Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nakumbuka katika kikao Cha mkutano Mkuu wa CCM, iliofanyika jijini Dodoma mwaka 2012, Jakaya Kikwete, akiwa ni Mwenyekiti wa CCM wa Taifa na wakati huo huo akiwa ni Rais wa Tanzania wa awamu ya 4 aliwaonya vikali CCM kuwa wasilitegemee Jeshi la Polisi, kuwafanyia siasa na badala yake wapambane wao wenyewe na vyama vya siasa vya upinzani Kwa hoja.
Aliendelea kudai kuwa wajibu mkubwa wa Jeshi la Polisi ni kuwalinda raia wote na Mali zao, bila kujali kuwa ni wa chama gani na Wala siyo kuwalinda watawala waliopo kuendelea kukaa madarakani.
Inaelekea hao CCM wamepuuza ushauri huo na badala yake wameendelea tu kuwatumia Jeshi la Polisi Kwa maslahi yao.
Nimesema kuwa wao CCM wameendelea kuwatumia Jeshi la Polisi Kwa maslahi yao, kutokana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa Polisi nchini, ACP David Misime, siku ya tarehe 12 mwezi huu, akiongea na waandishi wa habari, akiwaambia kuwa wao Jeshi la Polisi wamepiga marufuku maandamano ya amani yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kuwa yatafanyika jijini Dar tarehe 23 mwezi huu iwapo tu, Jeshi la Polisi, ifikapo tarehe 21 mwezi huu, itakuwa bado haitawarejesha viongozi wao waliotekwa na watu inayodai Jeshi letu la Polisi, kuwa ni watu wasiojulikana!
Lazima itambulike kuwa wajibu namba Moja wa Jeshi la Polisi ni kuwalinda raia na Mali zao, sasa kutokana na wimbi kubwa linaloendelea nchini hivi sasa la raia kuendelea kutekwa na wengine kuuawa kinyama bila hatua zozote kuchukuliws na Jeshi la Polisi, ni dhahiri kuwa Jeshi la Polisi, limeshindwa wajibu wao namba Moja wa kuwalinda raia na Mali zao na wanalazimika viongozi wake wakuu, ambao ni Waziri wa Mambo ya ndani, Yusufu Masauni na IGP, Camilius Wambura wajuzulu mara moja.
Hiki kiburi Cha kutotaka kuwajibika Kwa hao viongozi wawili ni dharau Kwa watanzania, waliowapa dhamana hiyo na badala yake wanashuhudia watanzania wakiendelea kutekwa na kuuawa wakati wao wakienddlea kung'ang'ania nafadi zao!
Suluhisho pekee la kusitisha maadamano ya Chadema siku ya Jumatatu ya tarehe 23 ni Kwa Jeshi la Polisi, kujitokeza hadharani kabla ya tarehe 21 na kueleza walipo viongozi wa Chadema na watu wengine waliopotea katika mazingira ya kutatanisha.
Kama Hilo lisipofanyika kabla ya tarehe tarehe 21, basi maandamano hayo ya amani yatafanyika tarehe 23, Kwa kuwa yanaruhusiwa Kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania