05 February 2024
Dakar, Senegal
KELELE ZA MARIDHIANO NA UMOJA WA KITAIFA ZASABABISHA RAIS MACKY SALL, KUJIVIKA CHEO CHA MWOKOZI WA TAIFA HIVYO KUVUNJA AHADI YA KUSTAAFU
Picha: rais Macky Sall wa Senegal
"Ninaondoka ofisini nikiwa na hali ya utulivu baada ya miaka 12 katika uongozi wa nchi. Ilikuwa safari na tukio la kipekee la kisiasa," Macky Sall aliiambia gazeti tajwa Le Monde la Ufaransa jioni moja katika siku za mwisho za Desemba 2023. Wakati huo, rais wa Senegal alikuwa akimalizia kwa utulivu hotuba yake ya mwisho kabla ya kuachia ngazi.
Mnamo Desemba 31, kama ilivyokubaliwa, kuaga kulikuwa kwa muda mrefu na kwa sherehe.
Rais alipojitokeza tena kwenye runinga Jumamosi, Februari 3, 2024 akiwa na sura nzito, nchi ilipigwa na butwaa. Baada ya kurejelea shutuma za ufisadi zilizotolewa katika Baraza la Katiba, alitangaza kwamba alikuwa amebatilisha agizo la kuitisha uchaguzi wa rais wa Februari 25, 2024.
Bila hata kutamka neno "kuahirisha," alizusha tetemeko la ardhi la kisiasa. Haijawahi kutokea tangu mwaka 1963 uchaguzi wa rais umeahirishwa nchini Senegal.
Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya kuanza kwa kampeni jumatatu 5 February 2024, taifa la Senegal lilijikuta likitumbukia katika sintofahamu. Uvumi wa kuahirishwa kwa uchaguzi ulikuwa umetanda kwa miezi kadhaa, na sasa uvumi umebainika kuwa ulikuwa ukweli.
Baada ya ghasia za Machi 2021 na Juni 2023, kufuatia kukutwa na hatia kwa mpinzani mkuu wa rais Sall, Bw. Ousmane Sonko, baadhi ya viongozi wa kidini, wapinzani na hata viongozi katika muungano wa Sall walikuwa wametetea wazo hilo la kuahirishwa uchaguzi.
"Hoja yao ilikuwa kwamba nchi ilihitaji kusuluhishwa na maridhiano kabla ya uchaguzi kuandaliwa. Vinginevyo, kulikuwa na hatari ya machafuko.
Hii ilizidi kuwa mbaya kufuatia uamuzi wa rais kutowania muhula wa tatu," alisema Moussa Diaw, ambaye mhadhiri wa utafiti katika Chuo Kikuu cha Gaston-Berger huko Saint-Louis
Source : Gazeti : Le Monde