Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Asante.
Jakaya ana utata fulani ambao sio mzuri..hili suala litaleta utata soon.
Ila umri nao ni shida....
 
Chuo cha ushirika moshi, kcmc, mwenge stefano moshi havina zaidi ya ekari 10 kila kimoja na maisha yanaendelea. Mwambieni JK aache mbwembwe
 
Bwana JK anang'aka siku hizi bwana kwani yupo na dadake Sammy.
 
Naunga mkono hatua ya JK. Na chuo kikihamishwa utakuwa ni uhujumu. Hapo chuo cha kilimo wana kama ekari zaidi ya 3,000 mjini. Kwa nini wasiwagawie wenzao.

Nasikia waliomba Tanganyika packers, wana maelfu ya ekari, kwanini wasiwape UD? Hayo ni maeneo ya wizara ya kilimo, kama waziri wa kilimo na mifugo anagoma kutoa eneo basi aambiwe bosi wake.
 
Naunga Mkono Kikwete Kaona Mbali

Kweli kaona mbali na pia ameona wazungu walivyokuwa wanachukuwa maeneo makubwa hata kama kulikuwa na watu wachache sana

Kwani watu wanaongezeka na ni bora kuwa na sehemu kubwa kuliko baadae kuhangaika kutafuta maeneo mengine

Hebu angalia Vyuo vikuu na ukubwa wake
 
Umeshawahi kufanya utafiti wa ukubwa wa maeneo ya vyuo kama UDSM na UDOM?

Na ujifunze vitu hivi.vikijengwa vinaweza kudumu miaka 100 na kuendelea.
 
Kwa nini anataka hicho chuo kihamishiwe katika mikoa mengine badala ya kubaki Dar tu?
 
Unafuu huo ni upi? Mbona kwenye nchi nyingine zenye vyuo bora vya umma hawavipanui kwa kuanzisha matawai mengi ndani ya nchi hiyo moja?
Hata nje ishu ya kutanua ipo mkuu. Mfano University of Calfornia, ina matawi kibao.
 
Ina matawi kibao ndani ya California ?
Huoni ingekuwa na maana zaidi kama Mbeya nayo ingekuwa na chuo kikuu kubwa mithili ya UDSM kiitwe University of Mbeya?!
Hata nje ishu ya kutanua ipo mkuu. Mfano University of Calfornia, ina matawi kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…