Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Hizi promo za nyungu na coctail za limau,tangawizi n.k ni hatari.

Nina miti kibao hapa home ya limao nikaenda kariakoo chini nikachukua mzigo wa tangawizi, vitunguu vyote vipo, blender iko standby,nilishaanza kujipa matumaini kwamba nikihisi tu kwa mbaaaaali kuna ki covid kinanyemelea fasta na mix coctail kui flush out.( false hope !??)

Sasa sina uhakika tena kila mtu anasema lake, walilosema jana hao hao wanasahau jana walisema kitu gani leo wanasema kupinga walichosema jana yake.

Kwa jinsi hiyo nitaamini vipi na yote mengine wanayosema kama yana ukweli.

Kwasababu ft 6 chini nitachimbiwa peke yangu naona zakuambiwa nizifanyie filtering halafu nichanganye na zangu.
 
Tiyari ameanza kukubali taratibu, nilivyokuwa nasikia namna anavyozungumza Majaliwa kwenye Msiba wa Balozi kijazi nikajua kabisa anasafisha njia kwa Jiwe kukubali Corona ipo nchini na watu wanapaswa kuchukua taadhari

Mimi nashauri angehutubia Taifa moja kwa moja kuhusu hili suala linalogharimu maisha ya watu na siyo kujificha makanisani kutoa matamko ya chini kwa chini kwa Jambo serious kama hili
DuH Bado hujaridhika.....!
 
Wahanga wa cororna walitakiwa wawe traced na watibiwe eneo maalum sio kujichanganya hospital na wagonjwa wengine. Na pia ukishajua huyu ni mgonjwa wa corona unatakiwa atibiwe kwa tahadhari lakini imekuwa kinyume. Wagonjwa wa covid wametapakaa kwenye zahanati

Wafadhili ndio nao mmewajibu kwa nyodo, msaada wa corona ndo basi tena. Kkila mwananchi apambane kivyake.
Wale wazee wasio na hata hela ya kula wakiumwa wakimbilie wapi?
Ni hatari

Serikali ya ovyo
Ni hatari kubwa wagonjwa wa corona kutibiwa kwenye zahanati
 
Sema una ombwe kwa sababu wewe siyo msemaji wa Watanzania. Je, wewe umezuiiwa kuifuata hiyo miongozo?
hujielewi, kama ni free rider na unaogolea kwenye anasa za uongozi huu mbovu, omba, tena omba sana, haka kamdudu Mungu afanye jambo kaondoke, ama sivyo huyu mtu wenu hakakwepi this time around.

hakuna mtu amewahi cheza na moto usimuunguze.
 
Anabana kushoto huku kulia anaachia taratibu. Kifuatacho itv atoke front line kumaliza huo ukakasi na vizuri iwe press ya taifa isiwe ile ya makanisani au kwenye misiba.
 
Pia watu waliokufa kwa Corona wanazikana hovyo na kuongeza maambukizi mara dufu!
Misongamano na kukaribiana na kuchanganyika,
Tukubali tukatae 2020 Lockdown ilitusaidia sana, daladala level seat, basi kuingia tunapuliziwa sanitizer, kushuka sanitizer, misiba hatukurundikana, harusi watu 50,

Kwa ajili ya kuhofu kukosa hela ujenzi, kushuka kwa makusanyo, hawawesemi. Life goes on as usual

Everyday is Saturday............................... 😎
 
He is now coming to his sense.

Alikuwa anawasifia watu wasipovaa barakoa sasa akili inaanza kumrudia.

Alisema corona haipo sasa akili inamrudia kuwa huu msala upo na hauna utani.

Nimesikia sasa anakimbilia kwenye vita ya uchumi, eti hii ni vita ya uchumi, corona ni vita ya uchumi, uchumi gani?
Wewe ni mjinga wa kiwango cha kumzidi shetani kabisa. Serikali kama serikali ule ni ufalme uliosimikwa na Mungu, mambo yote unayoyaona usije dhani yapo kwa bahati mbaya, ni calculated. Uzuri rais wetu anahofu ya Mungu na anamuamni Mungu ndiye mponyaji wa taifa, so ujinga wenu wala si kitu kwake.
 
hujielewi, kama ni free rider na unaogolea kwenye anasa za uongozi huu mbovu, omba, tena omba sana, haka kamdudu Mungu afanye jambo kaondoke, ama sivyo huyu mtu wenu hakakwepi this time around.

hakuna mtu amewahi cheza na moto usimuunguze.
Nilitaka ku laik hii comment naogopa sasa kwenda hela.
 
Back
Top Bottom