Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Hizi promo za nyungu na coctail za limau,tangawizi n.k ni hatari.

Nina miti kibao hapa home ya limao nikaenda kariakoo chini nikachukua mzigo wa tangawizi, vitunguu vyote vipo, blender iko standby,nilishaanza kujipa matumaini kwamba nikihisi tu kwa mbaaaaali kuna ki covid kinanyemelea fasta na mix coctail kui flush out.( false hope !??)

Sasa sina uhakika tena kila mtu anasema lake, walilosema jana hao hao wanasahau jana walisema kitu gani leo wanasema kupinga walichosema jana yake.

Kwa jinsi hiyo nitaamini vipi na yote mengine wanayosema kama yana ukweli.

Kwasababu ft 6 chini nitachimbiwa peke yangu naona zakuambiwa nizifanyie filtering halafu nichanganye na zangu.
 
DuH Bado hujaridhika.....!
 
Ni hatari kubwa wagonjwa wa corona kutibiwa kwenye zahanati
 
Tayari kwenye mabank duniani huko lazima kuna alert imetolewa sio bure
 
Sema una ombwe kwa sababu wewe siyo msemaji wa Watanzania. Je, wewe umezuiiwa kuifuata hiyo miongozo?
hujielewi, kama ni free rider na unaogolea kwenye anasa za uongozi huu mbovu, omba, tena omba sana, haka kamdudu Mungu afanye jambo kaondoke, ama sivyo huyu mtu wenu hakakwepi this time around.

hakuna mtu amewahi cheza na moto usimuunguze.
 
Anabana kushoto huku kulia anaachia taratibu. Kifuatacho itv atoke front line kumaliza huo ukakasi na vizuri iwe press ya taifa isiwe ile ya makanisani au kwenye misiba.
 
Pia watu waliokufa kwa Corona wanazikana hovyo na kuongeza maambukizi mara dufu!
Misongamano na kukaribiana na kuchanganyika,
Tukubali tukatae 2020 Lockdown ilitusaidia sana, daladala level seat, basi kuingia tunapuliziwa sanitizer, kushuka sanitizer, misiba hatukurundikana, harusi watu 50,

Kwa ajili ya kuhofu kukosa hela ujenzi, kushuka kwa makusanyo, hawawesemi. Life goes on as usual

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Wewe ni mjinga wa kiwango cha kumzidi shetani kabisa. Serikali kama serikali ule ni ufalme uliosimikwa na Mungu, mambo yote unayoyaona usije dhani yapo kwa bahati mbaya, ni calculated. Uzuri rais wetu anahofu ya Mungu na anamuamni Mungu ndiye mponyaji wa taifa, so ujinga wenu wala si kitu kwake.
 
hujielewi, kama ni free rider na unaogolea kwenye anasa za uongozi huu mbovu, omba, tena omba sana, haka kamdudu Mungu afanye jambo kaondoke, ama sivyo huyu mtu wenu hakakwepi this time around.

hakuna mtu amewahi cheza na moto usimuunguze.
Nilitaka ku laik hii comment naogopa sasa kwenda hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…