Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Badala ya kujenga UDSM kampasi ya Mbeya kwa nini kisijengwe chuo kikuu cha Mbeya?

Kwa nini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa wa Mbeya?
Nawao mbea wataanzisha cha kwao baadae wataenda kufungua campus yao Dar es salaam.
Au nasema uongo.
 
watu wanaongezeka,miji inakua,teknologia na mahitaji yanatanuka ndio maana wanaforecast long term plan unafikiri mbeya baada ya miaka 20 au 30 itakua hivyohivyo
Miji inakua, lakini siyo kweli kuwa chuo lazima kiwe katika eno moja contiguous. Likipatikana eneo hilo, basi itakuwa ni jambo zuri, lakini siyo kunyang'aya raia maeneo yao ili kupata eneo contiguous kwa ajili ya chuo miaka 50 ijayo. wakitaka eneo kubwa namna hiyo, wasijenge mjini; Nyerere alijenga UDSM nje kabisa ya mji na kutoa eneo kubwa ililo nalo leo, hakuomba eneo kubwa pale Lumumba kilipokuwa.
 
Waende hata hapo jirani Mkoa wa Rukwa nina uhakika watapata hizo ekari 500. Ipeni fursa na mikoa ya pembezoni.
 
Tafiti zinahitaji pesa/budget.

Hapo ndipo ugumu ulipo.
 
Tatizo wengi wanatembea vichwani mwao na sababu za kukariri, hawajui hivyo tunavyoviona leo vilijengwa wakati population ya eneo husika ilikuwa ndogo, sasa hivi miji imekuwa na idadi ya watu imeongezeka.

Kwasasa ni ngumu sana kupata eneo lenye ukubwa huo maeneo ya mijini, vinginevyo waende porini wakajenge miundombinu ya barabara, maji, na umeme kwanza, then ndio waweke hicho chuo na mahitaji yake kama hosteli, nyumba za walimu n.k

Nashangaa watu wanasema forecasting ya 20-30 yearz to come, kama vile sasa hivi hakuna watu wenye maeneo yao ambao tayari wameshayaendeleza pale ambapo hicho chuo kinaweza kujengwa, wao wanafikiria kama vile bado tupo 1961.
 
Badala ya kujenga UDSM kampasi ya Mbeya kwa nini kisijengwe chuo kikuu cha Mbeya?

Kwa nini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa wa Mbeya?
Inaitwa grooming

Unaanza na affiliation kwanza halafu baadae mnamature mnaanza kujitegemea
1. Chuo cha afya Muhimbili kilikuwa part ya UDSM, sasa hivi kinajitegemea
2. Sokoine ilikuwa part ya UDSM sasa hivi kinajitegemea
3. Ardhi university ilikuwa part ya UDSM sasa hivi kinajitegemea
 
Miji inakua, lakini siyo kweli kuwa chuo lazima kiwe katika eno moja contiguous. Likipatikana eneo hilo, basi itakuwa ni jambo zuri, lakini siyo kunyang'aya raia maeneo yao ili kupata eneo contiguous kwa ajili ya chuo miaka 50 ijayo.
chuo sio lazima kijengwa katikati ya mji wanawezakutafuta eneo nje kabisa ya mji ambapo hakuna makazi wakajena pia hii husaidia kitanua miji mfano UDOM wakati wanatega lile eneo kulikua ni porini vibaya mpaka watu wakashangaa lakini saivi kule kumekua mjini huduma zimesogea
J.Kikwete ni visionary sana
 
Waje Mtwara niwauzie viwanja vya ukoo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mwambie mama Tibaijuka ndo anajua kutetea ardhi ya mkoa KUMEGWA
 
Kuwa na makazi pekee hakutoshi kufanya eneo lionekane halina mwenyewe, yapo mashamba yenye wenyewe huko porini, na mpaka Kikwete anaambiwa chuo kimeshindwa kupata eneo la ukubwa analotaka maana yake kuna sababu, na sababu mojawapo kubwa ni hiyo, maeneo mengi tayari yako occupied sio mapori tu yasiyo na wenyewe au pasipo na makazi ya watu, ndio maana nawaambia wakiendelea kulazimisha wawe tayari kulipa fidia.
 
Eneo la Tanganyika parkers lipo kubwa tu zaidi ya eka 3000 kwa Nini wasigawe. Halafu liko Mjini kabisaaa
 
Siyajui maeneo ya Kampasi, lkn kwa vyovyote vile eneo kubwa ni muhimu sana kwa higher learning Institutions zenye hadhi kama UDSM. Let us make a comparison with some USA universities.

1. Berry College​

With 27,000 acres (110 km2),

2. United States Air Force Academy​

This College has approximately 18,455 acres which makes it the 2nd largest campus in the USA

3. US Military Academy​

The area of this largest campus is approximately 16,080 acres. This biggest academy has taken 3rd position by the site in the USA.

4. University of the South​

With the 13,000 acres, the campus has taken 4th place by area in the USA.

Pennsylvania State University​

The region of this University campus is approximately 8,556 acres

6. Stanford University​

It has the largest university campus in America, which contains 8180 acres

7. Liberty University​

The University area has to take 7,000+ acres which reach the 7th position by area in the USA.

8. Michigan State University​

With the 5,239 acres, the campus has taken8th place by area in the USA.

9. Texas A&M University​


With the 5,115 acres, the largest university campus has taken 9th position by area in the United States and the biggest university in Texas.

10. Tuskegee University​

It has another largest university campus in America, which contains 5,000 acres.

11. University of Minnesota​


With the 2730 acres, the campus has taken 11th place by area in the USA.

12. Ohio University​

The University area has to contain 1764+ acres, taking the 12th position by area in the USA.

Eneo kubwa ni muhimu.....
 
Elimu ni gharama na uwekezaji suala la kufidia ni sehemu ya uwekezaji bro mbona ni simple logic, ninavyojua miradi karibu yote serikali inapotaka kuwekeza huwa wanalipa fidia
 
Umeskia wapi?
 
Kikwete kapiga bull.
Mbeya hawezi kukosa eka 500.
 
Sababu nchi hii kila kitu lazima atafutwe wa kulaumiwa
 
Mkuu kaongea vizuri kama Mbeya hawana ardhi ya kutosha ekari 500 basi hilo tawi la UDSM litaenda kuanzishwa mikoa mingine kama Rukwa, Katavi na kwingineko kwenye mapori meengii tuu yasiyo na mwenyewe.
 
Nadhani nchi hii hatutakuja kukubaliana hata jambo moja. Yaani hata hili watu wanambeza Jakaya??? Acre 50 chuo au primary hiyo. Halafu Kikwete mwenyewe anayewapigania mpate eneo kubwa nna uhakika wajukuu zake hawatakuja kusoma huko. Watanzania tuna vichwa vya mende kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…