Rais Mstaafu Jakaya Kikwete agomea eneo la ekari 50, ataka ekari 500

Tuache utani ekari 500 ni sawa na mita 70 x ekari 500 = 35,000 meter square then ukigawanya kwa mita 100 kujua ni viwanja vya mpira vingapi vyenye square mita sawa ni sawa sawa na viwanja 350 vya mpira vyenye mita square 100 kila upande.
Mkitaka eneo tupu la pamoja lisilo na makazi kama fidia hamtolipa basi nendeni Chunya wilaya maana huko kote ni mkoa wa Mbeya na ni wilaya kubwa kuliko zote mkoa wa Mbeya na ni wilaya inayoongoza kwa maeneo yake makubwa kutokaliwa na watu,hata ekari buku mtapata ila mkae mkijua pande zote mtazungukwa na wanyama pori tu.
 
IFM sio chuo kikuu, ni taasisi ya Elimu ya juu.
 
Naunga mkono hoja ya Jakaya Kikwete mbeya wakipata campus ya udsm mkoa utaendelea sana kijamii na kiuchumi.
iende pale ipeleke changamoto kwenye vyuo vilivyopo. wanafunzi wanaomaliza vyuo vilivyopo mbeya wengi wanaishia kuendesha bodaboda na bajaji kutokana na kupata elimu ya kiwango cha chini, hawaajiriki.
 
Badala ya kujenga UDSM kampasi ya Mbeya kwa nini kisijengwe chuo kikuu cha Mbeya?

Kwa nini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa wa Mbeya?
Hili nalo neno
Kila mkoa uwe na chuo chake
 
Badala ya kujenga UDSM kampasi ya Mbeya kwa nini kisijengwe chuo kikuu cha Mbeya?

Kwa nini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika mkoa wa Mbeya?
Mbeya kama kijiji
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Atumie ushawishi wake kukitwaa chuo cha kilimo uyole, hizo ni akili finyu sana campus college unataka ekari 500 akili gani hizo? Wahame tu apeleke hio college Chalinze.
Kuna kitu kinaitwa future expansion. Hebu waza kikubwa mkuu
 
Kwenye baadhi ya miradi ni lazima "Raia" wapishe. Cha msingi walipwe fidia zao wakapate maeneo mengine.
Ukiwafanya "Raia" wawe untouchable utashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo. Au vinginevyo barabara, zahanati, vituo vya afya, n.k utaenda kujenga baharini huko kusiko na watu au kwenye mapori ya Selous
 
Yaani nchi inashangaza sana, watu wanapinga hadi upanuzi cha chuo. Mimi nilijua labda JK anataka shamba alime yeye na familia yake.
 
Mnataka kuzalisha ma graduate zaidi, kwani Hawa waliopo mmewafanyia Nini?
Kazi mnapeana wenyewe, kila anayeteuliwa ana koneksheksheni watoto wa wakulima Ni waendesha boda Boda na wamachinga, nao pia mmeanza kuwaandama hata kabla ya 17/3/2022
Kwahiyo tuache kuzalisha wasomi ?
Tubomoe shule na vyuo ?
 
Naunga mkono hoja ya Jakaya Kikwete mbeya wakipata campus ya udsm mkoa utaendelea sana kijamii na kiuchumi.
Tayari wanayo, huu mwaka wa 6 au wa 7 wapo Mbeya. Ila wanatumia facilities za hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya.

Ili kujenga majengo yao pqmoja na hospitali, wanahitaji eneo kubwa zaidi. Wamezikataa ekari 50 kwamba hazitoshi.

Graduates wa kwanza wa Udaktari wa UDSM Mbeya College of Health and Allied Sciences wamehitimu mwaka jana, mahafali ya leo walikua ni batch ya pili kuhitimu.
 
Kulipa fidia ili kupisha miradi ya serikali ni kweli na ndiyo utendaji haki, ila siyo uamuzi mzuri wa serikali kutumia raslimali zake kulipa fidia ili kujenga chuo ambacho kinaweza kujengwa sehemu nyingine bila kulipa fidia. Halihii ni tofauti kabisa na ujenzi wa miundo mbinu kama barabara na reli ambayo topographic conditions zinakuwa zinataka ipite eneo fulani ambalo tayari linatumiwa na raia. Ujenzi wa zahanati na vituo vya afya unaweza kusababisha baadhi ya raia wakahamishwa kusudi kuziweka huduma hizo ziwe karibu na wananchi wengi wanaolengwa na huduma hizo. Chuo kikuu hakilengi watu wa Mbeya tu, kinaweza kuwa popote, na hivyo kulipa watu fidia kusudia maeneo yao yatumiwe na chuo kikuu ni matumizi mabaya ya raslimali za serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…