Rais Museveni anapambana vilivyo na harakati za magharibi kueneza ushoga: Viongozi wetu jifunzeni kitu!!

Rais Museveni anapambana vilivyo na harakati za magharibi kueneza ushoga: Viongozi wetu jifunzeni kitu!!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477

Sheria kali dhidi ya mashoga inatungwa Uganda, hata wamiliki wa nyumba watakaokodisha kwa mashoga watakamatwa​

6 Machi, 2023

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisaini mswada dhidi ya mashoga na kuwa sheria mwaka 2014, katika ikulu ya rais ya Entebbe, February 24, 2014.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akisaini mswada dhidi ya mashoga na kuwa sheria mwaka 2014, katika ikulu ya rais ya Entebbe, February 24, 2014.
Shirikisha

Mswada unatayarishwa nchini Uganda kwa lengo la kuharamisha kabisa mapenzi ya jinsia moja, ukiwa na adhabu ya hadi miaka 10 gerezani na faini ya hadi shilingi milioni 10 za Uganda.

Mswada unawalenga watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, wamiliki wa nyumba na hoteli, wamiliki wa vyumba vya burudani, mashirika yanaoyoeneza ushoga, waandishi wa habari, watengenezaji filamu miongoni mwa wengine.

Kwa mara nyingine tena, Uganda inajaribu kutunga sheria kali dhidi ya ushoga, mara hii mswada unalenga kila mtu anayechangia kwa namna yoyote kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini humo.

Asuman Basalirwa, mbunge wa manispaa ya Bugiri, mashariki mwa Uganda, ambaye ameandaa mswada huo, ameambia Sauti ya Amerika kwamba mswada wake unalenga kuweka mazingira magumu kabisa kwa ushoga kufanyika Uganda, kwa kuwalenga wafadhini wa ushoga, wanaoeneza, wamiliki wa hoteli, vyumba vya burudani na wenye nyumba za kawaida za kukodisha.

Adhabu kwa watakaovunja sheria
Wanaoneza ushoga kwa kuchapisha vitabu, na wafadhili, watatozwa faini ya shilingi milioni 100 za Uganda. wanaomiliki vyumba vya kufanyia ushoga watahukumiwa miaka 7 gerezani huku wamiliki wa nyumba watakaokodisha kwa watu walio katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja watahukumiwa mwaka mmoja gerezani.

Mtu yeyote atakayejaribu kushawishi mwingine kufanya mapenzi ya jinsia moja atafungwa miaka 5 gerezani na atakayepatikana na makosa ya kusimamia au kubariki ndoa hizo atafungwa miaka 10 gerezani.
Waandishi wa habari, wahariri, watengenezaji filamu watakaofichua waathiriwa wa ushoga bila idhini yao watatozwa faini ya shilingi milioni 5.

Sheria ya mwaka 2014 dhidi ya mashoga ilifutwa na mahakama
Mswada wa Asuman hata hivyo una adhabu ndogo ikilinganiswa na mswada uliopitishwa na bunge mwaka 2014, kusainiwa na rais Yoweri Museveni kuwa sheria na baadaye kufutwa na mahakama kwa msingi kwamba wakati ulipokuwa unapitishwa, hakukuwa na idadi ya wabunge wanaohitajika kupitisha mswada bungeni. Sheria hiyo ilikuwa na adhabu ya Maisha gerezani.

Asuman, anasema kwamba ushoga unaenezwa na watu wanaochapisha vitabu na kufadhili vitendo hiyvo, mambo ambayo hakuna sheria katika sheria za sasa za Uganda kushughulikia hilo.

Viongozi wa dini nchini Uganda, saw ana rais Yoweri Museveni wamesema kwamba hawatakubali vitendo vya ushoga nchini humo.
 
Mungu awasimamie katika haya yanayoendelea duniani

Ila cha ajabu hata Ulaya kuna watu wengi wanapinga ingawa serikali zinalazimisha
Hata watangazaji wa radio nawasikia hawako radhi na yanayoendelea
Ila kila leo wanayaongelea sana na kuponda sana na mijadala ni mingi
 
Ni jambo jema sana , sad thing ni kwamba hatoboi
Hayo ndiyo mawazo ambayo mabepari wa magharibi wanataka tuwe nayo!! Mawazo ya kutojiamini, mawazo ya kujiona hatuwezi, mawazo ya unyonge! Kwa bahati mbaya baadhi ya mawazo kama hayo wanayo viongozi!! Tunataka viongozi mashujaa, wanaoijiamini, wasio waoga na wazalendo kweli kweli na walio tayari kupoteza maisha yao ili kulinda maslahi ya Taiofa letu!! Kwa hapa nmkumbuka JPM!!
 
Cheap populality,m7 anajua sana kucheza na akili za waganda.
 
Alitakiwa apambane zaidi kuondoa umaskini na kuimarisha demokrasia, miaka 40 madarakani ila taifa la hovyo sana.
 
Hayo ndiyo mawazo ambayo mabepari wa magharibi wanataka tuwe nayo!! Mawazo ya kutojiamini, mawazo ya kujiona hatuwezi, mawazo ya unyonge! Kwa bahati mbaya baadhi ya mawazo kama hayo wanayo viongozi!! Tunataka viongozi mashujaa, wanaoijiamini, wasio waoga na wazalendo kweli kweli na walio tayari kupoteza maisha yao ili kulinda maslahi ya Taiofa letu!! Kwa hapa nmkumbuka JPM!!
Yaaani Uganda awashinde hao jamaa? Mtu mwenyewee demokrasia kwake Bado ni changamoto
 
Sodoma na Gomorrah,
NI DHAMBI NA CHUKIZO KWA MOLA WETU, TUNAZO SHERIA ZINAZOKATAZA HAYA, TUWE MAKINI "TUSIJE KUPAZA SAUTI ZAIDI TUKAKUTA TUNAUTANGAZA KWA NGUVU BILA KUFAHAMU" TUPAMBANE NAO KIMYA KIMYA KWA SHERIA TULIZO NAZO.
 
Alitakiwa apambane zaidi kuondoa umaskini na kuimarisha demokrasia, miaka 40 madarakani ila taifa la hovyo sana.
Sijui kwanini pro US mnakatisha tamaa Sana viongozi wanaojitahidi kudhibiti ushoga! Mkiitwa mashoga mnachukia, Sasa Nini tafsiri ya ulichokoment?
 
Kuna raia humu wnaponda alichofanya museveni...inasikitisha Sana asee!! Yani hawaoni umuhimu kabisa wa Sheria Kali kama hizo... Mashoga wakubwa nyie👎
 
Back
Top Bottom