..sina uhakika kama Harvard wana matawi nje jimbo waliloko ambalo ni jimbo la Massachusetts.
..lakini viko vyuo vikuu vingine vikubwa duniani ambavyo vimekuwa na matawi nje ya mahali vilipoanzishwa.
..nitakurudisha ktk historia ya vyuo vikuu ktk ukanda wetu wa AFRIKA MASHARIKI.
..chuo kikuu cha Makerere kilianza kama tawi la London University. Wahitimu toka Tz, Ug, na Kya, wa miaka ya 50 walitunukiwa shahada za London University ingawa walisomea Kampala.
..Pia chuo kikuu cha Dar Es Salaam nadhani shahada za kwanza za sheria zilikuwa za London University.
..Baadae Dar Es Salaam kikawa sehemu ya University of East Africa, kabla ya kila nchi kuamua kuwa na chuo kikuu chake.
..Tuje kwenye chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Muhimbili ilikuwa kitivo cha Tiba, kabla haijaamuliwa iwe chuo kikuu kinachojitegemea.
..Twende IFM hapa Dsm. IFM kunatolewa shahada ya MBA toka chuo kikuu cha Strathclyde kilichoko Scotland.
..Kwa maoni yangu, sio vibaya chuo kikuu chochote kuwa na matawi ktk maeneo tofauti na pale kilipoanzishwa.