Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Ina matawi kibao ndani ya California ?
Huoni ingekuwa na maana zaidi kama Mbeya nayo ingekuwa na chuo kikuu kubwa mithili ya UDSM kiitwe University of Mbeya?!
Mkuu Ardhi University ilikuwa kampasi ya UDSM na MUHIMBILI pia ilikuwa kampasi ya UDSM sasa hivi Ni vyuo vikuu vinavyojitegeme, kwa hiyo hata hilo tawi la Mbeya siku moja linaweza kuwa kama unavyowaza. Hoja aliyoitoa Rais mstaafu ina mashiko pia hata kwa wazo lako hapo baadae.
 
Hivi eneo la UD main campus ni ekari ngapi? Na hakuna muda kweli walilikata kata kuliuza kwa majirani na wavamizi?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Najiuliza kwa nini wasijenge chuo kikuu kingine kijitegemee kiitwe Mbeya University. Kaka wanataka kukifanya Udsm kuwa chuo cha mikoa yote basi wabadili jina waite Tanzania University ili wajenge campus kila mkoa kuliko jina la mkoa mmoja kuingia mkoa mwingine.
 
Huwa nashindwa kuwalewa kabisa watanzania ambapo wanajiribu kuleta siasa kwenye jambo la msingi kama elimu. Huwezi kukipa chuo cha UDSM heka 50 tu , huku ukitambua kwamba makazi yanatanuka na wanafunzi huendelea kudahiliwa kila siku. Kuna siku hizo heka 50 zitakuwa ndogo na utalazimika kutanua tena, hivyo ni heri wapewe 500 hadi 1000.

Kubwa zaidi Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinahitajika sana Mbeya kwasababu wanatoa shahada za udakatari wa binadamu, hivyo ni lazima wanafunzi wakae jirani na hospitali kubwa kama ile ya Rufaa, kwasababu ya mafunzo. Lakini ikumbukwe kwamba hospitali ya rufaa mbeya ina idara kubwa za tafiti ya magonjwa ambayo ni muhimu sana kwa wanafunzi wanaosoma udaktari.

Hakuna hasara yoyote tunayoipata katika hili, watanzania hebu tuacheni siasa...
 
JK kwa hili kaongea kiume na kaonesha uongozi

500 Acres ni sawa na 2,000,000 SQM. (2kmx2km) eneo hili kwa Mkoa wa Mbeya wanaweza kupata.

Kwa University kupewa 50 acres ambazo ni 200,000sqm (sawa na 400mx500m) ni eneo dogo sana kwa chuo kikuu.
 
wapeleke tu icho chuo kwa wajomba zangu upande wa mama, pale Iringa (academic town). kule kuna maeleo mengi sana watapewa hata 2000
 
Ardhi University ilianzishwa mahususi kwa ajili ya kozi za kuendeleza ardhi na mipango maji. Muhimbili mahususi kwa ajili ya udaktari na kozi nyingine za afya, SUA mahususi kwa ajili ya Kilimo hilo tawi la Mbeya ni mahususi kwa ajili ya kozi zipi?
 
Wapeleke mara ya ngapi?
wapeleke tu icho chuo kwa wajomba zangu upande wa mama, pale Iringa (academic town). kule kuna maeleo mengi sana watapewa hata 2000
 
Waje Kagera eneo lipo tutawapa.
 
Badala ya kujenga UDSM kampasi ya Mbeya kwa nini kisijengwe chuo kikuu cha Mbeya?

Kwa nini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa wa Mbeya?
Sioni tatizo hapo kwa sababu hata Sokoine University ilikuwa kampasi ya UDSM na baada ya kijitosheleza kikawa Chuo kamili. Kwa hiyo hii kampasi ya Mbeya ikijitosheleza itakuwa Chuo kamili.
 
Vyuo vingine vikubwa duniani kama Havard huwa vinakuwa na branches nyingi nyingi katika nchi zao?

..sina uhakika kama Harvard wana matawi nje jimbo waliloko ambalo ni jimbo la Massachusetts.

..lakini viko vyuo vikuu vingine vikubwa duniani ambavyo vimekuwa na matawi nje ya mahali vilipoanzishwa.

..nitakurudisha ktk historia ya vyuo vikuu ktk ukanda wetu wa AFRIKA MASHARIKI.

..chuo kikuu cha Makerere kilianza kama tawi la London University. Wahitimu toka Tz, Ug, na Kya, wa miaka ya 50 walitunukiwa shahada za London University ingawa walisomea Kampala.

..Pia chuo kikuu cha Dar Es Salaam nadhani shahada za kwanza za sheria zilikuwa za London University.

..Baadae Dar Es Salaam kikawa sehemu ya University of East Africa, kabla ya kila nchi kuamua kuwa na chuo kikuu chake.

..Tuje kwenye chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Muhimbili ilikuwa kitivo cha Tiba, kabla haijaamuliwa iwe chuo kikuu kinachojitegemea.

..Twende IFM hapa Dsm. IFM kunatolewa shahada ya MBA toka chuo kikuu cha Strathclyde kilichoko Scotland.

..Kwa maoni yangu, sio vibaya chuo kikuu chochote kuwa na matawi ktk maeneo tofauti na pale kilipoanzishwa.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…