Rais, mchukue Robert Heriel wa JamiiForums awe mwandishi wako wa hotuba 2025

Gabeji

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
1,530
Reaction score
1,903
Rais, nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pole na Kazi nzito ya kuliongoza Taifa letu pendwa hili la Tanzania. Mambo ni mengi sana ya kuendelea kusemezana na wewe kupitia jukwaa letu pendwa la Jamiiforums, muda ni kidogo sana kama kawaida yangu ya kuendelea kutoa ushauri juu ya mambo ya kiongozi kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa letu pendwa. Mh Rais.

Rais najua una macho mengi yamo humu ndani yanakusaidia kuangalia kinachoendelea ndani ya utawala wako.

Rais ikikupendeza nakuomba umteue huyu ROBERT HERIEL wa humu Jamiiforums akusaidie kukuandikia hotuba za kitaifa.

Rais nimeamua kuandika hili kwa sababu nimeona team Yako inayokuandikia hotuba haipo vizuri sana kiasi kwamba kuweza kuwavuta watu waache Kazi zao, na kuja kukusikiliza wewe, nimesikiliza hotuba nyingi sana zako, hazina mvuto, sana hazigusi hisia za makundi mbalilmbali, kama watu chini, masikini, wamachinga, wafanyakazi, wafanya biashara n.k

Rais ningetamani sana kuona watu wanavutiwa na hotuba zako zaidi kwa kugusa hisia za wananchi mbalimbali ndani ya Taifa letu pendwa la Tanzania.
Rais kwanini umteuwe huyu ROBERT HERIEL?
1. Ni mwandishi mzuri sana wa mambo ya kijamiii, kisiasa, kiuchumi, na kn, ameandika makala mbalimbali zinahusu mambo mbalilmbali.
2. Huyu mtu ni gifted namna ya kutumia lugha inaweza kuibua hisia za watu wa rika na makundi mbalilmbali.
3. Mtu huyu anajua mambo mengi yanahusu jamii, changamoto na anatoa soluhisho zake.
4. Amewai pewa tunzo na jukwaa hili la jamii forum, ya kuwa miongoni mwa wandishi bora zaidi ya expects 100000 wa humu ndani .naomba mods mniwekee huo uzi unaonesha huyo ROBERT HERIEL akichukua tunzo.
5. Anawezo mkubwa wa kufanya uchambuzi wa maswala mbalilmbali ya kijamiii, kiusalama,kisiasa,kiuchumi nk.
6. Mtu huyu Mh.rais hafungamani na CHAMA chochote hii ni baada ya kuona makala zake alizoandika. Nisikuchoshe sana mh.raisi

Bila shaka hata wajumbe wa humu jamii forum wanakubaliana na mimi kuwa huyu mtu ni special gifted in writing skills. Nakuomba kwa unyenyekevu mkubwa mh rais fanya nae Kazi huyo mtumishi wa Mungu , sina wasifa wake ( cv) ila najua mods watakuwa wanajua cv yake.

Namba yake ya simu nitaiweka hapa chini hii namba huwa anaweka karibia kila makala yake, jamani mm sio Robert msiseme najipigia debe ni kwa ajili ya masilai mapana ya taifa letu pendwa Tanzania na kumsaidia mama.
"Nakuomba mods" niwekee badhi ya links za nyuzi zake za huyu ROBERT HERIEL I'li mh. Rais aone kwa macho yake mwenyewe
Pia naomba mods uzi huu ukae angalau siku tatu au zaidi ikiwapendeza utawala wenu I'li mh raisi aupate. Hii ni kwa ajili ya kuwamotivate wanajamiii forum,Lakini pia cv yake ni muhimu sana muweke hii ni kwa ajili ya masilai mapana ya taifa na wanajamiii forum wote nawasilisha .
By mwinjilist Gabeji.
 
Huyo mtibeli havumilii uongo, unafki na dhulma. Hiyo kazi haimfai hata kidogo, maana itamfanya adanganyez adhulumu na kuona haki ikipindishwa na asiwe na la kufanya.

Atamchana makavu Mh, mwisho tumkute kwenye viroba ufukweni au achapwe risasi ya kisogo.
 
kwa maslahi mapana ya familia hii pana na muhimu sana ya JF, nadhani angebaki humu humu kwenye platform hii ili hatimae aendelee kuibua hisia zenu vizuri zaid kama ambavyo point yako ya pili inavyosema. Akiondoka nani atachochea hisia tena humu jukwaani?

au mbadala wake atakua nani kwa mfanao, na itapendeza zaidi
 
Mbona unaandika kama mwenyewe uliyempigia debe,ofcourse ndio wewe bhana.

Maana jamaa nyuzi zake huwa ndefu sana na wewe nyuzi yako ni ndefu wakati ilitakiwa iwe na maelezo machache sana kwa sababu ujumbe upo very clear.

Lakini pia kitendo cha kutumia maandishi mengi kumpigia debe jamaa ni ishara kuu kwamba wewe ndio yeye.

Ni vyema ukasubiri watu wakusemee kuliko kutafuta mbinu za kujisemea mwenyewe,huwenda bado haujafikia huo uwezo ambao unajipigia debe.
 
Wapo wengi wanaoibua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…