Rais Museveni amteua mwanae Muhoozi Kainerugaba kuwa CDF

Rais Museveni amteua mwanae Muhoozi Kainerugaba kuwa CDF

Sema kwasababu kiafrica ukiwa kiongoz unageuka mfereji wa familia lakin ukweli ndani ya familia wakati mwingine kuna watu ni Smart sana basi tu kiafrica Africa inaonekana sio.
Nchi sio familia, haifanani hata kidogo na familia, nchi inatakiwa iendeshwe kwa katiba na utaratibu ambao watu wengi wameafikiana na kukubaliana nazo ziwaongoze, sio kujifanyia mambo kienyeji tu kadri mtu anavyojisikia akiamka.
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemteua Mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu mpya wa Majeshi (CDF) Nchini Uganda akichukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri anayehusika na masuala ya biashara kwenye mabadiliko mapya aliyofanya katika Baraza la Mawaziri la Nchi hiyo usiku huu.

Muhoozi aliwahi kuwa kwenye nafasi ya Ukamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda lakini October 04,2022 Museveni aliamua kumuondoa na nafasi yake ikachukuliwa na Meja Jenerali Kayanja Muhanga ambaye alikuwa Kamanda wa Opereshemi Shujaa inayoendeshwa Nchini DRC.

Millard Ayo

Pia soma:

Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni dhahiri sasa amelewa madaraka. Ni kweli kwamba hajui madhara ya kauli aliyotoa kuhusu kuivamia Kenya?

Mtoto wa Museveni atangaza kugombea Urais 2026
The Beginning of the End!

Uzoefu duniani kote unaonyesha kwamba vitendo kama hiki alichofanya Rais wa Uganda huwa inakuwa mwanzo wa mwisho wa Utawala dhalimu uliofitinika beyond repair, "Fall of Museven in Uganda" is underway.
 
Kazi iendelee, Mu7 piga kazi mpaka maji waite Mma, hata sisi huku tuna muCCM unatupeleka mputamputa mwendo wa ngili mkia juu.
 
Museveni amejifunza kitu kutoka Tanzania baada ya Kifo cha Magufuli.

Kiuhalisia hakukuwa na Humuimu wa kumwachia Rais Samia madaraka hata kama alikuwa ni Makamu, kulikuwa kuna nafasi kubwa sana ya viongozi wengine kuchukua madaraka kama wangekuwa na ushawishi Jeshini.

Tanzania tuna mfumo mzuri sana na imara wa kupokezana madaraka kutoka CCM kwenda CCM, sio rahisi mtu mmoja kubaki na nguvu kubwa baada ya kumaliza Urais wake.

Tanzania tunachokosa ni viongozi wazuri kupokezana madaraka, yaani Baada ya Nyerere alipaswa aje Mkapa au Mtu kama Magufuli baada yake aje Makonda/Bashiru/Majaliwa/Mpina/Lissu kama angekuwa na malezi ya Nyerere/Mkapa au Magufuli tungekuwa sawa na China au Mataifa ya Ulaya kwa Maendeleo.

Bahati mbaya tuna sequence ya ovyo sana kwenye kuachiana madaraka, imagine Baada ya Mkapa tukapata Kikwete now tuna Samia, just imagine.

Museveni ameona hili na anataka kuwe na consistency ya Itikadi
 
Ndio maana linchi lake likubwa lenye kila rasilimali limeachwa mbali sana kiuchumi hata na vinchi vidogo vidogo kama Japan, Ujerumani, Italia na Uingereza
Russia pamoja na ukubwa wake wote na rasilimali lukuki kushinda nchi yoyote duniani lakini inazidiwa na kanchi kadogo kama South Korea au Japan nchi ambazo kupata hata kokoto tu ni shida kama ilivyo upatikanaji wa umeme au maji katika Tanzania.
 
Nchi sio familia, haifanani hata kidogo na familia, nchi inatakiwa iendeshwe kwa katiba na utaratibu ambao watu wengi wameafikiana na kukubaliana nazo ziwaongoze, sio kujifanyia mambo kienyeji tu kadri mtu anavyojisikia akiamka.
Ni kwa vile demokrasia zetu hazijakua na elimu zetu ni ndogo. Kwa Africa uongoz ni fursa tofauti na wazungu kwao uongoz ni legacy. Unaweza kuwa na baba rais akaja mtoto na hata mjukuu ishu ni kuwa ni kiongoz au ni fursa kama kampuni ya kurithi
 
Museveni amejifunza kitu kutoka Tanzania baada ya Kifo cha Magufuli.

Kiuhalisia hakukuwa na Humuimu wa kumwachia Rais Samia madaraka hata kama alikuwa ni Makamu, kulikuwa kuna nafasi kubwa sana ya viongozi wengine kuchukua madaraka kama wangekuwa na ushawishi Jeshini.

Tanzania tuna mfumo mzuri sana na imara wa kupokezana madaraka kutoka CCM kwenda CCM, sio rahisi mtu mmoja kubaki na nguvu kubwa baada ya kumaliza Urais wake.

Tanzania tunachokosa ni viongozi wazuri kupokezana madaraka, yaani Baada ya Nyerere alipaswa aje Mkapa au Mtu kama Magufuli baada yake aje Makonda/Bashiru/Majaliwa/Mpina/Lissu kama angekuwa na malezi ya Nyerere/Mkapa au Magufuli tungekuwa sawa na China au Mataifa ya Ulaya kwa Maendeleo.

Bahati mbaya tuna sequence ya ovyo sana kwenye kuachiana madaraka, imagine Baada ya Mkapa tukapata Kikwete now tuna Samia, just imagine.

Museveni ameona hili na anataka kuwe na consistency ya Itikadi
Kama kuna mtu anafikiria kwamba ni familia ya Museveni tu ndio ina hati miliki na maono ya kuweza kuiongoza Uganda basi ni dhihirisho la ufinyu wa fikra kwa mtu huyo.

Nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 haiwezi kutegemea kutawaliwa na familia ya mtu moja na kwa fikra za kipumbavu namna hiyo kutolewa na mwafrika inahalalisha kabisa Afrika kuwa hapa ilipo.
 
Museveni amejifunza kitu kutoka Tanzania baada ya Kifo cha Magufuli.

Kiuhalisia hakukuwa na Humuimu wa kumwachia Rais Samia madaraka hata kama alikuwa ni Makamu, kulikuwa kuna nafasi kubwa sana ya viongozi wengine kuchukua madaraka kama wangekuwa na ushawishi Jeshini.

Tanzania tuna mfumo mzuri sana na imara wa kupokezana madaraka kutoka CCM kwenda CCM, sio rahisi mtu mmoja kubaki na nguvu kubwa baada ya kumaliza Urais wake.

Tanzania tunachokosa ni viongozi wazuri kupokezana madaraka, yaani Baada ya Nyerere alipaswa aje Mkapa au Mtu kama Magufuli baada yake aje Makonda/Bashiru/Majaliwa/Mpina/Lissu kama angekuwa na malezi ya Nyerere/Mkapa au Magufuli tungekuwa sawa na China au Mataifa ya Ulaya kwa Maendeleo.

Bahati mbaya tuna sequence ya ovyo sana kwenye kuachiana madaraka, imagine Baada ya Mkapa tukapata Kikwete now tuna Samia, just imagine.

Museveni ameona hili na anataka kuwe na consistency ya Itikadi
Unaumwa mavi wewe mbwa,unapata furaha gani ukiona watu wakiteseka kwa kisingizio cha maendeleo ndiyo maana watu walifurahi sana baada ya yule mbwa mwenzenu kufa.
 
Ndio maana linchi lake likubwa lenye kila rasilimali limeachwa mbali sana kiuchumi hata na vinchi vidogo vidogo kama Japan, Ujerumani, Italia na Uingereza

Russia pamoja na ukubwa wake wote na rasilimali lukuki kushinda nchi yoyote duniani lakini inazidiwa na kanchi kadogo kama South Korea au Japan nchi ambazo kupata hata kokoto tu ni shida kama ilivyo upatikanaji wa umeme au maji katika Tanzania.

Nyie watu wengi mnaoizungumzia Demkrasia kwa kuilinganisha na nchi za Ulaya basi hamjajua vizuri historia ya Ukoloni na mikataba ilikuwa unaingia na
 
Ndugu zangu Watanzania,

Napenda tu kuwapeni taarifa wale ambao mlikuwa hamfahamu kuwa Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweli Kaguta Museveni Amemteua Mwanae Jenerali Muhoozi kuwa Mkuu wa majeshi ya Nchi hiyo. Uteuzi huo ambao una maana kubwa sana katika Taifa la Uganda na ambao umezusha maneno mengi sana kwa wachambuzi wa siasa na hata wananchi wenyewe wa Uganda.

Rais Huyo ambaye ndiye Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu sana kuliko Rais yeyote yule katika ukanda huu wa Afrika mashariki na ambaye wengi wamezaliwa wamemkuta na bado ujana wao unaelekea kuisha bado Rais wao yupo madarakani akiendelea na kazi za kuwatumikia waganda.kwa kuwa Rais huyo alizaliwa mwaka 1944 na sasa amemteua mwanaye ambaye alizaliwa mwaka 1974 kuongoza Jeshi la Uganda.

Kwa wasiofahamu pia jambo lingine ni kuwa Rais Museveni ni kama ndugu yetu tu kwa kuwa amesoma hapa hapa Nchini elimu yake ya chuo kikuu katika chuo kikuu cha Dar es salaam yaani UDSM maarufu kama Mlimani. Kozi ya sayansi ya siasa..lakini ni miongoni mwa viongozi wanaoipenda na kuiheshimu sana Tanzania na watanzania.ni kiongozi ambaye yeye na serikali yake huwezi ukamsikia akiwafanyia hujuma watanzania wala kuwawekea vikwazo vya aina yoyote ile mpakani ,viwe ni vya kibiashara au nini. Ni kiongozi ambaye anaendelea pia kumuenzi sana Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere.

Ni Kiongozi ambaye anaweza kutusaidia hata kijeshi ikiwa tupo na tumeingia vitani kupigana na nchi yoyote ile. Kwa ufupi ni kuwa uwepo wa Mheshimiwa Yoweli Kaguta Museveni madarakani ni sehemu pia ya usalama wetu katika mpaka wetu na yeye.maana hana shida na sisi wala ugomvi na sisi wala kinyongo au chuki au kisasi na sisi.ndio maana amekuwa akitupatia ushirikiano wote kwa kila jambo.Ni ndugu yetu wa Damu ambaye hawezi kutudhuru wala kututishia amani wala kutulaza macho wala kumhofia.

Tofauti na majirani zetu fulani hivi kama wawili hivi ambao kamwe siwezi kuwataja ni lazima tuishi nao kwa akili sanaaa maana hawaaminiki wala hatupaswi kubweteka wala kujisahau wala kuwaamini sana.maana hawatabiriki na wana chokochoko za chinichini na kujiona wao ni bora sana .japo sisi hawatuwezi kwa lolote lile,ndio maana tumekuwa tukiwachukulia hivyo hivyo na kuishi nao kwa akili kubwa na ya tahadhari kwa kila nyanja kuanzia uchumi,biashara,ulinzi na usalama, ushirikiano na mengine mengi tu.

Nimeona niwapeni habari hii kwa kuwa Uganda ni mshirika wetu kwa mambo mengi sana ya kiuchumi, kibiashara na mengine mengi tu.maana ni lazima ujuwe kesho nani anaweza kuja kuwa Rais wa nchi hiyo ili ujuwe mapema huyo atakaye kuja ni mtu na kiongozi wa aina gani na anamtizamo upi na msimamo upi juu ya masuala mbalimbali pamoja na vipi anaitizama nchi yetu na upi ni msimamo wake katika mambo mbalimbali.lazma ufahamu anasimamia nini na anaamini nini hasa kwa mambo yatakayogusa maslahi yetu ambayo kwa sasa tunaendelea vyema katika utawala wa Mheshimiwa Yoweli Kaguta Museveni. Siasa ni sayansi na sayansi ina kanuni zake ambazo ukizikosea huwezi kulipata jibu hata ungefanyeje.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Back
Top Bottom