Lakini inapendeza zaidi kikijengwa sehemu moja kwa ajili ya kurahisisha utawala!Muhimu wasilazimishe kutafuta hizo hekari 500 kwa kuwapora wanyonge ardhi yao, wakitaka kuzipata wawe tayari kuwalipa fidia wote watakaoathirika na hili wazo la Kikwete.
Sioni sababu kwanini wasijenge vitu vichache vya msingi kwa eneo lililopo, hizo nyumba za wahadhiri, hosteli, na hospitali vinaweza kuwa sehemu nyingine bora pasiwe mbali sana na chuo, kuliko kulazimisha vyote viwe pamoja kama chuo kimekuwa mbuga ya wanyama.
Changamkeni. Tengeni eneo kubwa kujenga chuo halafu muwape bure chuo chochote kinachohitaji wajenge tawi. Hata kama ni maeneo mawili au matatu tengeni.Serikali haiwezi kutukubalia, kama ilitunyima Bukoba University miaka hiyo, unahisi itakubali sahizi.
..sina uhakika kama Harvard wana matawi nje jimbo waliloko ambalo ni jimbo la Massachusetts.
..lakini viko vyuo vikuu vingine vikubwa duniani ambavyo vimekuwa na matawi nje ya mahali vilipoanzishwa.
..nitakurudisha ktk historia ya vyuo vikuu ktk ukanda wetu wa AFRIKA MASHARIKI.
..chuo kikuu cha Makerere kilianza kama tawi la London University. Wahitimu toka Tz, Ug, na Kya, wa miaka ya 50 walitunukiwa shahada za London University ingawa walisomea Kampala.
..Pia chuo kikuu cha Dar Es Salaam nadhani shahada za kwanza za sheria zilikuwa za London University.
..Baadae Dar Es Salaam kikawa sehemu ya University of East Africa, kabla ya kila nchi kuamua kuwa na chuo kikuu chake.
..Tuje kwenye chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Muhimbili ilikuwa kitivo cha Tiba, kabla haijaamuliwa iwe chuo kikuu kinachojitegemea.
..Twende IFM hapa Dsm. IFM kunatolewa shahada ya MBA toka chuo kikuu cha Strathclyde kilichoko Scotland.
..Kwa maoni yangu, sio vibaya chuo kikuu chochote kuwa na matawi ktk maeneo tofauti na pale kilipoanzishwa.
Kagera ardhi ipo ya kutosha tunawakaribisha wakinyimwa ardhi huko, waje kagera.Changamkeni. Tengeni eneo kubwa kujenga chuo halafu muwape bure chuo chochote kinachohitaji wajenge tawi. Hata kama ni maeneo mawili au matatu tengeni.
Serikali haiwezi kutukubalia, kama ilitunyima Bukoba University miaka hiyo, unahisi itakubali sahizi.
Kwa sasa wameshutuka, ngoja tuone ndani ya miaka 10 ijayo kama wataweza.Itakubali kama wabunge na madiwani wenu wote wataamua kuwa na msimamo mmoja kutaka hivyo bila kukoma.
Mnafanya siasa, Mbeya University of Science and Technology (MUST) imejengwa kule Iyunga na Sistila na wakapewa eneo kubwa tu na watu wakalipwa fidia. Halafu eneo ambalo wanalopewa siyo eneo ambalo linakaliwa na watu, ni eneo ambalo litakuwa wazi tena ardhi yake haiko chini ya Granted Right of Occupancy. Kwanini mnahisi kwamba kila kitu anachofanya Mzee Kikwete ni dhulma tu ???Muhimu wasilazimishe kutafuta hizo hekari 500 kwa kuwapora wanyonge ardhi yao, wakitaka kuzipata wawe tayari kuwalipa fidia wote watakaoathirika na hili wazo la Kikwete.
Sioni sababu kwanini wasijenge vitu vichache vya msingi kwa eneo lililopo, hizo nyumba za wahadhiri, hosteli, na hospitali vinaweza kuwa sehemu nyingine bora pasiwe mbali sana na chuo, kuliko kulazimisha vyote viwe pamoja kama chuo kimekuwa mbuga ya wanyama.
Kagera ndio hakufai kabisa, nani aje kusoma sweken shitimbi huko. nafikiri kama wakiona Mbeya hawana eneo, wapeleke Shinyanga, Arusha, Songea au Sumbawanga wakapambane na wachawi huko.Msingependa kuwa na Kagera University?
Msisubiri wanyimwe, tengeni eneo halafu waiteni. Waambieni, "Mzumbe hapa tuna ekari 200, kama mnaweza chukueni mjenge chuo. Vigezo na masharti kuzingatiwa." Kuweni proactive.Kagera ardhi ipo ya kutosha tunawakaribisha wakinyimwa ardhi huko, waje kagera.
Unaongelea nchi gani? Me nimesoma Germany [emoji629], Gottingen University na kina matawi. Vyuo vikubwa karibu vyote vina matawi nchini mwao na nje kama China na Africa na vingine vinaingia collaboration ili vijitanue.Unafuu huo ni upi? Mbona kwenye nchi nyingine zenye vyuo bora vya umma hawavipanui kwa kuanzisha matawai mengi ndani ya nchi hiyo moja?
Harvard University ina eneo kubwa sana ambalo ni mji wao kabisa, lakini wenzetu hawana haja ya kuanzisha Constituent Universities kwasababu nchi ina uwezo wa kuanzisha vyuo vikuu vingine vikubwa. Sisi Tanzania hatuwezi tu kuanzisha vyuo vikuu kama uyoga, hatuna rasilimali hizo. Ndiyo maana utakuta tuna wahadhiri wanafundisha vyuo zaidi ya viwili,....Vyuo vingine vikubwa duniani kama Havard huwa vinakuwa na branches nyingi nyingi katika nchi zao?
Unaujua Jitegemee Sec,Makongo Sec ni ekari ngapi?Mkuu, Sekondari ni ekari 3½ kwa mjini na 5 kwa maeneo ya mashambani.
Kagera siyo sitimbi, nchi inayopakana na nchi tatu utasemaje ni sitimbi?Kagera ndio hakufai kabisa, nani aje kusoma sweken shitimbi huko. nafikiri kama wakiona Mbeya hawana eneo, wapeleke Shinyanga, Arusha, Songea au Sumbawanga wakapambane na wachawi huko.
Chuo kuwa na matawi nje ya nchi sioni tatizo,chuo kuwa na matawi ndani ya mkoa mmoja sioni tatizo, ambacho sielewei ni chuo cha serikali kuwa na matawi katika mikoa tofauti ndani ya nchi. Kwa nini serikali isianzishe vyuo tofauti vinavyojitegemea katika kila mkoa au kanda?
Itashindikana kukiendeleza hapo mbele, eneo ni dogo sana kwa Chuo. Angalia UDOM ilivyo na eneo kubwa mpaka raha.Safi sana Kikwete. UDSM inapewaje ekari 50 imekuwa sekondari hiyo?
Kwani mbeya hawana chuo kikuu?Badala ya kujenga UDSM kampasi ya Mbeya kwa nini kisijengwe chuo kikuu cha Mbeya?
Kwa nini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa wa Mbeya?
Well said [emoji122]Harvard University ina eneo kubwa sana ambalo ni mji wao kabisa, lakini wenzetu hawana haja ya kuanzisha Constituent Universities kwasababu nchi ina uwezo wa kuanzisha vyuo vikuu vingine vikubwa. Sisi Tanzania hatuwezi tu kuanzisha vyo vikuu kama uyoga, hatuna rasilimali hizo. Ndiyo maana utakuta tuna wahadhiri wanafundisha vyuo zaidi ya viwili,....
Apo ata viwanja vya mpira ni ngumu kupataMkuu, Sekondari ni ekari 3½ kwa mjini na 5 kwa maeneo ya mashambani.