Uchaguzi 2020 Rais Magufuli umetutia sana Moyo vijana wako kwenye suala la ajira

Sio Rahisi kwa Kiongozi mkubwa ku-admit mateso ya vijana..

Na kakiri kwamba ATALISHUGHULIKIA suala la ajira kwa NGUVU zote.

Msema kweli ndie mpenzi wa MUNGU .

Vijana twendeni pamoja na Rais Magufuli.View attachment 1598263
Kwani kwa wafanyakazi alisemaje kipindi cha kampeni zilizopita 5years back, na vijana wanaotajwa hapo wewe kwa akili yako unadhani hawajui kipindi chote hiko hata leo aje kusema hayo? Unasema msema kweli mpenzi wa Mungu ni sahihi kabisa, tuambie pia na mtu anaye hadaa watu ni nani?
Mnakuwa wepesi kudanganywa kama mmerogwa. Ndo mana mnaambiwa someni muelimike ili msishikiwe akili hizo
 
Wanabodi,

Huwa siandiki uzi kama sijapata hisia/kuwiwa kuandika ,siandiki kiushabiki ila napenda kushusha nyuzi nikiwa kama kijana mzalendo wa Taifa la Tanzania na mpenda maendeleo.

Huwa napenda ku- declare' kuwa mimi ni mwanachama hai wa Chama cha Mapinduzi lakini sio msifia chochote ili bora liende lakini napenda ku-analyse vitu na kuangalia vina maslai gani kwa taifa.

Kama kijana mzalendo napenda kuungana na watanzania wengine kutambua kazi nzuri iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kipindi hiki tulichowapa dhamana ya uongozi kwenye taifa hili.

Huwa sipendi kuyaelezea waliyoyafanya maana kuna nyuzi nyingi humu zinaelezea maendeleo na mikakati pamoja na miradi mikubwa yenye tija kwa taifa iliyokamilika na ambayo bado iko mbioni kukamilika,hakika hili ni jambo jema sana na Hongera CCM ,Heko Rais Magufuli.

Nautambua uwezo wako shupavu wa kulivusha taifa letu la Tanzania kwenye hiki kipindi cha miaka mitano,kwenye majanga mbalimbali yaliyotokea yakiwemo ajali za majini,hali ya nchi pamoja na hili janga la corona,haikua rahisi kama Taifa kuvuka kwenye vipindi hivi vya mapito.

Mhe Rais ,kama kijana ambae nafahamu hali za vijana wenzangu hasa hasa wale wahitimu kwa kipindi cha miaka mitano toka mwaka 2015-2020 kulikua na changamoto kubwa sana ya ajira .

Na nilipanga niandike uzi wa kuelezea jinsi vijana wanavyohangaika huku na kule kwenye suala hili mtambuka.

Sitaki kujikita sana ndani ndani kwenye vitabu vya muasisi wa Taifa hili la Tanzania akiongolea kuhusu ajira na elimu lakini wote tunajua Mwalimu Nyerere alithamini na kusisitiza sana watu wafanye kazi (ajira).

Mhe Rais,Tuongee ukweli na bahati nzuri wewe ni mpenzi wa MUNGU na ni msema kweli,Serikali imekua muajiri nambari moja kwenye Taifa hili.

Serikali imekua ikitoa ajira almost 80% kwa vijana na watu wote,na imekua ikifanya hivi kwenye idara zake nyingi zikiwemo ajira za majeshi (polisi,jwtz,magereza,zimamoto ,idara ya uhamiaji etc).

Pia Serikali kwa miaka yote imekua ikitoa ajira nyingi kwa madaktari,wahandisi ,waalimu wa msingi na sekondari n.k

Nisingependa kutaja idara zote ambazo Serikali huwa inaajiri lakini Mhe Rais kwa kipindi toka mwaka 2015 mpaka sasa Serikali haijawahi kutoa zile ajira za wengi,kwa maana nyingine tumekua na idadi ya wahitimu wengi wa vyuo vikuu na vyuo vingine toka mwaka 2015 mpaka sasa .

Hii ni kusema tuna graduates wa intake kama 5 au 6 toka mwaka 2015 ambao wengi wao wako mtaani na wameshindwa kujiajiri na wala hawajaajiriwa na sekta binafsi.

Nimesikiliza kwa makini Mkutano wako wa kampeni leo pale segerea,na ukaongelea kipaumbele chako cha kwanza ambacho ulikifanya cha "Kudumisha Amani na Usalama", ukaongelea hali ilivyokua wakati unaingia madarakani ,kwamba hakukua Hali nzuri ya Usalama na ukatoa mifano ya kuuwawa kwa askari kibiti na lile tukio la Ubungo la majambazi kuiba NMB Mhe Rais nikupongeze hapo ulifanikiwa na umefanikiwa sana, HATUNA ujambazi wala wizi wa kutumia silaha tena,hali ni shwari na tunajisikia kweli tuko kwenye nchi yetu.(KONGOLE SANA).

Mhe Rais,kwenye suala la ajira kiukweli kabisa ndani ya kipindi hiki toka 2015 mpaka sasa serikali ni HAIJAFANYA vizuri kwenye hii sehemu.

Kuna sababu nyingi,labda serikali ilikua ina vipaumbele vingine vya haraka sana vya kufanya ndani ya miaka hii mitano,mfano huwezi kuanza na kipaumbele cha Ajira kwa vijana wakati kuna kipaumbele cha haraka cha Amani na usalama wa Raia.

So kwa mantiki hiyo naelewa kwa nini Serikali yetu haikutoa kipaumbele cha AJIRA kwa vijana kwenye miaka hii mitano ya uongozi wako.

Mhe Rais Magufuli, nimesikiliza maneno yako haya ya leo kwa umakini sana na nikayatafakari jioni ya leo ,naomba niyarudie hapa kwa kunukuu ...

" Vijana wanakosa Ajira,Vijana wanadharaulika,Wengine wamemaliza kusoma hawapati Ajira"
"Miaka mitano inayokuja nataka suala la ajira NILISHUGHULIKIE kwa nguvu zote,kama tunaweza kupandisha uchumi,kujenga Flyover,siwezi kushindwa suala la ajira kwa vijana".

Mhe Rais Magufuli, maneno haya na ahadi hii ulikua unaisema ukiwa unamaanisha na naamini imetoka ndani ya sakafu ya moyo wako, na inaonesha wazi unajua kila jambo linaloendelea kwa vijana wako wahitimu wa Tanzania.

Vijana waliosoma kwa kodi za watu maskini,vijana ambao wana matumaini ya kuingia kwenye soko la ajira,vijana ambao umesema wanadharaulika,Tafadhali usiwaache hawa vijana Mhe Rais.

Tumeashuhudia nafasi nyingi za kazi zilizokua zinatangazwa kupitia UTUMISHI ,na tumeona UMATI wa watu wengi wakijitokeza pale DUCE kwa ajili ya usahili .

Juzi juzi tumeona msururu mrefu wa vijana pale uwanja wa mkapa tena wahitimu wakiwa wanagombea kuingia kwenye usahili wa nafasi za muda za NEC,Mhe Rais hii inaonesha vijana wako wana ARI ya kufanya kazi kwa bidii ndo mana wanastahimili kukaa kwenye foleni ndefu za kungojea usahili.

Huku kwenye sekta binafsi Mhe, taasisi binafsi zinawatumia vijana hawa kwenye INTERNSHIPS na VOLUNTEERING zisizo na mwisho,kweli kuna kujitolea kwenye kupata ujuzi wa kazi lakini kuna makampuni yanawatumia hawa vijana kwenye shida zao kwa KUWANYONYA nguvu zao na kutowapatia japo kifuta jasho.

Mhe Rais sisemi uchukue vijana wote utoe AJIRA kwao,la hasha bali Serikali yako tukufu inaweza ikaandaa mikakati ya kutosha kwenye hili suala mfano Serikali iandae Mazingira wezeshi ya vijana kujiajiri,Serikali iandae program za kuwanoa vijana kwenye suala la ajira,pale TAESA wanajitahidi ila sio sana.
Serikali iangalie fursa za ajira kwa vijana wake pia nnje ya Tanzania mfano kiswahili kinakua sana africa na duniani kwa ujumla na tuna wahitimu wengi watalaamu wa kiswahili.

Mhe Rais madamu umesema unajua kwamba "Vijana WANADHARAULIKA basi fanya kitu kwa kundi hili "

Serikali yako tukufu iandae hata miswada iende bungeni ikawe sheria kuhusu mazingira wezeshi ya ajira kwa hawa vijana wako.

Mhe ,kama tulivyokomaa kwenye kupandisha uchumi wa nchi yetu basi tukomae hawa vijana wawe pia kwenye daraja la kati kwenye upatikanaji wa ajira na mazingira wezeshi ya ajira (Favourable).

Na umesema leo suala hili la ajira UTALISHUGHULIKIA kwa NGUVU zote basi sisi hatuna shaka na wewe.,MUNGU akupe nguvu kwenye hili,ulikumbuke na vijana wa Tanzania watakukumbuka sana.

Ulikua na mambo mengi sana,programs nyingi sana zipo kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili na umekua nazo bize sana kwenye kuhakikisha zinatekelezwa basi sasa ni muda muafaka wa kutumia miaka mitano inayokuja kushughulikia japo kwa asilimia 70 suala la Ajira kwa vijana.

Mhe Magufuli hakuna kama wewe,hakuna chama dume na bora kama CHAMA CHA MAPINDUZI katika kuongoza nchi.

Kama kijana mzalendo wa nchi hii sioni chama kingine cha kuwapa ridhaa ya kuongoza taifa hili kubwa kama chama chetu Tawala cha CCM.

Nirudie tu kwa kauli yako ya leo umenitia sana moyo na umetupa moyo na umerudisha matumaini kwenye vile vipande vipande vya mioyo ya vijana iliyokua imepasuka kwa ajili ya mahangaiko na husstles za kutafuta ajira kwa miaka mitano.

Naamini pasi na shaka haukusema hili la leo ili vijana tu wakupe kura,nimeona kwa macho yangu na kuamini moyoni ulilisema hili ukiwa UNAMANISHA toka ndani ya MOYO wako.,kiukweli kwa serikali kutotoa ajira kwa kipindi cha miaka mitano kimefanya kuwe na jam' kubwa sana ya wahitimu huku mitaani.

Kama serikali ingalitoa ajira toka mwaka 2015 ,tungekua na angalau haueni' kwenye soko la ajira.,kusingekua na mlundikano wa wahitimu,imefikia hatua mpaka baadhi ya watendaji wa juu wa serikali yako wanatonesha vidonda vya wahitimu hawa kwa kauli zao zisizo na staha pasi kujali Mioyo ya vijana hawa iliyopondeka pondeka.

Nimalize kwa kusema Mhe Rais Magufuli umetupa Tumaini Jipya leo kwa vijana wote wa kitanzania kwenye suala hili la ajira na Kwa niaba ya vijana wote wa Taifa hili nakuombea Afya njema na Ulinzi wa MUNGU uwe pamoja nawe kwenye kufanikisha Maono yako kwa Taifa hili.

MUNGU ibariki Tanzania.

MUNGU Ibariki Africa.

Kwa maoni na ushauri usisite kumuandikia Muandishi kwenye barua pepe godjohn8@gmail.com

CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEE.....!
Andishi refu pumba tupu.
Nakushauri ulipeleke Uhuru media na sio hapa ili misukule wenzio walisome
 
moyoafricatz umeonesha kuwa una matumaini na matumaini hayo yatakuinua.

Nimebahatika kupata na kuisikiliza "video clip" ya wafanyabiashara wa Arusha, wengi wao ni vijana. Tofauti na wasemavyo wapinzani kuhusu Rais Magufuli, ebu wasikilize.

Katika "clip" hiyo, kuna mengi ya kujifunza, kupokea na kuyafanyia kazi badala ya kuilaumu Serikali kuhusu ajira. Wajibu wa Serikali ya kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara unatoa fursa zaidi siyo tu za kiuchumi pia ajira au kujiajiri.

Hebu tuambie mazingira gani mazuri yamewekwa ya kufanya biashara hapa Tanzania. Kuanzisha biashara leo ni ngumu zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 10 iliyopita!

Acheni Propaganda sisi wengine tuna deal moja kwa moja na wafanyabiashara kila siku tunajua maumivu yao na hawana pa kusemea. Kila.mmoja anaogopa.
 
Sio Rahisi kwa Kiongozi mkubwa ku-admit mateso ya vijana..

Na kakiri kwamba ATALISHUGHULIKIA suala la ajira kwa NGUVU zote.

Msema kweli ndie mpenzi wa MUNGU .

Vijana twendeni pamoja na Rais Magufuli.View attachment 1598263

Mtu mwenye akili, akikuambia jambo la kijinga na wewe ukamkubalia, atakudharau - Mwl. Nyerere
Maguful anatudharau sana huyu... Matatizo kayatengeneza yeye mwenyewe, kashindwa kuyatatua alafu leo anakuja kututhibitishia anavyotudharau...
Ni akili ndogo tu ndo watampigia kura hili dubwasha...!
 
Hujui unachoongea kuhusu ajira na hii Ni siasa tu mzee
Mzee Ana miradi mikubwa inayohitaji pesa nyingi Sana ambayo kuitekeleza Ni Pasua kichwa kwake kuajiri, kuongeza mishahara na vyeo,kulipa mafao Ni hasara hiyo pesa Ni Bora apeleke kwenye miradi yake ili aonekane mwamba kafanya makubwa

Lakini anajaribu kuweka Mambo sawa kujibu hoja za wapinzani lakini kiukweli anatafuta dhamana tu akipita itakuwa imepita pia
Huyu jamaa Kawa mnyenyekevu juzi tu na wananchi walivyokuwa wasahaulifu wameshamsahau
kagundua Mambo Ni tofauti na alivyodhani ndiyo maana kajirudi kuwa mnyonge
Lakini akipita msimu huu Hana Cha kupoteza Tena huu ndiyo itakuwa msimu wa kulimia meno kwelikweli
Kwa sababu nguvu anayotumia kwenye kampeni na pesa anayotumia lakini bado wananchi hawamuelewi
Kama atashinda Ni kwa nguvu zake binafsi na analifahamu Hilo kwa hiyo kazi mnayo itakuwa Ni mwendo wa visasi tu

Unajua mtu akitaka kufanya Jambo kwa Siri akikaa nalo moyoni Kuna namna anaweza kuwa ameliongelea kwa namna fulani lakini wengine sio rahisi mkaelewa alichomaanisha
Yaani hatokuwa na mpango
Na majimbo ambayo upinzani utashinda
Sasa mtu wa aina hiyo hafai kuwa kiongozi wa nchi
Majimbo yenye wabunge wa upinzani walipelekewa maendeleo ili kuwafanya wananchi waone kwamba ccm Ni Bora kuliko hao wapinzani lakini wenye akili huwa tunatambua mchango wa viongozi wetu kwamba kupitia hao tumepata maendeleo kupitia ccm yaani Kama Jimbo lingekuwa ccm hata hayo maendeleo tusingepata kwa kuwa tayari tungekuwa kwenye himaya ccm huwa wanadeal na majimbo muhimu ambayo yako upinzani na wanayahitaji kwelikweli
 
moyoafricatz umeonesha kuwa una matumaini na matumaini hayo yatakuinua.

Nimebahatika kupata na kuisikiliza "video clip" ya wafanyabiashara wa Arusha, wengi wao ni vijana. Tofauti na wasemavyo wapinzani kuhusu Rais Magufuli, ebu wasikilize.

Katika "clip" hiyo, kuna mengi ya kujifunza, kupokea na kuyafanyia kazi badala ya kuilaumu Serikali kuhusu ajira. Wajibu wa Serikali ya kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara unatoa fursa zaidi siyo tu za kiuchumi pia ajira au kujiajiri.

Uvccm ndio wafanya biashara?
 
1.Somesha watu namba ili wakuabudu
2.komoa na washughulikie washushe wawe masikini wafanyabiashara haswaa Hadi wakimbie wa nje,wenye pesa wote ni wamepiga dili.
3.Ua sekta binafsi kazi zote wape suma jkt.
4.Vunja vunja kabisa diplomasia ili export ife
5.Ua demokrasia na Uhuru
6.Ondoa punguza mzunguko wa pesa mtaani
7.Nyima watumishi haki zao za kikatiba za nyongeza za mishahara ili ajira binafsi zife
8.ongeza Kodi kila sehemu ili ukusanye kingi mara moja hata biashara zife we ushapata Kodi yako
9.Ua competition kwa kufanya monopoly biashara zote miliki wewe.

Hizi ni sera za kikomunisti za kuwafanya watu wawe masikini ili uwatale anaegoma kukuabudu mshughulikie mtumie Uhamiaji,tra,mpe uhujumu uchumi kisha ficha file lake aozee ndani milele au atoe pesa kununua Uhuru wake.

Wenzetu waliona mbali Sana huwezi pewa uongozi Kama una poverty mind
 
Vijana waTz watakuwa na ujinga ikiwa leo hii ndio wanapewa kipaumbele wakati kwa miaka 5 walibebeshwa kauli za "jiajiri"

Salama unaoongolewa leo ni wa Ben kupotea kama kiberiti, azory kupotea kama sh 50 kwenye mchanga na watukupigwa kusingiziwa kesi za ml ama usalama gani?

Ninawaasa mkitaka mlimie meno this time wapeni CCM nchi
@godjohn8@gmail.com, mwenye mawasiliano hayo ni mvivu kufikiri yahani anaamini kuwa haiwezekani kulinda amani na kuajiri???, Yahani kuimarisha amani kunazuia waalimu watumwe kwenda kufundisha, ma dr. kwenda kutibu!!!....... Miaka 5 inatosha kuwaonesha kuwa Magufuli hana mpango na ajira, zote za serekali na binafsi, hana kabisa mpango huo na anajitahidi kupunguza payroll ya serekali iwe ndogo iwezekanavyo.
Hawa vijana wasiojifunza hata kwa kuona wanasaidiwa vipi?. Subirini aapishwe wakione cha mtema kuni.
 
Kwenye ilani wanadai wameajiri 6M.

Kwenye kampeni wanatuambia kama tumeweza kujenga flyovers vijana sitoshindwa kuwaajiri, that means zile ajira 6M kwenye ilani sio kweli.

Yani statement inayotoka leo lazima ikinzane na ya kesho au juzi.

Kwani kijani mnakwama wapi?
Kama hujawahi kuchanganyikiwa na unatamani uchanganyikiwe sikiliza kauli za mzee baba kwenye kampeni zake. Kama aliwaahidi wafanyakazi mishahara minono na maslahi mazuri katika kampeni zilizomuingiza madarakani 2015 na wafanyakazi hawakumuangusha matokeo yake kila mtu anajua. " nitapunguza mishahara mikubwa mikubwa, mingine itabaki hivyo hivyo na sina mpango wa kuongeza" .
Hiyo ya ajira kwa vijana ni gia ya kupatia kura na kasema vijana ni 60% ya wapiga kura wote. Sasa akili kwenu vijana.
 
viwanda vimemshinda, wafafanyabiashara kawavuruga wamehamisha mitaji yao hizo ajira atazitoa wapi? huyo mzee ni muongo mkubwa.
Alafu ansema kuwa wametengeneza ajira million 6 tangua aingie madarakani. Yahani jamaa ana ndimi 2. Utapeli mtupu.
 
Sio Rahisi kwa Kiongozi mkubwa ku-admit mateso ya vijana..

Na kakiri kwamba ATALISHUGHULIKIA suala la ajira kwa NGUVU zote.

Msema kweli ndie mpenzi wa MUNGU .

Vijana twendeni pamoja na Rais Magufuli.View attachment 1598263
Kila kiongozi mwenye maono huwa kipaumbele cha kwanza ni ajira. Sasa Sasa haha anataka kutwambia hakuona tatizo la ajira wakati anaingia madarakani au hakikuwa kipaumbele kwake kama Fly over.

Mkuu ameshanza kuelewa somo la maendeleo ya watu badala ya maendeleo ya vitu. Lakini kitu anachotakiwa kukisema wazi ni jinsi gani atatengeneza hizo ajira. Hizo fly over na reli wote tunajua ilikuwa ni mipango ya JK na yeye kaitekeleza tu. Kitu alichofanya ambacho hatukuwa kukisikia ni Bwawa la Umeme la Nyerere. So far simuoni kama yuko creative ..... ingawa wote tunajua ni msimamiaji mzuri.
 
Wanabodi,

Huwa siandiki uzi kama sijapata hisia/kuwiwa kuandika ,siandiki kiushabiki ila napenda kushusha nyuzi nikiwa kama kijana mzalendo wa Taifa la Tanzania na mpenda maendeleo.

Huwa napenda ku- declare' kuwa mimi ni mwanachama hai wa Chama cha Mapinduzi lakini sio msifia chochote ili bora liende lakini napenda ku-analyse vitu na kuangalia vina maslai gani kwa taifa.

Kama kijana mzalendo napenda kuungana na watanzania wengine kutambua kazi nzuri iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kipindi hiki tulichowapa dhamana ya uongozi kwenye taifa hili.

Huwa sipendi kuyaelezea waliyoyafanya maana kuna nyuzi nyingi humu zinaelezea maendeleo na mikakati pamoja na miradi mikubwa yenye tija kwa taifa iliyokamilika na ambayo bado iko mbioni kukamilika,hakika hili ni jambo jema sana na Hongera CCM ,Heko Rais Magufuli.

Nautambua uwezo wako shupavu wa kulivusha taifa letu la Tanzania kwenye hiki kipindi cha miaka mitano,kwenye majanga mbalimbali yaliyotokea yakiwemo ajali za majini,hali ya nchi pamoja na hili janga la corona,haikua rahisi kama Taifa kuvuka kwenye vipindi hivi vya mapito.

Mhe Rais ,kama kijana ambae nafahamu hali za vijana wenzangu hasa hasa wale wahitimu kwa kipindi cha miaka mitano toka mwaka 2015-2020 kulikua na changamoto kubwa sana ya ajira .

Na nilipanga niandike uzi wa kuelezea jinsi vijana wanavyohangaika huku na kule kwenye suala hili mtambuka.

Sitaki kujikita sana ndani ndani kwenye vitabu vya muasisi wa Taifa hili la Tanzania akiongolea kuhusu ajira na elimu lakini wote tunajua Mwalimu Nyerere alithamini na kusisitiza sana watu wafanye kazi (ajira).

Mhe Rais,Tuongee ukweli na bahati nzuri wewe ni mpenzi wa MUNGU na ni msema kweli,Serikali imekua muajiri nambari moja kwenye Taifa hili.

Serikali imekua ikitoa ajira almost 80% kwa vijana na watu wote,na imekua ikifanya hivi kwenye idara zake nyingi zikiwemo ajira za majeshi (polisi,jwtz,magereza,zimamoto ,idara ya uhamiaji etc).

Pia Serikali kwa miaka yote imekua ikitoa ajira nyingi kwa madaktari,wahandisi ,waalimu wa msingi na sekondari n.k

Nisingependa kutaja idara zote ambazo Serikali huwa inaajiri lakini Mhe Rais kwa kipindi toka mwaka 2015 mpaka sasa Serikali haijawahi kutoa zile ajira za wengi,kwa maana nyingine tumekua na idadi ya wahitimu wengi wa vyuo vikuu na vyuo vingine toka mwaka 2015 mpaka sasa .

Hii ni kusema tuna graduates wa intake kama 5 au 6 toka mwaka 2015 ambao wengi wao wako mtaani na wameshindwa kujiajiri na wala hawajaajiriwa na sekta binafsi.

Nimesikiliza kwa makini Mkutano wako wa kampeni leo pale segerea,na ukaongelea kipaumbele chako cha kwanza ambacho ulikifanya cha "Kudumisha Amani na Usalama", ukaongelea hali ilivyokua wakati unaingia madarakani ,kwamba hakukua Hali nzuri ya Usalama na ukatoa mifano ya kuuwawa kwa askari kibiti na lile tukio la Ubungo la majambazi kuiba NMB Mhe Rais nikupongeze hapo ulifanikiwa na umefanikiwa sana, HATUNA ujambazi wala wizi wa kutumia silaha tena,hali ni shwari na tunajisikia kweli tuko kwenye nchi yetu.(KONGOLE SANA).

Mhe Rais,kwenye suala la ajira kiukweli kabisa ndani ya kipindi hiki toka 2015 mpaka sasa serikali ni HAIJAFANYA vizuri kwenye hii sehemu.

Kuna sababu nyingi,labda serikali ilikua ina vipaumbele vingine vya haraka sana vya kufanya ndani ya miaka hii mitano,mfano huwezi kuanza na kipaumbele cha Ajira kwa vijana wakati kuna kipaumbele cha haraka cha Amani na usalama wa Raia.

So kwa mantiki hiyo naelewa kwa nini Serikali yetu haikutoa kipaumbele cha AJIRA kwa vijana kwenye miaka hii mitano ya uongozi wako.

Mhe Rais Magufuli, nimesikiliza maneno yako haya ya leo kwa umakini sana na nikayatafakari jioni ya leo ,naomba niyarudie hapa kwa kunukuu ...

" Vijana wanakosa Ajira,Vijana wanadharaulika,Wengine wamemaliza kusoma hawapati Ajira"
"Miaka mitano inayokuja nataka suala la ajira NILISHUGHULIKIE kwa nguvu zote,kama tunaweza kupandisha uchumi,kujenga Flyover,siwezi kushindwa suala la ajira kwa vijana".

Mhe Rais Magufuli, maneno haya na ahadi hii ulikua unaisema ukiwa unamaanisha na naamini imetoka ndani ya sakafu ya moyo wako, na inaonesha wazi unajua kila jambo linaloendelea kwa vijana wako wahitimu wa Tanzania.

Vijana waliosoma kwa kodi za watu maskini,vijana ambao wana matumaini ya kuingia kwenye soko la ajira,vijana ambao umesema wanadharaulika,Tafadhali usiwaache hawa vijana Mhe Rais.

Tumeashuhudia nafasi nyingi za kazi zilizokua zinatangazwa kupitia UTUMISHI ,na tumeona UMATI wa watu wengi wakijitokeza pale DUCE kwa ajili ya usahili .

Juzi juzi tumeona msururu mrefu wa vijana pale uwanja wa mkapa tena wahitimu wakiwa wanagombea kuingia kwenye usahili wa nafasi za muda za NEC,Mhe Rais hii inaonesha vijana wako wana ARI ya kufanya kazi kwa bidii ndo mana wanastahimili kukaa kwenye foleni ndefu za kungojea usahili.

Huku kwenye sekta binafsi Mhe, taasisi binafsi zinawatumia vijana hawa kwenye INTERNSHIPS na VOLUNTEERING zisizo na mwisho,kweli kuna kujitolea kwenye kupata ujuzi wa kazi lakini kuna makampuni yanawatumia hawa vijana kwenye shida zao kwa KUWANYONYA nguvu zao na kutowapatia japo kifuta jasho.

Mhe Rais sisemi uchukue vijana wote utoe AJIRA kwao,la hasha bali Serikali yako tukufu inaweza ikaandaa mikakati ya kutosha kwenye hili suala mfano Serikali iandae Mazingira wezeshi ya vijana kujiajiri,Serikali iandae program za kuwanoa vijana kwenye suala la ajira,pale TAESA wanajitahidi ila sio sana.
Serikali iangalie fursa za ajira kwa vijana wake pia nnje ya Tanzania mfano kiswahili kinakua sana africa na duniani kwa ujumla na tuna wahitimu wengi watalaamu wa kiswahili.

Mhe Rais madamu umesema unajua kwamba "Vijana WANADHARAULIKA basi fanya kitu kwa kundi hili "

Serikali yako tukufu iandae hata miswada iende bungeni ikawe sheria kuhusu mazingira wezeshi ya ajira kwa hawa vijana wako.

Mhe ,kama tulivyokomaa kwenye kupandisha uchumi wa nchi yetu basi tukomae hawa vijana wawe pia kwenye daraja la kati kwenye upatikanaji wa ajira na mazingira wezeshi ya ajira (Favourable).

Na umesema leo suala hili la ajira UTALISHUGHULIKIA kwa NGUVU zote basi sisi hatuna shaka na wewe.,MUNGU akupe nguvu kwenye hili,ulikumbuke na vijana wa Tanzania watakukumbuka sana.

Ulikua na mambo mengi sana,programs nyingi sana zipo kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili na umekua nazo bize sana kwenye kuhakikisha zinatekelezwa basi sasa ni muda muafaka wa kutumia miaka mitano inayokuja kushughulikia japo kwa asilimia 70 suala la Ajira kwa vijana.

Mhe Magufuli hakuna kama wewe,hakuna chama dume na bora kama CHAMA CHA MAPINDUZI katika kuongoza nchi.

Kama kijana mzalendo wa nchi hii sioni chama kingine cha kuwapa ridhaa ya kuongoza taifa hili kubwa kama chama chetu Tawala cha CCM.

Nirudie tu kwa kauli yako ya leo umenitia sana moyo na umetupa moyo na umerudisha matumaini kwenye vile vipande vipande vya mioyo ya vijana iliyokua imepasuka kwa ajili ya mahangaiko na husstles za kutafuta ajira kwa miaka mitano.

Naamini pasi na shaka haukusema hili la leo ili vijana tu wakupe kura,nimeona kwa macho yangu na kuamini moyoni ulilisema hili ukiwa UNAMANISHA toka ndani ya MOYO wako.,kiukweli kwa serikali kutotoa ajira kwa kipindi cha miaka mitano kimefanya kuwe na jam' kubwa sana ya wahitimu huku mitaani.

Kama serikali ingalitoa ajira toka mwaka 2015 ,tungekua na angalau haueni' kwenye soko la ajira.,kusingekua na mlundikano wa wahitimu,imefikia hatua mpaka baadhi ya watendaji wa juu wa serikali yako wanatonesha vidonda vya wahitimu hawa kwa kauli zao zisizo na staha pasi kujali Mioyo ya vijana hawa iliyopondeka pondeka.

Nimalize kwa kusema Mhe Rais Magufuli umetupa Tumaini Jipya leo kwa vijana wote wa kitanzania kwenye suala hili la ajira na Kwa niaba ya vijana wote wa Taifa hili nakuombea Afya njema na Ulinzi wa MUNGU uwe pamoja nawe kwenye kufanikisha Maono yako kwa Taifa hili.

MUNGU ibariki Tanzania.

MUNGU Ibariki Africa.

Kwa maoni na ushauri usisite kumuandikia Muandishi kwenye barua pepe godjohn8@gmail.com

CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEE.....!
Ni kweli baada ya 28/10/2020 apige kote kote kwenye ajira na hayo maendeleo etc ingawa pia tukumbuke dunia inapita kwenye wakati mgumu na hiyo covid-19 etc na tunategemea na mataifa mengine kama UK etc

Unemployment rate hits highest level in three years​

Published19 minutes ago
Related Topics
Breaking News image

The UK unemployment rate has surged to its highest level in over three years as the pandemic continues to hit jobs.
The unemployment rate grew to 4.5% in the three months to August, compared with 4.1% previously.
An estimated 1.5 million people were unemployed in the period, 209,000 more than a year earlier, the Office for National Statistics (ONS) said.
It comes as the government prepares to impose tough local lockdown rules that will force some businesses to close.
Jonathan Athow, the ONS's deputy national statistician for economic statistics, said: "In the latest period almost half a million fewer people were in work than just before the pandemic, while almost 200,000 others said they were employed but were currently not working nor earning any money.
"Since the start of the pandemic there has been a sharp increase in those out of work and job hunting but more people telling us they are not actively looking for work.
"There has also been a stark rise in the number of people who have recently been made redundant."

Related Topics​

More on this story​

Back
Top Bottom