Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Haa haa. Something is very wrong in upstairs. Hata hajui kuwa barakoa hazivaliwi muda wote mpaka unapokuwa umelala au uko nyumbani. Anajifanya hajui kuwa barakoa ni pale unapokuwa kwenye msongamano wa watu wengi tu.
Nanukuu tena... "Siku ina masaa 48"
 
Tiyari ameanza kukubali taratibu, nilivyokuwa nasikia namna anavyozungumza Majaliwa kwenye Msiba wa Balozi kijazi nikajua kabisa anasafisha njia kwa Jiwe kukubali Corona ipo nchini na watu wanapaswa kuchukua taadhari

Mimi nashauri angehutubia Taifa moja kwa moja kuhusu hili suala linalogharimu maisha ya watu na siyo kujificha makanisani kutoa matamko ya chini kwa chini kwa Jambo serious kama hili
kukubali Nini?!!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Ni vema akalihutubia Taifa ili kuweka mwongozo thabiti dhidi ya Corona.
 
He is now coming to his sense.

Alikuwa anawasifia watu wasipovaa barakoa sasa akili inaanza kumrudia.

Alisema corona haipo sasa akili inamrudia kuwa huu msala upo na hauna utani.

Nimesikia sasa anakimbilia kwenye vita ya uchumi, eti hii ni vita ya uchumi, corona ni vita ya uchumi, uchumi gani?
Kwenye corona ukijitoa ufahamu na kujitia una roho ngumu lazima unyooshwe.
 
Hapa ndipo nimejifunza kama watu ndani ya taifa hili tukiamua kusimama na kupigania haki zetu kwa pamoja hakika tungeshinda kila vita inayokuja mbele yetu.

Uoga ni dhambi, na dhambi huzaa mauti; tatizo letu tu waoga, wengine ni wavivu wa kusubiri mpaka wengine waanze, na wale wachache wasiojielewa wanaojipendekeza kwa watawala hata kama baadhi ya maamuzi ya hao watawala yanawaumiza mpaka wao.

Kwa hili niwapongeze viongozi wa dini kwa kuonesha njia na uthubutu, naamini sasa wameuona umuhimu wao katika kuongoza kondoo wao kwenye njia sahihi, na wajue pia, popote wanapochelewa kuchukua maamuzi sahihi, wanasababisha kuchelewesha ukombozi wa watanzania.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwahiyo hii kauli tu ya kwamba vaeni barakoa ndio mlikuwa mnaipigania?

Vituko haviishi duniani
 
Kwahiyo mmeridhika, hadi muambiwe mvae barakoa ndio mfurahi. Vaeni sasa baba yenu kasema
Mkuu kauli ya kiongozi ina mamlaka na ni rahisi watu kuitii, kiongozi sio sawa na wewe anapoongea.

Rais akiongea utopolo kuna watu wanajazwa utopolo
Akiongea sense kuna watu wanapata sense.

Take it to the head.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwahiyo hii kauli tu ya kwamba vaeni barakoa ndio mlikuwa mnaipigania?

Vituko haviishi duniani
Sasa unavaaje barakoa wakati naniiii..... haipo TZ??
 
Hii paragraph imehitimisha nia ya serekali katika kupambana na janga la corona ni ipi.

Imagine social distancing pamoja na kuvaa barakoa vimepondwa na kuonekana kuwa havina maana na maombi yamewekewa msisitizo!View attachment 1708025
Magufuli ana ugomvi binafsi na mzee Barakoa. Inabidi wapatanishwe kama hawajaumizana.
 
Back
Top Bottom