BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Rais Yoweri Museveni amesaini Sheria ya Matumizi ya Mitandao yenye vifungu vya kuwabana watumiaji mitandao endapo watachapisha au kusambaza habari zinazoikera Serikali au watu binafsi.
Sheria inatamka kuwa “Mtu yeyote anayetumia mitandao ya kijamii kuchapisha au kusambaza habari zilizopigwa marufuku na sheria za Uganda au kuficha jina lake au picha halisi, anavunja sheria"
Pia inazuia mtu yeyote kupata taarifa za mtu mwingine bila idhini, kusambaza habari kuhusu Watoto bila idhini ya mzazi, kutuma au kusambaza habari zenye uchochezi, na kutuma au kusambaza habari ambazo zinaweza kuwa za kuharibu sifa ya mtu.
====================
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesaini mswada wa matumizi ya mitandao ya kijamii na kuwa sheria na hivyo kuwaweka watumiaji wa mitandao hiyo katika hatari ya kufungwa hadi miaka 5 gerezani endapo watachapisha au kusambaza habari ambazo zinaikera serikali au watu binafsi.
Sheria hiyo yenye utata imetajwa na wanaharakati wa kutetea uhuru wa kujieleza na habari kuwa ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza.
Mojawapo ya vingele kwenye sheria hiyo inahusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kikao cha bunge mwezi Septemba.
Museveni amesaini sheria hiyo alhamisi wiki hii.
“Mtu yeyote anayetumia mitandao ya kijamii kuchapisha habari, kusambaza habari ambazo zimepigwa marufuku kulingana na sheria za Uganda, or kuficha jina lake au picha halisi, anavunja sheria,” inasema sheria hiyo mpya.
“Anayechapisha habari kwenye mitandao ya kijamii au kusambaza habari iliyochapishwa, anawajibika. Iwe ni mtu binafsi au shirika,” inaendelea kusema sheria hiyo.
Inaweka marufuku kwa mtu yeyote kupata taarifa za mtu mwingine bila idhini, kusambaza habari kuhusu Watoto bila idhini ya mzazi, kutuma au kusambaza habari zenye uchochezi, na kutuma au kusambaza habari ambazo zinaweza kuwa za kuharibu sifa ya mtu.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu habari na mawasiliano Moses Magogo, amesema sheria hiyo ilitungwa kwa kuzingatia haja ya kuilinda kila mtu anayetumia na asiyetumia mitndano ya kijamii na kwamba Maisha ya watu yamekuwa yakiingiliwa na watumizi wa mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, wakosoaji wanataka sheria hiyo kufutwa, wakisema kwamba inakandamiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.
Sheria hiyo ilipitishwa na bunge Septemba 8, 2022. Inatoa kifungo cha hadi miaka 5 gerezani au faini ya dola 2,619 (Shilingi milioni 10 za Uganda) au kufungwa jela na kulipa faini kwa Pamoja.
Sheria hiyo inalenga watumiaji wa mitandao yote ya kijamii kama YouTube, WhatsApp, Facebook, Instagram, Twitter, WeChat, TikTok, Sina Weibo, QQ, Telegram, Snapchat, Kuaishou, Qzone, Reddit, Quora, Skype, Microsoft Team na Linkedin.
Mnamo mwaka 2018, serikali ya Uganda ilianzisha tozo ya kila siku kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Baada ya hatua hiyo kufeli, serikali ilianzisha tozo ya asilimia 12 kwa mtu yeyote anayenunua kifurushi cha internet.
Serikali ya Uganda imekuwa ikifunga mitandao ya kijamii na huduma ya internet kila mara hasa wakati wa uchaguzi.
Mtandao wa kijamii wa facebook ulifungwa Januari 2021 ulifungwa kutokana na amri ya serikali, lakini raia wa Uganda wamekuwa wakitumia mfumo wa siri wa kupata facebook, maarufu VPN.