Escrowseal1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 4,618
- 4,605
Hiyo sahihi nahsi alimwambia mama salma amwekee office chair kwanza. Msoga gang na walamba asali ndo mjue kuwa kufa nako kupo hasa mnapojilimbikizia mali za walala hoi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo wewe ni 70+Ni vile tu hujui mkuu,ila member tumesoma wote pale Namupa seminary Lindi.
Unapokuwa mwanasiasa huwa unaondokwa na aibu, staha na utu.Natamani kuuona unafiki wa Msoga siku Edo akitangulia endapo Maulana amepanga atangulie kabla yake nami nikijaliwa uhai.
Bladfaqen.
Nimepokea kwa mshituko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe.
Nimemfahamu miaka mingi, tumetoka nae mbali na tumesaidiana kwa mengi. Familia zetu, na mapito ya maisha yetu yamehusiana sana.
Bernard Kamillius Membe alikuwa ni mtu wa msaada mkubwa kwangu katika maisha yangu ya kikazi na kisiasa. Nilimuamini na kumtumainia katika nafasi zote alizohudumu kwenye Baraza langu la Mawaziri. Aliwahi kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Mambo ya Ndani, na Wizara ya Nishati na Madini.
Halikadhalika, aliwahi kuwa Waziri wangu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataita kwa miaka 9 ambapo alifanya kazi kubwa na nzuri ya kuendeleza maslahi ya Tanzania katika medani za Kimataifa.
Nautambua mchango wake mkubwa alioutoa kwenye Chama Cha Mapinduzi alipokuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taita, Mjumbe wa Kamati Kuu na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Sekretariati ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Katika nafasi zote hizo, alijitoa kwa moyo wake wote na kuacha alama za kudumu.
Nilimfahamu Mheshimiwa Membe kama Mwanadiplomasia Mbobezi, Mwanamikakati makini, Msomi mzuri, Mcha Mungu, Mzalendo, Mchapakazi Hodari na mtu jasiri ambaye hakuogopa kusema na kulisimamia analoliamini. Hakika Taifa limepoteza mmoja wa watu wake muhimu.
Natoa salaam za rambirambi na mkono wa pole kwako Shemeji yangu Dorcas Membe na watoto wenu Cecilia, Richard na Dennis, pamoja na wajukuu, ndugu na jamaa wa Marehemu Bernard Kamillius Membe.
Nawapeni pole kwa msiba mkubwa uliowakuta, lakini napenda kuwahakikishia kuwa hamko wapweke. Mimi pamoja na Mke wangu Salma na wana familia wetu wote, tuko pamoja nanyi katika majonzi na kuomboleza.
Tunawaombea kwa Mola awajalie moyo wa subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu mnachopitia.
Tukumbuke daima, "Sisi sote ni waja wake, na kwake tutarejea” Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Tumuombee kwa mola marehemu mpendwa wetu, apumzike kwa amani na Roho yake aiweke Mahala Pema Peponi. Amina.
View attachment 2619640View attachment 2619643
View attachment 2619666
Mzee wa fitinaMwana mtandao
Najikuta natamani kuongozwa na kikwete. Kila zama na kitabuUbinadamu wa Jakaya unaweza kuuona hata katika maandishi yake
Urafiki wao haukuanzia njianiNatamani kuuona unafiki wa Msoga siku Edo akitangulia endapo Maulana amepanga atangulie kabla yake nami nikijaliwa uhai.
Bladfaqen.
Hakuna ampangiaye mwanadamu mwenzake siku ya kifo chake.Vipi Membe si mtu mzuri ndio maana kafariki, wanaompenda waende kuzikwa naye kama kejeli zilizo kuwa zinatoka dhidi ya JPM, tujue tu Kikwete na Makamba Sr siku zenu pia zinakaribia, na siku yenu ikifika kejeli zote mlizomtupia JPM zitatupiwa mizoga yenu pia.
Yawezekana ukatangulia wewe, na usiipate hiyo siku.Bado yeye..siku hiyo ntafanya bonge la sherehe.
Hata mimi nikitangulia hakuna tatizo ila tujue tu siku atakayokufa Kikwete, Makamba Sr, Lissu, Mbowe na takataka zote zilizotoa kejeli dhidi ya kifo cha JPM tutakumbushia tu msemo wao, “ wazuri hawafi”. Wavumilie tu na sisi furaha zetu wakati wanazika mizoga yao pia.Hakuna ampangiaye mwanadamu mwenzake siku ya kifo chake.
Unajuaje, pengine wewe utatangulia kabla ya Kikwete au Makamba?
Wangapi waliokuwa wenye afya njema wamekwishafariki lakini waliokuwa wamelazwa vitandani wakaamka kwenda barabarani?
Wazee wangapi wamekuwa wakihudhuria misiba ya vijana na watoto?
Kifo ni fumbo, hakuna anayeweza kujitapa kuwa analijua jibu lake.
Pole sana Jakaya kwa kufiwa na mtu wako wa karibu. Pole sana familia ya Membe.
Tumwombe Mungu aijalie Roho ya Bernard Membe pumziko la amani. Tunamwomba Mungu wa huruma na msamaha, akayatazame Mema yake na yakawe sababu ya msamaha pale alipopungukiwa kama mwanadamu.
Yule Mzee anaroho ya paka,na kuumwa kote kule?!