benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano amesema utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, ni matokeo ya juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuthamini, kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili nchini.
Alitoa kauli hiyo akiwa mkoani Dares Salaam alipokuwa mgeni katika hafla ya utoaii tuzo hiyo kwa mwaka 2023 iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kuratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa washiriki kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika nyanja za ushairi na riwaya.
Rais Chissano aliwataka Watanzania kumsaidia Rais Samia na kumpa ushirikiano zaidi kuendeleza Kiswahili na mambo mbalimbali ya kitaifa kwa ujumla.
"Msaidieni Rais Samia, anafanya kazi hii kwa makini sana..." alisema Chissano na kuongeza: "Utoaji wa tuzo hi ni kuendeleza amali muhimu ya Kiswahili nchini Tanzania na katika Afrika kwa jumla."
Kwa mujibu wa Chissano, Kiswahili nyumbani kwake ni Tanzania hivyo Watanzania hawana budi kukilinda na kukitumia kwa tija kama lugha adhimu.
"Kiswahili ni lugha yetu Afrika, tukilinde kukikuza na kukipa heshima kwa kukitumia katika elimu, siasa na masuala mengine ya kijamii," alisema Rais mstaafu huyo.
Aliwapongeza pia Watanzania kwa kuenzi mchango wa Nyerere katika kukuza Kiswahili, na pia kupongeza uhusiano wa kihistoria baina ya Tanzania, Msumbiji na nchi nyingine uliowezesha kupatikana kwa ukombozi wa nchi za Afrika.