Assalaam alaykum wanajf,kumekucha!
Kabla sijaanza kutembeza Biashara yangu ya Al Kasus nikasema nitabaruku kidogo kutokea pale nilipoishia.
Mtoa hoja ni lazima ujue kutofautisha kati ya SERA ZA NCHI ZA MAMBO YA NJE na DIPLOMASIA YETU...these are two different entities.
Kwa nafasi aliyopo mstaafu mh.Jakaya Kikwete kamwe hawezi kuiwakilisha nchi kwenda kusimamia SERA YA MAMBO YA NCHI ZA NJE.
Yeye anapotoka kutuwakilisha basi hutambaa katika uwanda wa DIPLOMASIA YETU....hatoki nje ya hapo.
SWALI
Je anaweza kuiwakilisha nchi pasina ridhaa ya serikali iliyopo madarakani?!!!
JIBU
Nope,haiwezekani.
SWALI
Je safari yake nchini Burundi amepata mwaliko binafsi?!!
JIBU
Inawezekana ukawa binafsi ama ukapitia foreign affairs.
SWALI
Kama haukuwa wa kibinafsi,je alitumwa kumwakilisha mh.Rais?
JIBU
Inawezekana kuwa ni hivyo.
Niseme tu,mh.Jakaya NI mwanasiasa mbobezi na mwanadiplomasia wa haja zaidi ya mh.Membe,amehudumu foreign affairs muda mrefu.Amefundisha siasa Jeshini,NI mzalendo wa kiwango Cha SGR za magufuli.
Hebu mtafuteni mzee Chizii na mumuulize ni kwa nini marehemu mzee Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa anarudiarudia kusema kuwa walikuwa ni vijana watatu tu kwa kipindi kile aliowavisha ITIKADI ya chama na Sera za nchi na wakaiva kwa kiwango cha kukata na shoka.
Nakudokezea tu atakutajia;
1.Dr Jakaya Kikwete
2.Edward Ngoyai Lowassa
3.Abdulrahman Kinana
Kwa hiyo vijana wenzangu mkae mkijua kuwa haya MASUALA ya mh.Kikwete kuzodolewa kuwa eti yeye ni mhutu....ni kutokujua tu historia ya makabila hapa afrika kwani makabila yanabadilika majina kutokana na vizazi kuwa vingi na kuhama kutoka eneo moja kwenda jengine Kama nilivyodadavua hapo juu.
Kwani hao waitwao "wahutu" ndio babu wa makabila yote nchini Tanzania kasoro wale wahamiaji na wafugaji wa asili ya BONDE LA UFA.....
Insh'allah nikimaliza kutembeza Al Kasus yangu hapa Tandale kwa mtogole nitakuja kuwaelezea undani wa mashambulizi yanayoelekezwa kwa mh.Jakaya Mara tu alipoutoa ule ushauri wake kuntu juu ya kukaa mezani kwa mahasimu wa kikabila na kiitikadi wa nchini RWANDA ya komandoo Paul Kagame.
Nawasilisha.