Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hongera kwa hoja zilizo na mashiko.
Mimi si mwumini wa demokrasia ya vyama vingi kwenye nchi maskini. Viongozi wa upinzani muda wote ni kuvuruga juhudi za Serikali iliyoko madarakani ili ichukiwe na wapiga kura. Wakati huohuo viongozi wa Serikali iliyoko madarakani huogopa kuwachukulia hatua wapinga maendeleo kwa kuogopa kuchukiwa na wapiga kura.
Hicho ndicho kilichotokea toka vyama vya upinzani viasisiwe nchini. Lakini upepo ulibadirika alipoingia Rais Magufuli, mtu asiyeyumbishwa na mthubutu kiasi cha kuwafunga midomo viongozi wa upinzani, wabwabwaji na wenye nia ya kuvuruga juhudi za maendeleo. Matokeo yake kila mtu ameona.
Kwa kuwa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, ambazo sasa zitanaongozwa na Chama kimoja, tutegemee maendeleo makubwa yatakayotokana na ushindani chanya na hai kati ya Halmashauri zote, na ndani ya Halmashauri (kwa maana ya Majimbo/Kata za uchaguzi).
Kenya hapo wana mfumo wa vyama vingi wenye nguvu, wanatuzidi kwa mbali sana kiuchumi. Au huku kwetu viongozi ni akili ndogo kiasi kwamba hawawezi kufanya kazi wakiwa na wapinzani? Enzi za Nyerere wakati tunavaa viraka ilikuwa ni chama kimoja, mbona hatukufikia kwenye hayo matamanio yako?