Rais, Makamu na Waziri Mkuu wameshiriki misa ya Krismasi katika Manisa gani? Ni upi ujumbe wao kwa Watanzania?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nimependa kuona salam za Christmas's za viongozi wa Kitaifa. Ningependa kusikia kauli zao kuhusu upungufu wa maadili, kuongezeka mauaji, kero za huduma ikiwemo upungufu wa umeme.

Lakini bado sijaweza kusikia salamu zao rasmi. Au awajashiriki misa ya Christmas's? Au watazungumza nasi jioni?

Merry Christmas kwenu nyote; tupendane na kuvumiliana
 
Kuna ushauri uliwahi kutolewa na mtumishi mstaafu mmoja kuwa mambo ya kidini yasichanganywe na siasa....Japokuwa wanasiasa wana dini zao. 🤔
 
Rais mwislamu, waziri mkuu mwislam kwanini unataka waende kanisani?
Wakitoa salama za xmas inatosha. Vice president yeye ni mkristo akishiriki kashiriki kama muumini
 
Vuta subra, soon utazisikia tuu !.
P
 
Maadili sio jambo linalopaswa kushughulikiwa na serikali hasa ngazi ya kitaifa. Maadili yanapaswa kuzungumzwa katika ngazi za dini, koo, makabila na kidogo serikali za vijiji.
 
Kama hujuwi endelea kutotaka kujuwa.....
Zama zimebadilika Mjomba kama bado hujashona kanzu Shona faster faster
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…