Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Salama.
Huwa viongozi na watumishi wa serikali wakijinasibu kuwa wanalipa kodi, lakini kilogic watu hawa hawalipi kodi hata kidogo, badala yake ni watumia kodi.
Wataalamu waliochunguza swala hili walikuja na mfano ufuatao. Ikitokea nchi ikakusanya kodi sifuri, basi kuanzia Rais, Waziri, Mbunge, na watumishi wa Serikali mishahara yao itakuwa 0, na hiyo kodi wanayodai kulipa kutoka kwenye mshahara itakuwa sifuri.
Watu hawa wanasubiria kodi iwape mshahara ndiyo 'eti' walipe kodi! Hawa ni watumia kodi na si walipa kodi. Mtu akisema mshahara wangu ni 1,000,000 halafu nalipa kodi 100,000, ni kuwa huyu halipi kodi yoyote na mshahara wake ni 900,000. Haongezi pesa yoyote kwenye kodi ya nchi. Tofauti na mfanyakazi wa sekta binafsi ambaye anazalisha bidhaa au huduma, anauza na kulipa kodi. Huyu ndiye anachangia kwenye kodi/utajiri wa nchi.
Sasa basi, hawa wala kodi siku zote watataka kodi iongezeke ili wapate kikubwa zaidi cha kutafuna. Na ubaya ni kuwa wamepewa mamlaka ya kuamua nani alipe kodi kiasi gani, matokeo yake kila siku kodi na tozo vitaongezeka.
Inabidi hili suala liangaliwe vizuri. Kodi kwenye mazao, biashara, madini nk isibadilishwe bila kushirikisha wadau wa sekta hizo. Kuna vyama vya wafanyabiashara, wakulima, wafugaji nk, wanatakiwa wote kuhusishwa na michakato ya kodi. Si sawa kwa anayefaidika na kodi kupangia wengine kodi ya kulipa.