Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Mnataka kuzalisha ma graduate zaidi, kwani Hawa waliopo mmewafanyia Nini?
Kazi mnapeana wenyewe, kila anayeteuliwa ana koneksheksheni watoto wa wakulima Ni waendesha boda Boda na wamachinga, nao pia mmeanza kuwaandama hata kabla ya 17/3/2022
 
Eneo la Tanganyika parkers lipo kubwa tu zaidi ya eka 3000 kwa Nini wasigawe. Halafu liko Mjini kabisaaa
Au chuo cha Uyole, wana ekari zaidi ya elfu tatu na wapo mjini kabisa. Pale ndiyo eneo zuri kabisa. Watoe ekari 500 UD wajenge chuo.
 
Unafahamu Marekani kieneo ni kubwa mara kumi zaidi ya Tanzania?
 
Nina swali fikirishi je hicho chuo ni kwamba kilianzishwa bila kuwa na 'plan' ?

Maana kama plan ilikuepo why wategemee sandakalawe ya kipande cha ardhi kama ujenzi ulikuwa planned?
 
Nina swali fikirishi je hicho chuo ni kwamba kilianzishwa bila kuwa na 'plan' ?

Maana kama plan ilikuepo why wategemee sandakalawe ya kipande cha ardhi kama ujenzi ulikuwa planned?
Labda waliahidiwa eneo, halafu leo wanaambiwa wanapewa 50acres. Maan vyuo vingi vimepewa maeneo Mbeya. Mzumbe na CBE wote wamepewa eneo.
 
hiyo Forest anayoisema Kikwete anataka wapeweko hekali 500-1000 ni ipi? au anatafuta migogoro na wananchi huyu mkwere?
 
Ekari 50 kwa chuo kikuu ni ndogo, labda kama ni maeneo ya mjini...
 
Kama wanavyo tayari kwa nini UDSM inaenda kufungua tawi huko? Hizo pesa kwa nini wasizitumie kuboresha miondombinu na kutoa scholarships za chuo????
Business oriented
 
..kuna chuo kikuu tayari.

..lakini watakuwa mabwege wakiichezea fursa hii iliyowaangukia.

..kuna mikoa na maeneo mengi hapa Tz yanamezea mate fursa ambayo Mbeya wameipata.
Naunga mkono hoja ya Jakaya Kikwete mbeya wakipata campus ya udsm mkoa utaendelea sana kijamii na kiuchumi.
 
"Hii siyo sekondari kupewa ekari 50, tunataka eneo kubwa la ekari 500 hadi 1000 tenga hata kule Forest, mkishindwa tunahamia mkoa mwingine utakaoweza kutoa eneo kubwa, huu ni ujumbe kwa nyie viongozi" amesema Kikwete.

Ni lazima waTanzania tuwe tunafikiria na kuwaza kesho na ufanisi wa shughuli tunayotaka kuifanya, tuache roho ya umasikini kuona ekari 500 ni nyingi sana hata ikiwa ni kwa ajili ya ukulima wa mtu mmoja. Hongera mzee Jakaya Kikwete kwa kuwapa ukweli, waTanzania wenye mawazo ya uchoyo kuwa kumiliki kingi ni dhambi !
 
Nadhani mfumo kama wa University Of London ni mzuri. Ambayo ina 17 member institutions and three central academic bodies. Mfano, UCL, LSE, City University, Queen Mary University etc.

Hata baadae zinawezeza kujitenga kama zikitaka kama Imperial College.

Wanaweza kuanzisha University Of Mbeya lakini ni member wa University Of Dar Es Salaam.
 
Mbeya tayari kuna vyuo vya serikali vya MUST na Mzumbe kwa nini visipanuliwe hivyo na viwe vikubwa kama UDSM badala ya kuendelea kuhamishia matawi ya vyuo vingine huko?
Kwaiyo Mzumbe kuwa na tawi Mbeya haina shida, ila UDSM ndio sio sawa ?
 
[QUOTE="bagamoyo, post: 40917988, member: 209]
Ni lazima waTanzania tuwe tunafikiria na kuwaza kesho na ufanisi wa shughuli tunayotaka kuifanya, tuache roho ya umasikini kuona ekari 500 ni nyingi sana hata ikiwa ni kwa ajili ya ukulima wa mtu mmoja. Hongera mzee Jakaya Kikwete kwa kuwapa ukweli, waTanzania wenye mawazo ya uchoyo kuwa kumiliki kingi ni dhambi !
[/QUOTE]

Leta master plan yenu ya mnachotaka kujenga... Jengeni hizo hamsini kwanza,tuone mtaishia wapi. Kikubwa kabisa tuhakikishieni mtapata fedha wapi za kufanya yote hayo. Tuwape 500 ama 1000 Halafu eneo likae miakia hamsini halijaendelezwa, hilo halikubaliki.
 
Mie sipendi yaan khaaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…