Rais Magufuli: Wafanyakazi msidanganywe serikali imepandisha mishahara kwa kupandisha madaraja na kupunguza kodi ya PAYE

Rais Magufuli: Wafanyakazi msidanganywe serikali imepandisha mishahara kwa kupandisha madaraja na kupunguza kodi ya PAYE

Rais Magufuli amesema ziko namna nyingi za kupandisha mishahara ikiwemo kupandisha madaraja watumishi na kupunguza kodi ya wafanyakazi PAYE.
Hivyo serikali imeamua kutumia njia hii na watumishi wote wananeemeka.

Rais Magufuli amewataka wananchi kumpuuza mgombea urais anayesema watumishi wa umma eti wameokotwa majalalani.
Source ITV

Maendeleo hayana vyama!
Magufuli aache uongo. Labda kama kapandisha madaraja wafanyakazi wa ikulu. Mie kuna ndugu yangu ana miaka 7 kazini ananiambia hajapandishwa daraja kazini.

Ni ukweli pia hajaongeza mishahara kwa miaka 5 na alichofanya mwaka huu wa fedha tena juzi mwezi wa saba baada ya kuona kampeni inakuja ndo akashusha kodi kidogo. Kule ni kuwalaghai wafanyakazi kwa sababu kwa nini hakufanya miaka yote nyuma amefanya juzi mwezi wa saba huku akijua kampeni zinaanza mwezi wa nane!!!

Jambo lingine ni pensioen. Watumishi wengi waliostaafu mwaka 2018,2019 na mwaka huu 2020 hawajalipwa pension zao. Wakifuatilia psssf wanaambiwa kuwa mfuko hauna hela. Kumbe yeye kabeba hela kaenda kujenga uwanja chato na kununua mandege
 
Hakuna BABA wa hovyo na wa familia hapa duniani, kama yule BABA muongo! Ukishaizoea tabia ya uongo kama mzazi, hakika watoto wako nao watakudharau, watakuchukia na pia watashindwa kukuamini kwa lolote.
 
Magufuli alitenga kasiku kabisa ya kuwajibu wafanya kazi.
Kunasiku alisema kabisa kua siwezi kuacha kujenga madaraja eti naongeza mshahara,kama hautaki kazi uache.
Katika sikukuu ya wafanya kazi pia aliwahi kusema kua aneona mshahara hautoshi aache kazi,kunawatu wanatakaka kazi watafanya.
magufuli amezoea kuchezeavichwa vya wapumbavu,lakini hapa kwa wafanya kazi hatocheza hata na pua ya mtu.
 
Rais Magufuli amesema ziko namna nyingi za kupandisha mishahara ikiwemo kupandisha madaraja watumishi na kupunguza kodi ya wafanyakazi PAYE.
Hivyo serikali imeamua kutumia njia hii na watumishi wote wananeemeka.

Rais Magufuli amewataka wananchi kumpuuza mgombea urais anayesema watumishi wa umma eti wameokotwa majalalani.
Source ITV

Maendeleo hayana vyama!
Sasapo ameonge nini
 
Uongo mtupuuu.Miaka 5 hakuna ongezeko,hawajalipwa malimbikizo yao,hawajapanda madaraja wala nini.Utapeli mtupu.

Watumishi wana hasira za sirisiri
Huyu Mzee muongo sana, kuna watu wameajiriwa kuanzia 2013 hakuna nyongeza ya mshara au kupanda daraja, na ni lini vitu viliacha kupanda bei??
 
Kwahiyo kodi imepunguzwa kwa miaka 5 iliyopita au kuanzia mwezi huu tu?
Vinginevyo wafanyakazi wamilikishwe kampuni za sgr stigler na mabenki ili wawe wanapata gawio.
 
Ina maana Magufuli hajui nini maana ya Mshahara kwa mfanyakazi?

Ngoja nimpe shule rahisi hapa.
Unaposhusha PAYE, hapo maana yake umepunguza makato ya kodi kwenye mshahara ghafi, lakini mshahara (Basic salary) unabakia ule ule. Na sio lazima mtumishi aone tofauti ya kile atakachopokea (Take home), maana PAYE inatofautiana kati ya mtu na mtu, kulingana na ngazi ya mshahara. PAYE iliyoshushwa na serikali mwaka 2016 iligusa mshahara wa kima cha chini, kwa zaidi ya 80% ya wafanyakazi hilo lisingewagusa kikamilifu.

Pili unapompandisha mtumishi daraja sio kwamba umeongeza mshahara bali umembadilisha mtumishi ngazi ya mshahara, hilo ni takwa la kisheria (sio huruma wala busara za mwajiri yaani serikali), na sio lazima mshahara uongezeke(take home), sio kila mtu hilo litamuhusu.
 
Magufuli: "Watz sio wajinga"

Mwisho wa kunukuu....
 
Kushusha PAYE na kupandisha madaraja huko sio kupandisha mshahara na wala sio mbadala wa kupandisha mshahara.
 
Huyu mtu n muongo sipata kuona.
Mtoto wangu akiichagua CCM bora nilinyonge likafie mbali huko.
 
Rais Magufuli amesema ziko namna nyingi za kupandisha mishahara ikiwemo kupandisha madaraja watumishi na kupunguza kodi ya wafanyakazi PAYE.
Hivyo serikali imeamua kutumia njia hii na watumishi wote wananeemeka.

Rais Magufuli amewataka wananchi kumpuuza mgombea urais anayesema watumishi wa umma eti wameokotwa majalalani.
Source ITV

Maendeleo hayana vyama!
Na hatudanganyiki kweli ,HATUJAONGEZEWA MISHAHARA!
 
Aisee nkajua amefufuka,..kumbe Ni post ya 2020..
Katika maisha yangu siwezi kumsahau huyu mtu..nliishi maisha ya kero tangia 2015..
 
Back
Top Bottom