Rais mpya wa Kenya, William Ruto anaonyesha dalili zote za kutokuwa kiongozi mzuri tangu mwanzo

Rais mpya wa Kenya, William Ruto anaonyesha dalili zote za kutokuwa kiongozi mzuri tangu mwanzo

Incompetent leader huwa na tabia za kujifichia kwenye dini Ili kuwahadaa watu
 
Wakenya niliwashauri mumchague Ruto ila ningependa tena kusema hatakuwa kiongozi mzuri kama nilivyokuwa namfikiria. Poleni.

Ameanza kuwanunua wapinzani wake jambo ambalo ni baya sana katika ustawi wa demokrasia, ili nchi yenu iendelee kuwa demokrasia imara mnahitaji watu wenye misimamo na watakaotoa upinzani imara serikali, anachokifanya Ruto ni kuuvunja upinzani uti wa mgongo.

Anaonekana ni mgawanya watu zaidi kuliko kuwa muunganishaji. Kiongozi mzuri anapaswa kuwa mtu muunganishaji. Nimemuona akitoa hotuba huku akimfanyia kebehi Kenyatta, hakuna ulazima wa hilo jambo tena kwa sasa, ni vyema angekaa kimya tu kuliko kumzungumzia kwa mzaha.

Anaonekana muda mwingi sana akiitumia kwenye mambo ya kidini, kwenye makongamano, akihubiri, akiimba, akifanyiwa maombi n.k. Mojawapo ya dalili ya viongozi wabovu na "incompetent" ni kujificha chini ya kivuli cha mambo ya kidini na mara nyingi wakimtaja sana Mungu ili kujionyesha ni watu wema. Bahati mbaya sana hii ni propaganda ambayo hununuliwa na raia wengi wenye akili ndogo.
Ndio vizuri avuruge Kunyaland kama Mwendazake alivyofanya Ili na sisi tuwakaribie kwenye uchumi
 
Hawezi kuivuruga Kenya kama alivyofyanya mwendazake, Katiba na mifumo ya nchi hiyo haimpi hiyo fursa.
Ndio vizuri avuruge Kunyaland kama Mwendazake alivyofanya Ili na sisi tuwakaribie kwenye uchumi
 
Hizi mbwembwe za kijinga hazikuwahi msaidia Mwendazake 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20221111-210723.png
    Screenshot_20221111-210723.png
    157.8 KB · Views: 8
Back
Top Bottom