baadhi ya Waislamu wanajiandaa Kumshtakia DC Jerry Muro kwa Mamlaka husika na kama asipochukuliwa Hatua haraka basi Wao Waislamu kama Waislamu watamshtakia Mwenyezi Mungu kupitia ile Dua yao moja Hatari sana ambayo wakiombea Ufe unakufa Kweli au wakiomba uwe Shoga unakuwa kweli au wakiomba uwe Mwendawazimu basi hapo hapo inakuwa hivyo. Nikiwa kama Mkristo nawaomba Waislamu Tanzania nzima wasilinyamazie hili la DC Jerry Muro na wamuadabishe upesi mno.
mi ni muislamu namsapoti jerry muro, manara hana uislamu wowote ni mlevi, anatangaza biashara ya kamari, huyo ni mjinga tu, hakuna muislamu atakaemsapoti huyo mdhalilishaji wa yanga, mwambie yanga waislamu tuko nyuma ya jerry muro tutamsapoti kwa kila hali.
 
Nanyie punguze kulalamika! Mbona hakuna ubaya wowote katika maongozi yake ?

-
 
Nawaaminia Waislamu na najua kama Mheshimiwa Rais atashindwa Kumwajibisha DC wake Jerry Muro basi Wao watamuwajibisha kwa namna yao ya Kipekee kabisa na nitashangaa kuona Waislamu wote nchini Tanzania wanalinyamazia hili. Nawakubali sana Waislamu hivyo msiniangushe katika hili na lazima DC Jerry Muro ama awaombeni Radhi haraka au asubiri yale Maombi yenu Maalum na ya Kipekee ya Wakaidi Kwake Allah ( Mwenyezi Mungu ) Msikubali kabisa Waislamu tafadhali.
Sasa wee Mzukulu ndiyo mchochezi no moja nashauri Jeshi la Police likufungulie Jalada la uchunguzi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzukulu,

Mtoa mada naona amechanganyikiwa kiasi cha kutaka kutupotosha na kutuchonganisha. Tumpuuze huyu. Hakuna mahali dini imedharauliwa ila ni ufinyu wa mawazo na upofu wa kuchanganua maudhui ya hoja husika.
 
Wakristo tumezidi sana Kuwadhalilisha na Kuwadharau Waislamu na Mimi kama Mkristo ninayejitambua najitoa muhanga Kuwatetea. Na Wakristo wenzangu mkizidi Kunipinga katika hili au msipokubaliana nami basi na Mimi muda wowote kuanzia sasa nitaukana ( nitaachana ) na huu Ukristo wangu wa Ulutheri ( Lutheran ) Kidhehebu na kuhamia rasmi kwa Waungwana na Watu wema na wavumilivu Waislamu.
Wwe Jela ina kwita jiangalie sana na unacho comment kwa mitandao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pumbavu kabisa, tangu mwaka uanze sijaona uzi wa kikuku kama huu, kwanza unajaza server za JF tuu kwa huu ushuzi
 
Mtoa mada naona amechanganyikiwa kiasi cha kutaka kutupotosha na kutuchonganisha. Tumpuuze huyu. Hakuna mahali dini imedharauliwa ila ni ufinyu wa mawazo na upofu wa kuchanganua maudhui ya hoja husika.
Tz watu wengi sana reason capacity zao ziko chini sana kama huyo mleta maada,na hiyo ni changa moto kubwa sana kwa Serekali!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah mnakuza mambo Sana waswahili ... Kuambiwa kafundishe madrasa ni tusi , kwahiyo angeambiwa kafundishe UDSM ndio mngefurahi??

Huyo Manara ana Inferiority Complexity anapenda kudharau wengine yeye akitikiswa kidogo anapanick... Atulie tucheze soka Kama anataka mipasho aingie kwenye ulingo wa siasa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manara.JPG

Hii picha nimeikuta fb, iwapo huyu ni Mwenyewe, sioni kosa, kwani mimi binafsi nilikua sijui kama Manara anaijua dini yake vizuri kufikia hatua ya kuwa mwalimu.

Nampongera Jerry kwani ndio aliyenipa ufahamu huo, kwamba, licha ya manara kuwa msemaji mzuri, pia ni mwanadini kindakindaki.

Sasa hiyo dhahaka imetoka wapi?
 
Back
Top Bottom