Mimi sitasombwa na upepo wa kimagharibi never,kwa kuwa najua ni illusion.Kalamu wewe ni wa kizazi kilichoibukia na kukulia kwenye awamu za Mwinyi,Mkapa na Kikwete.Kipindi hiki ndipo Wazungu walipotimiza adhma yao uvu ya kuingiza uchafu wao mwingi kwenye vichwa vya watu wetu,including you.Hata historia yetu wameifuta kwa makusudi hayo hayo,wakisaidiwa na vibaraka wao waliowapandikiza kwenye system yetu.Ipo haja, tena kwa makusudi kabisa, kubadili mitaala mashuleni,ili kujaribu ku-flush out mawazo na mentality zote za kimagharibi.
You are indoctrinated and mind controlled by the West Kalamu.I can infact add,you are also enslaved.Na utumwa huu ni mbaya sana, kwa kuwa hujui kwamba umtumwa,and so you cannot get out of it.Hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere talked about this kind of slavery you are you in.Alisema ni utumwa mbaya sana,kwa kuwa hujui kwamba umtumwa,and therefore nobody can get you out of it.
Yaani sasa ndio unajifunua zaidi kuliko wakati mwingine wowote kuhusu ujinga/giza nene sna ulilomo.
Wakati huu si wakati tena wa kuzungumzia "Magharibi wala Mashariki wala kwingine kokote, enzi hiyo ilishapita zamani sana na bahati yako mbaya wewe ukabaki nyuma, nyuma sana; mbali kabisa hata kabla ya enzi za ukoloni!
Kama umeenda shule, na umesoma kidogo hata kufikia ngazi ya digri ya kwanza, ni wazi kabisa elimu hiyo haikukusaidia kukuondoa ujinga, na kukuwezesha kufikiri na kuchambua mambo. Elimu ambayo Mwalimu Nyerere aliisisitiza; elimu ya kumkomboa mtu na sio elimu ya kukariri tu na kushinda mithani kama unavyoonyesha hapa.
Unapata elimu ya kukuweka huru, na siyo elimu ya kuendelea kukushikilia ubaki na mawazo ya kitumwa kama uliyonayo wewe.
Elimu iliyotuwezesha kuondokana na ukoloni na kutuwezesha sisi wenyewe kutambua na kujiamria ni nini kilicho cha manufaa kwetu.
Elimu inayotupa uwezo kufikiri na kuchambua sisi wenyewe mambo yetu kwa akili zetu na sio kubaki tunalialia juu ya watu wengine toka nje (Magharibi) kama ulivyo ganda wewe.
Elimu inayotuwezesha kujua ni nani rafiki na ni nani adui, na kuamua kukataa kunyanyaswa na yeyote.
Wewe bado umeganda kule kule kwa zamani ukihofia kila kitu kana kwamba huna utashi na uwezo wa kutegemea akili yako.
Tanzania, kama nchi zingine zote, tumepiga hatua sana tokea tupate uhuru wetu.
Tunao sasa hivi wasomi wengi na wazuri, karibu kila aina ya nyanja inayojulikana duniani; hata kama wengi wao hatuwatumii ipasavyo kwa sababu mbalimbali; na sababu mbovu kabisa ni kama huu msimamo wako mbovu kabisa wa kudhani tu kwamba kuna kundi la watu linatuwinda kila mara litumalize!
Tuna watu walio na sifa nzuri kabisa kwenye mambo ya kisayansi, ambayo wewe unaichukulia kana kwamba ni siraha wanayotumia hao wasiotutakia mema kuitumia na kutumaliza, hutaki kabisa kuelewa kwamba tuna wataalam wazuri hapa hapa kwetu wenye uwezo wa kutambua mtego kama upo. Wewe unabaki tu huko huko kwenye 'conspiracy' za hovyo kabisa, kwa kukosa kwako kuwa na elimu ya utambuzi/uchambuzi wa mambo.
Watu kama wewe ndio maadui wakuu ndani ya taifa hili, na kwa bahati mbaya aina yenu baadhi wamo hadi kwenye ngazi za juu kabisa serikalini na ndio wanaofanya maamuzi muhimu.
Tanzania inapata hasara kubwa sana, hasa wakati huu, kwa sababu hata vijana wetu wanaotakiwa kuandaliwa ili wapiganie hadhi ya taifa hili hawapewi fursa hiyo. Tunaachwa nyuma na wenzetu. Itatuchukua muda mrefu sana kuondoka huku nyuma tunakobaki na kufikia ngazi za wenzetu tukishaondokana na mawazo ya watu mgando kama wewe.
Ni shida sana kueleza mambo haya kwa mtu mwenye fikra mbovu kama wewe ili kuweza kukuondoa gizani.
Lakini, kama unataka kubaki huko, baki peke yako, usishawishi na wengine kukubali ujinga wako.