Acheni Wivu
Ni Zamu Wa Zenj.
Mbona Mwendazake alikuwa anamtuma Bashite
Bashite kama mkuu wa mkoa alimwakilisha wapi raisi wa JMT nje ya mipaka ya nchi ya Tanzania? Kama kwenye mkoa aliokabidhiwa sawa, napo mamlaka yake yana mipaka, wanasema bila kuathiri vifungu vingine vya sheria mama.
Kwa maana hiyo rais kavunja katiba ?
Wajuvi wa sheria ya katiba wa wanaweza kuweka neno sahihi hapo, kama imevunjwa au imetamatishwa. Ila kwa maono yangu, sioni mwanga ukiingia kwenye karavati(tunnel) nililopo, hivyo bado ni giza mno, ngoja niendelee kukaza mwendo, pengine mbele huko nitaanza kuona mwangaza na kupata tumaini la kutoka kwenye hili tunnel na kujua huko nje kukoje ili nichague mwelekeo utakaonipendeza.
Wanafunzi wanapiga kelele darasani, monitor wa darasa hajulikani, mwalimu aliwaambia wanafunzi yeye hawezi kutumia fimbo wala ukali wa sauti, wanafunzi ni waelewa, hivyo akiwaambia wataelewa na wamuelewe hivyo.
Andika majina ya wapiga kelele darasani, waliofeli ni viboko, watoro waadhibiwe, mimba za utotoni fukuza mwanafunzi na weka jela mtia mimba, usafi wa mwanafunzi ukikaguliwa kila alhamisi, mchaka mchaka kila asubuhi kujiweka fiti kwa masomo ya siku nzima, wimbo wa taifa kuimbwa kila siku tukiwa mstarini kuongeza hamasa na ile sense of ownership, uzalendo.....n.k
Nimekumbuka enzi za shule ya msingi Nanjilinji.
Kazi iendelee