Hapa ndipo nimejifunza kama watu ndani ya taifa hili tukiamua kusimama na kupigania haki zetu kwa pamoja hakika tungeshinda kila vita inayokuja mbele yetu.
Uoga ni dhambi, na dhambi huzaa mauti; tatizo letu tu waoga, wengine ni wavivu wa kusubiri mpaka wengine waanze, na wale wachache wasiojielewa wanaojipendekeza kwa watawala hata kama baadhi ya maamuzi ya hao watawala yanawaumiza mpaka wao.
Kwa hili niwapongeze viongozi wa dini kwa kuonesha njia na uthubutu, naamini sasa wameuona umuhimu wao katika kuongoza kondoo wao kwenye njia sahihi, na wajue pia, popote wanapochelewa kuchukua maamuzi sahihi, wanasababisha kuchelewesha ukombozi wa watanzania.