Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe Jakaya Kikwete atunukiwa medali kwa mchango wake katika harakati za kurejesha amani nchini Burundi

Rais wa Burundi amemtunuku nishani ya amani Rais mstaafu wa Tanzania mh JM Kikwete kama ishara ya kuheshimu juhudi zake za kuleta amani nchini humo.

Nishani hiyo imepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Burundi kwa niaba ya mstaafu Kikwete.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hongera sana mheshimiwa Kikwete, kwa tuzo.
 
Ha ha umegundua huyu jamaa hajifichi , toka Genta mpaka Mzikulu na majina kibao hapo katikati
 
Mpatanishi wa Mgogoro wa Burundi ulikuwa chini ya Mwlimu Nyerere , na baada ya kifo; nafasi yake ilichukuliwa na Comrade Mandela na makubaliano yalisaniwa mwaka 2002 mjini Arusha. Rais aliyekuwa madarakani alikuwa Buyoya na baadaye alifuatia Nkurunziza aliyeleta taabu ya kuachia madaraka.
 


Nasubiri kwa hamu muendelezo wako ukimaliza kuuza al kasus
 
Nasubiri kwa hamu muendelezo wako ukimaliza kuuza al kasus
Oooo sawasawa,ngojea nikusanye videni vyangu vijiweni huku.......kahawa wamenikopa ee nikasema nihamie kwenye al kasus,yanajirudia yaleyale,mtu Wala hajui km lita za maziwa ghali,viungo mpake tuagize toka Chokocho Pemba na kule Mtae Lushoto,aaagh mamwinyi banaa....
 
Hongera sana hizo zote ni juhudi za serikali ya awamu ya tano
 
Asante kwa kuweka sawa but Mhe Kikwete ndo alikuwa Kama coordinator wa ule mgogoro kwa nafasi yake ya waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kwa kipindi hicho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…