Rais Magufuli, wateule wako hawakucheleweshi kwa shughuli za maendeleo tu, wanakuchelewesha pia kuifanya Tanzania nchi ya utawala bora

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kauli uliyoitoa jana mkuu wa nchi yetu inatia moyo, maana umetambua wazi kuwa wateule wako wengi hawaendani na kasi yako. Mbali na hilo wengi ni wacheza maigizo kwenye luninga ya taiifa yaani TBC wakijifanya wanatekeleza ilani ya CCM.

Kama hata wewe mkuu wa nchi umetambua kuwa wateule wako ni waigizaji kwenye runinga huku miradi mingi haijatekelezwa basi tambua kuwa sio kuwa wateule wako hawaigizi kwenye utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo tu, bali hata usimamizi wa sheria ili utawala wa sheria uwepo( utawala bora).

Tulitegemea awamu ya tano, unyanyasi wa raia kutoka kwa vyombo vya dola upungue, kubambikia kesi raia wanyonge kupungue na viongozi kuchukua sheria mkononi kusiwepo. Lakini tunaona ni kinyume kabisa na jinsi ulivyotuaminisha kipindi unachukua madaraka 2015.

Pia soma:
 
Mzizi wa matatizo yote ni rais mwenyewe, hana kanuni za utendaji na hasikilizi washauri.
Very true

Jiwe ndiyo tatizo nchi hii, kwa kujifanya yeye ni mungu mtu, ambaye akiamua kitu, hata kama kiko kinyume cha sheria, lakini nyinyi watendaji wake ni lazima mkitekeleze!

Kinyume cha hapo, unakaribisha kutumbuliwa!
 
Mi natamani awe anakaa kimya tu. Maana kila akisimama akitoa kauli analeta taharuki. Yeye kila speech ni kujimwambafy na kulaumu wenzake tuuuuuu. Hivi yeye ni kuwa huwa hakosei au? Kulaumu watendaji wake, kulaumu nchi nyingine na kuna siku atamlaum Mungu japo anajifanya mkristo kiliko Ukristo wenyewe.
 
He got into power by fluke same way like Trump and He will leave shamefully in the same manners like trump as well ...

Ni swala la muda tu subirini mtaona ...

Endeleeni kuota .. jembe halipo kwa bahati mbaya ..
 
Kauli uliyoitoa jana mkuu wa nchi yetu inatia moyo, maana umetambua wazi kuwa wateule wako wengi hawaendani na kasi yako. Mbali na hilo wengi ni wacheza maigizo kwenye luninga ya taiifa yaani TBC wakijifanya wanatekeleza ilani ya CCM.

Kama hata wewe mkuu wa nchi umetambua kuwa wateule wako ni waigizaji kwenye runinga huku miradi mingi haijatekelezwa basi tambua kuwa sio kuwa wateule wako hawaigizi kwenye utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo tu, bali hata usimamizi wa sheria ili utawala wa sheria uwepo( utawala bora).

Tulitegemea awamu ya tano, unyanyasi wa raia kutoka kwa vyombo vya dola upungue, kubambikia kesi raia wanyonge kupungue na viongozi kuchukua sheria mkononi kusiwepo. Lakini tunaona ni kinyume kabisa na jinsi ulivyotuaminisha kipindi unachukua madaraka 2015.

Pia soma:
Na wanamuangusha kinoma, inasikitisha sana sana..
 
He got into power by fluke same way like Trump and He will leave shamefully in the same manners like trump as well ...

Ni swala la muda tu subirini mtaona ...
Natamani sana huo muda ufike! Haiwezekani mtu mmoja tu na kwa utashi wake binafsi awadhulumu wafanyakazi stahiki zao kwa sababu za hovyo hovyo tu.
 
Back
Top Bottom