Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassani nakusalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania..............
Mh Rais Mimi ni raia wa Tanzania,hivi Sasa ni SAA kumi na dakika 25 Natumah wewe utakuwa umepumzika kutokana na kazi nzito hasa za kipindi hiki ulipo ziarani.
Mh Rais Mimi raia wako MWANANCHI mwema kabisa nimeumizwa na UTAWALA wa AWAMU ya SITA mpaka ninajiuliza nimekosa Nini kwako au kwa Mungu muumba?(nimeona sio busara kujizuru Mimi nikafa pasipo kusema,nimeona Bora niseme ili kama utasikia kupitia hapa utauponya moyo wangu na ukishindwa basi hata yatakayojili nawe ubebeshwe sehemu ya dhambi zangu ukajibu siku ya kihama.)
Mh Rais nisikikuchoche,
Ukatili NILIO FANYIWA.
1. MAUAJI YA BINTI YANGU MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO SHULE YA SECONDARI LINDI GERLS KIDATO CHA TANO PCB.(NAOGOPA KUMTAJA JINA MAANA KILA NIKIANDIKA JINA LAKE ANANIJIA UBONGONI).
Mh Rais kutokana na mlango wa ikulu yako kufungwa kwa WANANCHI walala hoi nilishindwa kufikisha taarifa hizi ikuluni kwako badala yake nilitumia jukwaa ili la jamii forum KUANDIKA yaliyojili mpaka mwanangu akauwa
Nilielezea jinsi mwanangu alivyo amia shuleni hapo ndani ya mwezi Mmoja TU mwezi wa pili nilipigiwa simu naitwa nikamuuguze mwanangu anaumwa nikaanza safari SAA SITA mchana kutoka Mbagara kwenda Lindi Nilifika Lindi SAA mbili za usiku nikakuota mwanangu akiwa ameisha Oshwa, valishwa pakwa lipustik, valishwa nguo mpya, wekwa kwenye Jeneza, TAYARI kuletwa DSM Mbagara kwa mazishi.
Mh Rais Mimi kama MZAZI nilihoji kwa Nini nimeitwa nikauguze nafika nakuta mahiti kaisha andaliwa na mkuu wako wa WILAYA ya Lindi,mkurugenzi wa halimashauri, PADRI kanisa katoliki, ocd Lindi na mkuu wa shule ya secondari Lindi?
Nilijiuliza waliniita Mimi MZAZi nikakubali kwenda kama hawakumuua mwanangu walikuwa na haraka Gani ya kumvua nguo mwanangu kumwosha pasipo ridhaa yangu MZAZi?haraka ilikuwa ya Nini?
Niliwauliza cheti Cha kifo Cha mwanangu kiko wapi au cheti Cha matibabu wakajibu MGONJWA alikuwa akitibiwa na Dawa za mseto kwa mantiki hiyo hawana cheti?
Nikauliza mwanangu aliumwa Nini?nikajibiwa ni marelia na u.t.i je Mh Rais u.t.i na marelia utibiwa na mseto?
Mh Rais naandika haya huku nalia naomba nifike ikulu yako nikuelezee jinsi watumishi wa serikali yako walivyo usika kumuua mwanangu,
Mh Rais Nina hakika taarifa hii unayo mezani kwako maana Moja ya watu wangu walinijulisha ilikufikia na maelekezo yako/yalimtaka RPC Lindi afukue mwili wa mwanangu ufanyiwe UCHUNGUZI,ili halikufanyika badala yake RPC Lindi kwa KUSHIRIKIANA na ndugu Mmoja kutoka jeshi la polisi kitengo Cha malalamiko Mr Wankyo walifanya wanayoyajua na KUANDIKA ripoti yakuwa kifo kilikuwa Cha kawaida taarifa ilifika mezani kwako Mh Rais kwa wakati UCHUNGUZI wa polisi umetumia MIEZI 7 baada ya kifo Cha mwanangu.
Ili nalo limepita Mh Rais kilio changu ni KIKUBWA.
.