Zanzibar 2020 Rais Mwinyi amuapisha Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar. Maalim Seif asema haukuwa uamuzi rahisi

Amakweli, njaa ina nguvu kuliko msimamo thabiti.
 
Imeisha Hiyo!!
 
Waislamu waungwana sana niliona kwa Alli, Shein, Jakaya na SASA Hussein maadili ya dini Yao yanawafanya wasiwe wanafiki WA kupitiliza kama Marais Wakiristo. Naamini Hussein atakuwa Rais muungwana na kuleta mabadiliko.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapigiwa kura na wananchi hateuliwi na Rais

Kule Znz Seif kateuliwa na Rais wa Znz wakati Samia aliteuliwa na Wananchi
Samia kateuliwa na chama kabla ya kupigiwa kura
 
Na kiyoyozi juu. Hii ni ithibati kuwa mwanasiasa sio kiumbe cha kukiamini hata siku moja.

Ila cha ajabu uchaguzi ukifika tena wale wale walalahoi watasapoti hawa hawa wanaotughilibu kwa manufaa yao binafsi.
CHADEMA pamoja na mapungufu yao lakini wana nafuu siyo hivi vyama lishe
 

Sawasawa tujali maslai ya Wananchi pamoja na Taifa ya leo na kesho.
 
Aliteuliwa kuwa Mgombea Mwenza sio kuwa Makamu wa Rais

Makamu wa Rais huchaguliwa sambamba na Rais kwny sanduku la kura
Samia kateuliwa na chama kabla ya kupigiwa kura
 
Nin
Ninajiuliza maswali haya;
Kweli maridhiano yanaweza kuwa yamekubaliwa na watu wakameza machungu ya uchaguzi na chaguzi zilizopita ili Zanzibar ijengwe LAKINI JE? YALE MAJAMBAZI YALIYOFANYA UHALIFU DHIDI YA UTU PEMBA NA UNGUJA YANACHUKULIWA HATUA GANI? JE WALE WALIOFUNGULIWA MASHTAKA FEKI, WALIOUAWA AMA KUJERUHIWA KATIKA KADHIA HIYO WANAPEWA NAFASI IPI?

Inapaswa hatua zichukuliwe dhidi ya uhalifu ili jinai zile za kishetani zisijirudie tena na waliobambikizwa kesi wasafishwe hadharani na SMZ ikiri hadharani kutorudia kuua raia wasio na hatia kwa sababu za kivyama au ule "upuuzi" mwingine.
Kinyume na hivyo hayatakuwa maridhiano bali mashabikiano ya kimaslahi.
 
Uamuzi uwe rahisi , usiwe rahisi yeye ni msaliti , vipi yeye na Zitto na ile kesi ya ICC wamepatanaje na maccm wanaenda kuifuta ?
 
Wanasiasa mnatukera mjue!

Kauli zenu bakini nazo moyoni. Unapotuambia tusamehe na kisahau na tupokee mkono wa maridhiano kiwepesi tu hivi mnatufikiriaje?

Niwashauri kitu ili tuone mko serious na maridhiano

1: kauli zenu ziende sambamba na kuwatambua na kuwafungulia mashitaka waliofanya uhalifu.

2: Familia na wahanga wote wa siasa za 2020 watafutwe, watambulike na wafutwe machozi

3: Serikali ijitokeze kuomba msamaha kwa jamii kuwa ilitenda sivyo na wale kiapo cha kujutia na wako ladhi kutafuta malidhiano kitaifa.

4: Wapatanishi na wanaotaka maridhiano watambuliwe na kumbukumbu iandikwe.

5: liweko tamko la kuuhakikishia umma kuwa proactively tutafanya liwezekanalo makosa ya namna hiyo kutojirudia na kuweka msingi wa kikatiba kulinda matakwa kama hayo.

Nje ya hapo nauona usanii tu

Mbali na hapo mimi naona ni unafiki tu mnaojaribu kutuelezea.
 
Waliovunjwa miguu walifatwa majumbani mwao?? Usiko tii sheria utashurutishwa...hebu geukia kwa mzee hapo uganda amesemaje kuhusu raia wanaorushia mawe polisi?? Nchi yetu ina amani hadi imepitiliza

Umeongea utoto gani dogo? Kuna watu nyumba yao imepigwa bomu. Halafu tofautisha amani na uoga uliopitiliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…