Rais Magufuli: Wengine wanasema nipo Chato, kwani waliambiwa Chato sitakiwi kuwepo? Hapa si ndio nilipozaliwa na hata nikifa nitazikwa?

Sio kwamba napingana na hoja za watu wengine, ambao wamekuwa wakitoa shinikizo la Rais kutoka Chato na kurudi Ikulu ya Dar es salaam au Dodoma. Ila najaribu kujiuliza haya maswali;

i) Je, utendaji wa Rais unapimwa kwa mambo anayofanya au unapimwa kwa mahali alipo?

ii) Je, Rais akiwa tu Chato au sehemu ingine yoyote Tanzania ambapo hakuna Ikulu, atakuwa anakosa moja kwa moja nguvu ya kuwa Rais?

iii) Kuna umuhimu gani haswa wa kuwa na shinikizo la kutaka Rais atoke Chato na aje ikulu?


Mi nahisi vitu vingine hivi ni kufuata tu mkumbo wa nani anasema kitu gani, iihali kuna wana harakati wanasema kwamba Rais atoke Chato aje ikulu, basi imekuwa kama hoja ya kujadiliwa, wakati ukiangalia kwa jicho la tatu, hakuna mantiki haswa nyuma ya hili jambo.

Kwangu mimi kwa kweli, sioni kama kungekuwa na tofauti yoyote kwenye hili janga la Corona hata kama Magufuli angekuwa huko ikulu watu wanapotaka awepo. Magufuli ni mtu yule yule akiwa Dodoma, Dar, Chato na popote pale.

Yaani watu wanavolalamika Rais arudi Ikulu, utasema kuna chochote kitachobadilika.
 
Raisi kuwa dar haina impact physically bali psychologically..yaani kumuona mkuu wa nchi yuko kwenye Frontline wakati wa vita inatia hamasa kupambana..

Hata kama physically kazi anaweza kufanyia akiwa hata kwenye handaki kajificha lakini tukimuona na yeye tunapata morali..

Ni hayo tu.. BTW yeye ndio rais anachotaka afanye hakuna wa kumuamlia.
 
Nimekuelewa sana, ila linapokuja suala la Rais ni Magu, ni mara chache sana mtu unaweza kuwa impressed Psychologically.
 
Itabdi na watendaji wa kata wafanye ile kitu inaitwa 'work from home'.
 
Wanaotaka Rais atoke Chato ni hao wanaoagizana kujifungia ndani. Imekula kwao
 
Na wengine wanakuita wewe ni CHATU.
Litolee ufafanuzi na hilo.
 
Angalau ukitumia lugha ya staha inakutofautisha na wasio na adabu kwa waliowazidi umri, sembuse Rais wa nchi?, Nafikiri hata Rwanda au Uganda usingepata muda huu ulioupata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…