Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Vyuo vingine vikubwa duniani kama Havard huwa vinakuwa na branches nyingi nyingi katika nchi zao?
Yep. Hapa US vyuo vingi maarufu tu pia vina branches nyingi tu. John Harvard University ina branches tatu, moja ipo Cambridge (hii ndiyo kubwa kabisa), campus ya pili ni ya Afya ipo Boston mjini (Longwood) na ya tatu ipo opposite na MIT (just crossing Charles River).
University of California ina campus around 9-10 kubwa yao ikiwa Berkeley. University of Texas pia ina campuses kadhaa (Austin, Dallas, El Paso); na vyuo vingine vingi tu vipo hivyo mkuu. Hoja ya JK ina mashiko.
 
Naunga mkono, na mpaka sasa huwa najiuliza watu walioplan ardhi ya UDSM main compus,maana nipakubwa mpaka Leo hapajajaa..safi sana.

Sema elimu yetu ya hovyo sana michepuo yetu bado ileile. Tuwekeze zaidi kwenye sayansi na tafiti za kutosha hasa katika kilimo na teknolojia..
 
Hekali hizo 1000 + zinapatikana pale mkoani Songwe , wahamishie hapo hicho chuo mambo yakakaa mwakekabisa.
 
Hata Secondary hazitoshi kwa wenye mtazamo wa mbali
Chuo bora siyo ukumbwa wa eneo ama majengo. Wekezenj kwenye ujenzi wa ubongo.

Huko SUA na UDSM kwenye eneo kubwa kuna lipi la maana limefanyika zaidi ya kuwa kinara wa ngono?
 
Chuo bora siyo ukumbwa wa eneo ama majengo. Wekezenj kwenye ujenzi wa ubongo.

Huko SUA na UDSM kwenye
Natambua umuhimu wa kuwa na eneo kubwa la taasisi Kama chuo kikuu , mfano ni Sasa wanafunzi wa udsm wanavyo hangaika kupata vyumba vya kulala mpaka wanapanga nje ya chuo.

Lakini mipango Bora ya ubongo ni muhimu iendane na mahitaji makubwa ya baadaye !

Unafikiri miaka 100 + ijayo idadi ya watu itabakia hii ??
 
Atumie ushawishi wake kukitwaa chuo cha kilimo uyole, hizo ni akili finyu sana campus college unataka ekari 500 akili gani hizo? Wahame tu apeleke hio college Chalinze.
 
awamu ya nne ilikuwa ya kifisadi mno,

matumizi mabaya ya madaraka,

baba mkuu wa chuo,

Mama Mbunge

Mtoto Mbunge,

Kwa kodi zetu.
 
Point nzuri sana; siyo lazima chuo kiwe katika eneo moja tu lililoshikana (contiguous). Madarasa, maabala, maktaba na ofisi vinaweza kuwa sehemu moja, mabweni eneo jingine na vile vile nyumba za waalimu na wafanyakazi zikwa sehemu nyingine tofauti. In fact, mazingira mazuri ya waalimu siyo kuwaweka waishi sehemu moja kama vile wanaishi kwota.
 
Kesho au keshokutwa utasikia chuo kinapelekwa Bagamoyo kwa kuwa.....
-Eneo la ekari 600 limepatikana
-Gharama za kuwafidia watu ni kidogo.
-China iko tayari kutusaidia bure kutujengea chuo, lakini lazima iwe Bagamoyo.
-Miundo mbinu muhimu kama maji, umeme, barabara, bandari viko karibu na eneo husika.

Kikwete mimi namjua, ni mjanja mjanja sana na anajua kucheza na bit.
 
watu wanaongezeka,miji inakua,teknologia na mahitaji yanatanuka ndio maana wanaforecast long term plan unafikiri mbeya baada ya miaka 20 au 30 itakua hivyohivyo
 
Vyuo vingine vikubwa duniani kama Havard huwa vinakuwa na branches nyingi nyingi katika nchi zao?
hata navyo vilianza kama branches lakini badae ndio vikawa hivyo,mfano Sokoine University of Agriculture kilikua ni branch ya UDSM by that time lakini sasa ni chuo kamili
 
kwa sasa hawezi maana angetaka angefanya akiwa Raisi na hata kama itawezekana itakua ni mpango mwingine
 
kwa sasa hawezi maana angetaka angefanya akiwa Raisi na hata kama itawezekana itakua ni mpango mwingine
 
Hivi lile eneo la Whitesands linafanyiwa nini sasa? UDSM ni mabingwa wa kuhodhi maeneo. Kama wamepanga kupeleka taasisi hiyo sehemu nyingine si waseme tu, maana maagizo ya kwenda Mbeya yalitolewa na Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…