Rais Mugufuli atakumbukwa na vizazi vingi wa Watanzania

Kwa lipi???🤣🤣🤣
Kwa kufanikiwa kuzuia utoroshaji wa Tanzanite kwenda Kenya na Indio waliokuwa wanaongoza kuuza Tanzanite duniani wakati hawana hata mgodi mmoja wa Tanzanite.

Kwa hili tutamkumbuka au vipi hili linaua demokrasia na diplomasia kimataifa?
 
Na KUTIA KIBINDONI TRION 1.5🤣🤣
 
Kama si mhusika Mkuu kwanini anapiga kimya kwenye matukio ya utekaji, utesaji, kupotezwa, kuuawa na hata uchunguzi wa matukio husika hataki? Haihitaji Phd ili kujua matukio mengi ya udhalimu tangu 2015 ambayo polisi hawakuyachunguza mhusika Mkuu ni yeye.

Kusikitishwa kwangu na kupotea kwa Ben ndio ushahidi wa kumhusisha mkulu kawa ndio muhusika?
 
Mkuu vipi bado mpaka leo huoni faida ya hii miladi?

Miladi hata mtoto wa chekechea ukimkabithi hazina anaweza kuifanya ni swala la kuchota pesa na kujenga jenga tu na kununua nunua tu midege na kujenga jenga tuu mijengo ya tume ya uchaguzi na mijengo ya mahakama. Hakuna mtu ambaye hajui ku spend hela bwana. Tatizo linakuja kwenye kuboresha ajira, afya, uchumi, na maendeleo ya watu kwa ujumla ndiyo tatizo uongozi. Ku spend hela za kuchota hazina siyo ujiniaz hata kilaza anaweza sawa dogo?
 
Kama si mhusika Mkuu kwanini anapiga kimya kwenye matukio ya utekaji, utesaji, kupotezwa, kuuawa na hata uchunguzi wa matukio husika hataki? Haihitaji Phd ili kujua matukio mengi ya udhalimu tangu 2015 ambayo polisi hawakuyachunguza mhusika Mkuu ni yeye.

Kwahiyo yeye kusema Kuna waropokaji na inabidi washughulikiwe kwako wewe ndio ushahidi kuwa yeye ndio mtekaji Ila watu wanao shitakiwa kwa kesi za uhujumu uchumi hadi wengine wanakili mahakamani mnasema kuwa wanabambikiwa kesi?

Unaushihidi upi kuwa matukio ya utekaji na mauaji hayachunguzwi na polisi au wewe ni mmoja wao?

Utaniuliza ni kwanini hawakamatwi, Kuna kesi ngapi hata huko nchi za nje zinachukua miaka na miaka wahusika hawajakamatwa hadi leo, mbona majambazi wanapora mali za watu humu mitaani mara nyingi tu mbona wengine hawajapatikana mpaka leo au ni yeye pia ndio anawatuma hao majambazi wakapore ndio mana hawakamatwi?

Katika matukio yote hayo yalio tokea lete ushahidi wa tukio moja uhusika wake usio shaka na si propaganda.
 
Miladi hata mtoto wa chekechea ukimkabithi hazina anaweza kuifanya ni swala la kuchota pesa na kujenga jenga tu na kununua nunua tu midege na kujenga jenga tuu mijengo ya tume ya uchaguzi na mijengo ya mahakama. Hakuna mtu ambaye hajui ku spend hela bwana. Tatizo linakuja kwenye kuboresha ajira, afya, uchumi, na maendeleo ya watu kwa ujumla ndiyo tatizo uongozi. Ku spend hela za kuchota hazina siyo ujiniaz hata kilaza anaweza sawa dogo?
Kama kujenga jenga ni rahisi namna hiyo mbona hizo awamu nyingine hazikuweza kujenga jenga au hawakuwa na hiyo hazina ya kuchota chota mahela?

Uchumi upi ambao hakugusa, afya ipi unaizungumzia mkuu mana vituo vya afya kila kata tena Kuna kata nyingine viko zaidi ya viwili, kugusa watu kivipi mkuu mana tunaona umeme hadi vijijini huko vipi hayo hayawagusi watu?

Wewe unataka aajiri tu hata Kama hakuna uhitaji huo serikalini Ila yeye aajiri tu si ndio, mfano walimu wa masomo ya arts wamejaa mpaka wengine wakashushwa kuja kufundisha shule za misingi alafu bado unataka aendelee kuajiri hao hao?
 
Wewe unadanganyika na takwimu za kupika wakati hali halisi ajira hakuna vijana wana miaka mitano wako mtaani hakuna vision ya kutengeneza ajira za vijana. Kujenga mijengo ya hospitali wakati watu hawana bima ya afya ni ulimbukeni. Propaganda zimekuingia sana wewe tanzania inakua kama north korea. Propaganda kila media zimshikiliwa kwa mtutu. Masaa 24 mnaangalia propaganda za kumtukuza mtu hadi zinawaingia kwenye damu. Kila anayesimama jukwaani anasifia tu ili apate cheo au asitumbuliwe. Wakati hali halis ya mtanzania ni mbaya. Umeme daliy wanakata. Maji mara moja kwa wiki . Ajira hakuna hela hakuna bima ya afya hakuna. Unajenga mradi moja kwa gharama ya nusu ya bajeti yote ya nchi unasahau mambo madogo yanayohusu wananchi.
 
Kama kujenga jenga ni rahisi namna hiyo mbona hizo awamu nyingine hazikuweza kujenga jenga au hawakuwa na hiyo hazina ya kuchota chota mahela?

Uchumi upi ambao hakugusa, afya ipi unaizungumzia mkuu mana vituo vya afya kila kata tena Kuna kata nyingine viko zaidi ya viwili, kugusa watu kivipi mkuu mana tunaona umeme hadi vijijini huko vipi hayo hayawagusi watu?

Wewe unataka aajiri tu hata Kama hakuna uhitaji huo serikalini Ila yeye aajiri tu si ndio, mfano walimu wa masomo ya arts wamejaa mpaka wengine wakashushwa kuja kufundisha shule za misingi alafu bado unataka aendelee kuajiri hao hao?

Ina maana vitu vilivyojengwa awamu zilizopita huvioni?
Hata hizo barabara anazotumia kwendea Chato zilijengwa na watangulizi wake.
 
Acha kuandika ujinga. Wewe una ushahidi wa kuonyesha uchunguzi unaendelea au unabwabwaja tu? Ben Saanane tangu apotee huu ni mwaka wa nne Azory mwaka wa tatu shambulizi la Lissu ni mwaka wa tatu. Hebu tuwekee ushahidi wa uchunguzi husika.

Narudia tena udhalimu wa kutisha unaoendelea Nchini mhusika Mkuu ni huyo dikteta.

Kwahiyo yeye kusema Kuna waropokaji na inabidi washughulikiwe kwako wewe ndio ushahidi kuwa yeye ndio mtekaji Ila watu wanao shitakiwa kwa kesi za uhujumu uchumi hadi wengine wanakili mahakamani mnasema kuwa wanabambikiwa kesi?

Unaushihidi upi kuwa matukio ya utekaji na mauaji hayachunguzwi na polisi au wewe ni mmoja wao?

Utaniuliza ni kwanini hawakamatwi, Kuna kesi ngapi hata huko nchi za nje zinachukua miaka na miaka wahusika hawajakamatwa hadi leo, mbona majambazi wanapora mali za watu humu mitaani mara nyingi tu mbona wengine hawajapatikana mpaka leo au ni yeye pia ndio anawatuma hao majambazi wakapore ndio mana hawakamatwi?

Katika matukio yote hayo yalio tokea lete ushahidi wa tukio moja uhusika wake usio shaka na si propaganda.
 
Waswahili husema, "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni".
Ni ukweli ulio wazi Sasa kuwa Rais Magufuli atakumbukwa na watanzania katika vizazi vingi vijanyo.
Kipindi chake cha uongozi kimekuwa na mambo mengi makubwa ambayo kiukweli yalihitaji ujasiri mkubwa kuyafanya.

Hakika Magufuli ni mtu mwenye uthubutu hata Kama akifeli baadhi ya mambo lakini watanzania wataiona nia yake njema.

Huu mkataba wa madini kusainiwa kwa mara ya kwanza Tanzania itanufaika na raslimali yake ya madini, hii inamfanya Magufuli kuingie kwenye vitabu vya kumbukumbu vya taifa hili hasa mtu atakapogusa nyanja ya madini. Huu ni ukweli ulio wazi japo Wana siasa wengi watapinga hili.
Vitosho na maneno mengi ya kukatisha tamaa mara kushitakiwa Miga n.k , laikini alisimamia msimamo wake hadi leo matokeo tumeyaona.

Itakapo tajwa kampuni mpya ya TWIGA moja kwa moja utamtaja Magufuli, ukitaja mabadiliko ya sheria za madini hapo lazima utamtaja Magufuli, chimbuko la mawazo ya kuanzishwa vitu hivi vyote ni yeye.

Hebu tuseme ukweli.
1; Wana Mwanza itawachukua miaka mingapi kumsahau Magufuli kwa uwepo la daraja la BUSISI? Waliwahi kuota kuwa wangekuwa na kitu Kama hiki?
Ujenzi wa Meli tano ziwa Victoria itawachukua miaka mingapi hadi kusahau.

2; Itatuchukua miaka mingapi hadi kusahau Tren ya Umeme SGR!!
Kila atakae iona hata Kama ni miaka 70 baadae jina la Magufuli litamjia kichwani.

3; Wananchi wa kigoma watamsahau vipi Magufuli kwa ujenzi wa mabarabara yanayounganisha mkoa wa kigoma na mikoa jirani, mkoa ambao Kama vile ulikuwa umesahaulika kabisa.

4; Tutakapoanza kutumia Umeme kutoka Bwawa la Nyerere tutamsahau vipi Magufuli watanzania.?

5; Utakapoona ndege za ATCL zikipasua anga atamsahau vipi Magufuli?

Hakika huyu ni shujaa wa taifa hili, wanasiasa watakataa kwasababu nawao pia wanahitaji kushika dola hivyo usitegemee kuwa watamuunga mkono Magufuli hata mara moja.
Lakini vitu anavyo vifanya vinajieleza.

Prof Lumumba hakuwa mnafiki aliposema " the Magufulification of Africa."

Licha ya mapungufu yake kiuongozi lakini hakika huyu ni kiongozi wa mfano wa kuingwa barani Africa.
Ni kweli ata kumbukwa kwa mengi. Hata la kuagiza soko zima waka jisaidie kwa Dc nayo ni maendeleo..
 
Hatuongei ovyo mkuu, lete ushahidi wa unacho kisema.
Atakumbukwa kwa yote, mema na mabaya. Kuna watu wamepotea awamu hii ya Magu unadhani ndugu zao watamsahau?, Wasiojulikana wanawiri zaidi awamu yake, kuna sheria kandamizi zimepitishwa, mfano ya mifuko ya hifadhi za jamii,.................lazima akumbukwe.
 
I will remember this guy for arbitrary killings by state security forces; torture; harsh and life-threatening prison conditions; arbitrary detention; political prisoners; arbitrary or unlawful interference with privacy; censorship, site blocking, and criminal libel; substantial interference with the rights of peaceful assembly and freedom of association; unlawful arrests and intimidation of civil society organizations, etc.
 
Back
Top Bottom