Nimeelewa ndugu mchangiaji!!Suala la Bunge kuonyeshwa live siyo mapenzi,hisani,kudra wala takwa la Rais.Suala la Bunge kuonyeshwa live ni haki yetu kikatiba.Haki huwa haiombwi kama unavyofanya bwana mleta uzi bali haki huchukuliwa kwa nguvu.Hatuna haja wala wajibu wa kumuomba Rais kuwa bunge liwe live bali tuna wajibu wa kuchukua haki hiyo kwa nguvu.Rais atake asitake suala la bunge kuwa live ni haki yetu wala siyo mapenzi yake.Umeelewa mleta mada?
Ni kweli bunge halina ladha wala mvuto hata chembe. Labda kwa wanaopenda kusikia vishindo kwenye madawati na ndiooooo!!!Japo litakosa ladha kwa kukosa wawakilishi wenye weledi mkubwa wa mambo ila watuletee tu tutafuatilia hivyo hivyo
Wawakilishi au Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM?Kwa kitendo cha Mama, namfananisha na marikia wa Sheba cha kuruhusu vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa kwani Marikia wa Sheba na yeye katika enzi zake kulitokea shida ya wanaume kuoa wake wangapi na sifa zipi lakini marikia alipoingia madarakani akapeta na kusema tuolewe tu bila mashariti hili taifa langu tuwe wengi. Mi nadhani hili kwa Mama liende sambamba na kufungulia bunge mubashara na lilushwe na TV zote za Tanzania kwa kadri inavyohitajika...