Rais Magufulli hawazii tena kuleta maendeleo ya Nchi ya Tanzania

Biggest solution ni katiba mpya ile ya warioba

Otherwise hao kina bashite na the like watakwara kila kitu hapo bongo
 
Na bado ! Mtakuja sana kutubu humu wenyewe kudadeki ! tuliwaambia , Wanafiki wakubwa nyie !
Na kweli

Mwanzo niliposoma, nilijiuliza hivi ndiyo huyu huyu britanicca, mshabiki kindaki ndaki wa Jiwe, ndiye aliyezishusha nondo hizi??

Na bado, watanzania wote tutafika mahali kumpinga huyu Jiwe kwa ngivu zote, kutokana na siasa zake za visasi, kuminya demokrasia, kulitumia Bunge ambalo lina wanaccm wengi kwa manufaa yake binafsi,kufanya double standard katika maumuzi yake, kuongeza umaskini kwa watanzania walio wengi, etc
 
Haha umenichekesha kwamba Magufuli mwenyewe ndo maendeleo
 

Wale waliokuwa na jeuri ya kwamba unanijua mimi ni nani sasa hivi yamerudi kwa hao hao waliosababisha hiyo jeuri. Ukijaribu kuangalia waliokuwa wanasema hivyo walikuwa wanatumia viongozi walioko madarakani au wakuu wa vyombo vya dola kuonyesha jeuri yao. Sasa hivi tunaona viongozi kama maDC, maRC, viongozi wa ccm nk wakionyesha jeuri hiyo ya kwamba unanijua mimi ni nani? Sasa hivi hata kiongozi wa ngazi ya chini tu wa ccm naye anasema unanijua mimi ni nani. Haya mambo tunayaona kwa macho yetu.

Nidhamu ingekuwa imerejea serekalini tusingesikia yale yaliyozungumzwa mbele ya rais na wafanyabishara. Kilichofanyika hivi sasa ni kuhakikisha vyombo vya habari vimezibwa mdomo ili watu walishwe taarifa atakazo rais tu, matokeo yake hadithi zinazosikika ni zile tu zinazomfurahisha rais huku ukweli mwingi ukiwa marufuku kuwafikia wananchi. Haya yanayoendelea ndani ya nchi hii ni kujaribu na kulazimisha wananchi wote waishi kwa mawazo ya rais tu, na inatumika nguvu kubwa kutii utashi binafsi wa rais. Kwa jumla ni kama taifa linalazimishwa kuishi ndani ya itikadi za kijamaa kisa ndio tabia ya rais.

Ni kweli kuna miundo mbinu mingi anajenga ila deni la taifa nalo limepaa. Lakini nafasi ya urais ni zaidi ya miundombinu. Ni vyema angebaki kwenye uwaziri wa ujenzi na sio kuwa rais kwani mambo mengi pia anayaharibu hasa uchumi na demokrasia.
 

Tupe mwenye DNA unayetaka wewe, kwanini unataja udhaifu tu, hakuna mazuri anayo fanya? Au unachuki binafsi?tunachotaka Maendeleo, wewe tueleze kwa uchache unataka kiongozi wa aina gani wa kuongoza Tanzania ya sasa, kama ni wewe mwenyewe tuambie ni wewe mwenyewe.
 
Nimekuelewa sana mkuu! Watz ni wavivu mno, wao wanamtegemea selikali ije iwaambie njoo hapa ufanye hiki.
Hapana pamoja na ukweli kwamba serikali ina wajibu wa kutengeneza miondombinu kuwezesha wananchi wake kupata unafuu katika shughuli za uchumi, hii awamu ya tano imebomoa hatua zote wananchi wake walizokuwa wamepiga hasa katika sekta binafsi.
Nchi kwa sasa inanuka umasikini.
 
Nimekuelewa sana mkuu! Watz ni wavivu mno, wao wanamtegemea selikali ije iwaambie njoo hapa ufanye hiki.

Hujui usemalo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Hebu taja mahali kuna kiwanda kimefungwa kwa kukosa wafanyakazi. Watu wanataaluma zao na ujuzi mbalimbali lakini hakuna wateja wa kununua taaluma au kazi zao. Sasa unaposema watu hawataki kazi sijui unamaanisha nini. Mfano mtu ni seremala, ametengeneza furniture na hakuna wateja wa kuzinunua, utasema mtu huyo anasubiri serekali?

Hata hawa vijana mnaowakashifu kuwa wanashinda vijiweni unadhani wanapenda? Unataka waende wakashinde nje ya ofisi za wizara? Au mnataka wakae ndani tu mpaka siku wanapata kazi ndio watoke nje ili wasikae vijiweni? Ni ni nani ametoka ofisini au kaacha shughuli yake akaenda kushinda kijiweni? Acheni lugha za kejeli kisa mmeajiriwa.
 
mkuu kifuatacho sasa itakuwa ni kuhakikisha tunaweka mikakati kabla rais hajaingia ikulu awekewe mwongozo japo katiba ipo lakin kuna ambayo nadhani hayajawekwa kwenye katiba

Ukishaona kiongozi anakimbia mdahalo ujue hapo hamna kiongozi bali kuna mtawala. Tuko umemjua huyu rais umewahi kumuona akishiriki mdahalo wa aina yoyote? Kama mtu anakwepa mdahalo ambapo ndio unaweza kupima uwezo wa mtu na busara yake, hapo unatarajia kupata kiongozi mzuri?

Unashangaa mtu anataka kazi lakini hataki usaili (interview), bali anataka apite anahubiri tu. Mtu wa hivyo akiingia madarakani anatekeleza agenda zinazo mpendeza yeye tu. Ndio maana unasikia anaongea kwa jeuri kwamba hajaahidi katiba mpya, kana kwamba nchi ni yeye na sio mahitaji ya wananchi.
 
Thank God.
Naona akili zimeanza kuwarudia
 
comred kwanini uongelei mwaka mmoja kumaliza ngwe ya awamu ya kwanza umempitisha moja kwa moja mpaka 2026

Kama tume ya uchaguzi na vyombo vya dola vinajiona vina wajibu wa kumtangaza yeye mshindi, huyo jamaa atakosa jeuri ya kusema hivyo? Sasa hivi chini ya awamu hii box la kura ni upuuzi kama upuuzi mwingine, sasa hivi rais ndio anaamua nani atangazwe mshindi! Na vyombo vya dola vinajitokeza na viongozi wa ccm kushangilia ushindi wa hujuma.
 
Heshima kwako mkuu tindo..hii ndio hali halisi...unajua mtu kama huyu ni masikini wa roho na selfish sana...
 
Umeandika kwa hisia na majuto makuu,ila hayana msaada kwetu,pekee chenye msaada ni huko kwenye chama chenu mumueleze basi na atoke koz imetosha kwa owezo wa ubongo wake.Atuachie nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…