Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
- Thread starter
- #21
Soma vizuri hapo. Levied by goverment on worker's income. Hiyo goverment inayotoza kodi ni ipi? Ndiyo wabunge, Rais, mawaziri na wafanyakazi wa serikali. So, serikali(Rais, mawaziri, wabunge na watumishi wa serikali,) ndiyo inayotoza wengine kodi. Wao wanaitumia kwa kufanya shughuli, kutoa huduma na kulipana mishahara. Kuhusu kodi wao hawalipi hata mia.Hebu tuangalie Tafsiri hizi juu ya kodi kisha tuendelee kujadiliana: Tafsiri ya kodi kwa kiswahili (kwa mujibu wa wikipedia) "Kodi (ushuru) ni malipo ya lazima ya pesa au aina nyingine ya malipo yanayotozwa na taasisi ya serikali kwa mujibu wa sheria kutoka kwa mlipakodi (mtu binafsi au chombo kingine cha kisheria) ili kufadhili matumizi mbalimbali ya umma"
Na ile ya Kiingereza "a compulsory contribution to state revenue, levied by the government on workers' income and business profits, or added to the cost of some goods, services, and transactions"
Ukiangalia hiyo Tafsiri ya kiingereza hapo nilipokoleza wino inaweka wazi kuwa "on workers'income" kwa maana hiyo hata wafanyakazi wa umma wanalipa kodi. Ile tafsiri ya kiswahili japo haijaweka wazi lakini hapo nilipokoleza wino pia " chombo kingine cha kisheria" inaweza kuwa na maana kutoka taasisi zinazotambuliwa rasmi na serikali, kwa maana hiyo kodi pia hutozwa kwa wafanyakazi wa taasisi hizi.
Na sina hakika sana, lakini wafanyakazi wa serikali ni civil servants, sidhani kama ni workers wale wazalishaji.