Rais Mstaafu Dkt. Kikwete akutana na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete akutana na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania

Mimi nakubaliana na wewe, Ila aina ya misaada ambayo israel inaomba US ni tofauti na sisi.
Hata hivyo kupenda kusaidiwa saidiawa sio sifa, naamini hata wewe hapo unapoishi hupendi kabisa kwenda kuomba msaada kwa jirani tajiri
Umenena jambo la busara sana. Hakuna kitu kibaya kama kuomba au kujiona huwezi kufanya maendeleo yako bila kuomba. Iwe ni nchi au mtu binafsi. Mbona kuna nchi ndogo ambazo hazina raslimali kama sisi na population ya watu around milioni 5 lakini hazilii njaa kama sisi? Hili la kusingizia kila nchi inaomba ni kukwepa wajibu wetu. Mimi sikumkubali kabisa Magufuli lakini kwenye kujiamini kuwa tunaweza kufanya sisi wenyewe bila kutegemea misaada mingi nitamkumbuka sana. Tatizo nilaloanza kuliona kwa mama Samia ni kuamini kuwa wawekezaji ndiyo watainyanyua nchi yetu na tunatakiwa tuwapigie magoti. Hili linatia shaka kubwa na tuombe Mungu tusirudi hali iwe kama kipindi cha Kikwete ambacho tulikuwa tunakumbatia hata wauza unga kwa kuona ni kama wawekezaji.
 
Wadau wa JF


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Donald Wright
Balozi Wright amempongeza Dkt Kikwete kwa mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Marekani

Balozi huyo pia amempongeza Dkt Kikwete kwa jitihada kubwa alizozifanya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kupitia mradi wa PEPFA

My best and favorite President ever folowed by Madam Prezida...!

(Sinaga uNaFiki)
 
Hakuongelea legacy hapo. Hili suala linamsumbua mpaka msibani chato.
 
Madhara ya kuchungulia mama yako akiwa analiwa na kubadilisha pedi lazima akili izame
Nlihisi hili ndo tatizo mlilo nalo kwenu. Umethibitisha kama ambavyo ulishawahi andika kuwa unaomba msaada upewe ushauri unahisi mmerogwa.😁
 
It’s true kuna makosa. Kikwete alikuwa na makosa yake na mwenda zake pia tunachokataa ni kutorudia makosa .mama aachwe atakapokosea tutamsema tena kwa sauti kubwaa Nan uzuri ni ana sikiliza sauti zetu .tunahitaji kujiamini na kujisimamia kama nchi .kati ya mambo mazuri mwenda zake tutamkumbuka ni kujiamini . We do not need to bow down to anyone for expense of our natural resources .kuna wajinga wana argue ati wameleta misaada mingi poor people wasijue ndo madhara tuliyoyaona awamu ya Nne ya mkwere. Nchi zetu hizi ukishaona vi meeting meeting mshenzi hivi ujue ndo unaingia 18 za beberu

Umesema kitu kimoja cha msingi ambacho Rais Samia akiendeleze toka kwa mwendazake nacho ni "KUJIAMINI na KUTHUBUTU KUFANYA MAAMUZI MAGUMU". Hizo ndio zilikuwa HALLMARKS za mwendazake na atakumbukwa kwa hayo!!

Pia ikumbukwe kuwa " kufanya kosa si kosa ,kosa kurudia kosa!"
 
Ila sijawahi kuwaona watu wanafiki kama chadema walimwita Kikwete dhaifu leo wanamsifia yupo vizuri
 
mahitaji ya nchi zinazoendelea ni mengi sana!
hitaji kubwa ni elimu na wala sio shule kama wengi wanavyofikiri bali ni kwaliopata elimu kwa njia ya shule kufikisha ujumbe kwa watanzania ili wajue hitaji lao ili wanapoenda kwenye uchaguzi toka mwanzo wajue kazi wanatoa wao na job discription ni hii.
kwa bahati mbay hata tunaotegemea watusaidie kwa ulimu tuliyowapa wamekuwa wa kwanza kulalamika na hasa line isipopita kwao huku wakiwa wabinafsi kwa jamii inayowategemea.
ifike wakati tukubali kila kiongozi ipo sehemu yake aliyofanya kwa uaminifu kwa kadri ya uwezo wake na timu yake aliyokuwa nayo. sidhani kama ni staha sana kutukana ili uonekane unajenga hoja yenye mashiko na wengi ni vijana ambao kwa bahati mbaya wengi wao wazazi hawakuwalea katika maadili na hasa kusimama wenyewe.
wengi wanaamini mapungufu yao yanasababishwa na fulani kitu ambacho kinaweza kuwa sio kweli.
ni swala lililowazi wasomi wameongezeka na uwezo wa serikali kuwahudumia wananchi ni mdogo kwa wingi wa mahitaji lakini pia hajira za moja kwa moja toka serikalini pia zimepungua kwa hiyo nini kifanyike inawezekana ikawa kutengeneza mfumo unaoweza kuwa rafiki kwa taifa kuwa na mafanikio na ndipo hapa tunapohitaji wasomi watusaidie na sio wanasiasa.
kwa bahati mbaya tumewaangalia wnasiasa zaidi katika mafanikio yetu na kusahau wataalamu ambao wengi wao hawajawa tayari kufanya kazi bure kwa manufaa ya nchi.
haijalishi tumepotea kiasi gani hebu tukubali tutoke huko malalamiko na mihemko haitatusaidia kitu zaidi ya kutuongezea uchungu na maumivu yasiyo na tija.
ifike wakati tuanze kufikiria tunamchango gani katika jamii kwa kipato nilichonacho,shule niliyonayo na kwa madaraka niliyonayo na tukiyachanganya yote tunaweza kugeuka na kila mtu akasema na kuwaza kaifanyia nini Tanzania.
Isaya 43:18-19
Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
 
Wanadhani ndiye aliyesababisha kifo cha mkemia, wasijue wao ndiyo walisababisha kwa kumpamba kwa mapambio hata pale alipokuwa anakosea. Kuna mtu aliye kwenye system na cheo kizuri tu nilizungumza naye akaniambia ile inner circle ya mkemia sasa hivi ndiyo inaona makosa waliyokuwa wanafanya na kuanza kujilaumu. BTW Kikwete naye utawala wake ulikuwa mbovu sana hivyo tuombe Mungu tuzirudi tena kule.
Nina mashaka makubwa na tunakoelekea. Ngoja tumalize hizi siku 100 za mwanzo, pengine mwanga tutauona.
 
Wadau wa JF


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Donald Wright
Balozi Wright amempongeza Dkt Kikwete kwa mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Marekani

Balozi huyo pia amempongeza Dkt Kikwete kwa jitihada kubwa alizozifanya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kupitia mradi wa PEPFA

Usijue kuwa amekwenda Ubalozi wa US kuhemea chanjo, si tumeambiwa chanjo (brands) za Pfizer-BioNTech/AstraZeneca zimeletwa kwa ajili ya mabalozi na wafanyakazi kwenye balozi zao hapa nchini? Si mnajua 'mtoto wa mjini' huwa hana aibu!
 
Hawa makamanda uchwara hawaeleweki. Walimuita Kikwete rais dhaifu na Vasco da Gama hivi sasa eti wanaanza kumsifia, ha ha ha. CCM itawatawaleni miaka nenda rudi kwa dizaini hii nyie uchwara wa ufipa.
Acha watawale tu, bora nitawaliwe na upuuzi wa CCM kuliko ujinga wa hao majamaa.
 
Hao “mabeberu” huwa hawatulazimishi kuwagawia bure rasilimali zetu. Ni viongozi wa serikali ya CCM hupenda kuandaa na kusaini mikataba ya kifisadi na “mabeberu”, period. “Beberu” akidai mkataba safi usio na ufisadi ananyimwa fursa na kutangaziwa kila aina ya mipasho.
Wapinzani wakidai mikataba ijadiliwe bungeni wanashambuliwa kwamba hizo ni “siri za nchi”. Kufichua ufisadi ni usaliti kwa taifa; eti unalivua nguo taifa! Ndio sababu hadi leo CHADEMA inatambulika na serikali na manazi wake kama “public enemy number one”. Mwendazake alitaka kuiangamiza na viongozi wake literally.
Huu ujinga wa kudai “mabeberu” wanataka kutuibia ni aibu kubwa sana ya awamu ya 5. Hata corona: eti nayo ni njama za mabeberu kutaka kutuibia rasilimali zetu; wtf! [emoji35] Hakuna mkoloni anayemshikia bunduki mtu siku hizi. Mnajipeleka wenyewe na propoza zenu za kiwizi halafu mnadai mmebakwa! Mbona nchi makini zinasaini mikataba ya maana sana?
[emoji106][emoji106][emoji120]
 
Wadau wa JF


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Donald Wright
Balozi Wright amempongeza Dkt Kikwete kwa mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Marekani

Balozi huyo pia amempongeza Dkt Kikwete kwa jitihada kubwa alizozifanya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi kupitia mradi wa PEPFA

Mhhhh hyu mzeee hata aibu hana
 
Back
Top Bottom