Rais mpya wa Kenya, William Ruto anaonyesha dalili zote za kutokuwa kiongozi mzuri tangu mwanzo

Rais mpya wa Kenya, William Ruto anaonyesha dalili zote za kutokuwa kiongozi mzuri tangu mwanzo

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Wakenya niliwashauri mumchague Ruto ila ningependa tena kusema hatakuwa kiongozi mzuri kama nilivyokuwa namfikiria. Poleni.

Ameanza kuwanunua wapinzani wake jambo ambalo ni baya sana katika ustawi wa demokrasia, ili nchi yenu iendelee kuwa demokrasia imara mnahitaji watu wenye misimamo na watakaotoa upinzani imara serikali, anachokifanya Ruto ni kuuvunja upinzani uti wa mgongo.

Anaonekana ni mgawanya watu zaidi kuliko kuwa muunganishaji. Kiongozi mzuri anapaswa kuwa mtu muunganishaji. Nimemuona akitoa hotuba huku akimfanyia kebehi Kenyatta, hakuna ulazima wa hilo jambo tena kwa sasa, ni vyema angekaa kimya tu kuliko kumzungumzia kwa mzaha.

Anaonekana muda mwingi sana akiitumia kwenye mambo ya kidini, kwenye makongamano, akihubiri, akiimba, akifanyiwa maombi n.k. Mojawapo ya dalili ya viongozi wabovu na "incompetent" ni kujificha chini ya kivuli cha mambo ya kidini na mara nyingi wakimtaja sana Mungu ili kujionyesha ni watu wema. Bahati mbaya sana hii ni propaganda ambayo hununuliwa na raia wengi wenye akili ndogo.
 
Ya Kenya tuwaachie wenyewe
Chukua hii
20220907_155744.jpg
 
Unafahamu maana ya kuwa na jirani anayejielewa?

Unajua maisha ya Tundu Lissu yaliponea chupuchupu Nairobi na Lema alienda uhamishoni Canada kupitia Nairobi ? Hao walikuwa Wakenya?
Huwezi chagua jirani, unajifunza kuishi na jirani. Unataka umchagulie jirani baba wa familia? Haitatokea
 
Back
Top Bottom